Tume ya Taifa ndo kiini cha viongozi wasiojali Wananchi

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,225
Kama tungekuwa na Tume Huru ya uchaguzi, tungepata viongozi bora..

badala yake Tuna watawala wanapatikana kwa njia ya Rushwa na kuchakachua kura.

Kama kiongozi anajua kuwa hana haja na kura za wananchi, anajua kuwa atapata uongozi kwa rushwa ama kwa kuchakachua tutegemee nini??

Je wakati tume ya kukusanya maoni inaendelea na kazi, je kwa nini Tume ya Uchaguzi isivunjweeeee....

KWanini hii Tume ya uchaguzi iliyokosa uhalali, iliyolalamikiwa katika uchaguzi wa 2010 bado inaendelea?

Nini kiini cha kudai katiba mpya......


je kama katiba mpya isipokuwa tayari kabla ya uchaguzi wa 2015, je tutafanyaje???
 
Ndugu mawazo yako ni sahihi lakini wao wanajua kuwa msitu ni uleule, miti ni ileile na nyani ni walewale hivyo wanajua hakuna jipya toka kwa watz
 
Ndugu mawazo yako ni sahihi lakini wao wanajua kuwa msitu ni uleule, miti ni ileile na nyani ni walewale hivyo wanajua hakuna jipya toka kwa watz

Mkuu hii ni tume ya ccm kwa faida ya ccm kwahiyo kuivunja ni ndoto.Ila kila kitu kina mwanzo na mwisho. Wakati utafika na tume itavunjwa.
 
Ni kweli ndg,matatizo yote yanayotukumba sasa yamesababishwa na hii tume kuchakachua kura na kututangazia viongozi wara rushwa!
 
Mkuu uko sahihi, inabidi watanzania wapenda amani na maendeleo tutafute mwarobaini wa hii kansa.

Vinginevyo hii kansa-tume ya uchaguzi-itatusababishia maafa makubwa

Mficha ugonjwa mauti humuumbua!
 
Sasa watanzania tufanyeje ili hii tume ivunjwe kuanzia sasa bila kusubiri madhara zaidi

Tume ya uchaguzi hawataki hata kuboresha daftari la wapiga kura
 
Tujadili Muundo Wa tume Huru ya uchaguzi

Tujadili endapo 2015 tutumie electronic voting system kama Ghana na Kenya
 
Tujadili Muundo Wa tume Huru ya uchaguzi

Tujadili endapo 2015 tutumie electronic voting system kama Ghana na Kenya

Mkuu Mpadmire,

Hakika Umeona chazo cha uongozi mbaya Tanzania kinapoanzia. Tume ya Taifa ya uchaguzi ni janga la Taifa 2015 kama hakuna marekebisho yoyote ya kikatiba yatakayokuwa yamefanywa.

Ninachokiona, watawala kwanza wameona kuchokwa kwao na watanzania: Ili wasalie madarakani kwambinu zao za kizamani hawatafanya marekebisho ya Tume! pili wataendelea kuchokonoa mgogoro wa Malawi for their own intention na tatu mchakato wa katiba utacheleweshwa.

Bila kusema mengi, Tume ya uchaguzi ya Taifa ndo itakuwa kisababishi kikubwa cha uvunjifu wa amani 2015. I really sense it and I see the fire out of Tume ya uchaguzi.
 
Hakika Mkuu Mutakyamirwa ---...2015 litatokea la kutokea tu iwe Mzozo na Malawi, ama kutokamilika katiba, na mengine tu ili mradi mafisadi wapone na waendelee kushika Dola.

hapo wananchi wataendelea kuumia zaidi na tutakuwa masikini kuliko Somalia.... People will be desperate na tutazalisha wakimbizi after 2015.
 
Nimeanza kuona mapicha picha hii tume ya rasimu ya Katiba Mpya
 
Hii tume ya uchaguzi ndo imeleta Viongozi wenye fedha uswisi, Viongozi wasio sikiliza kilio cha wananchi
 
Back
Top Bottom