Tume ya Mipango, wanapanga nini?

Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,447
2,000
Wakuu nawasalimu kwa kuwatakia amani na mwisho mwema wa mwaka 2013.
Tukiwa tunamaliza mwaka 2013 nimeona nije na mada inayohusu Tume ya Mipango na mipango yake.
Ukisoma hapa utaona mapendekezo ya Mpango wa maendeleo ya Taifa mwaka 2014/15http://www.mipango.go.tz/documents/Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2014-15.pdf

Ukiisoma hiyo document haina tofauti na bajeti za wizara au hotuba za wanasiasa wanazotoa kila mwaka bila kutekelezeka.Mimi sio mchambuzi mzuri ila ntajitahidi nieleweke.

Riporti hii ina mapendekezo mengi sana. Huwezi kuwa na mipango mingi kwa muda wa miaka miwili ukidhani utayatekeleza kama mipango yenyewe inategemea nchi wahisani na mikopo kutoka nje.

Nchi kama Tanzania tuna rasilimali za kutosha kama Madini,gesi na utalii nk. Ntajikita katika machache kulingana na upeo wangu na jinsi ninavoona kwa wenzetu.

Madini...
kwanini tusiwe na mipango ya kuwajengea wazalendo uwezo wa kutafiti na kuchimba madini yetu wenyewe? mzalendo anaweza kuingia ubia na kampuni za nche,serikali ikawa ndio operator wa madini yanayochimwa, kodi ilipwe walau 25% income tax na 40% special tax.. wako wazungu na wageni walio machimboni na kwenye migodi yetu. Serikali haifadiki na kodi zao kwani mishahara yao hulipwa katika nchi zao na sio kupitia bank za Tanzania. wanakuja wataalamu wa world bank kufanya kazi nchini, wanaishi nchini tunawachekea.
Mgeni anaishi nchini bila kulipa kodi tunaona kawaida sana huku tukikimbizana na kodi za bia,soda na sigara katika bejeti ya nchi..Mipango hamjui hili?
hao wageni migodini wanaolipana UDS 20,000 and above angelipa kodi kiasi gani kwa mwezi kama sheria ingewabana mishahara yao ipitishwe bank za Tanzania ili ikatwe kodi?Tungepata fedha nyingi sana katika pato la taifa. kwanin tunawachekea??


Sekta ya Anga.
Sekta ya anga ni muhimu sana katika ukuaji wa nchi.Tunahitaji ndege walau 10 zenye kukonect Tanzania na nchi za afrika na ulaya. nchi inaweza kujipanga tukapata Boeng 777 hata 2 tukiamua wakaingia ubia na KLM ili watalii wanaokuja nchin waje kwa ndege zetu faida ibakie kwetu.Tuangalie wenzetu Kenya,waliona mbali sana. waliimarisha sekta ya anga kwa sababu hiyo.KIla asbh na jioni zipo ndege za KA zinazokwenda na kuleta watalii na wale waanounganisha ndege kwenda sehemu zingine.Sasa wana ndege inayokwenda Amsterdam Nchi za Asia.. Safari hizo zinawaingizia fedha za kutosha za kigeni na ajira kwa wananchi wao,wao hawakujikita kujenga viwanja vingi vya ndege na kuviita international kama sisi tnavokazana na viwanja lakini ndege hatuna na uwanja wa Dar tunawaza kuupanua kwa kiwango cha kizamani.

.Haina haja kwa waziri mkuu kuomba mashirika ya China yaje kuchuma fedha zetu wakati tunaweza kuanzisha yetu wenyewe. Wakenya wana nini nasi tushindwe? Tukishaweza hapa tuangalia sasa namna ya kulink uchumi wetu na sekta ya anga.

Uwekezaji wa ndani na Nje
Suala lingine ni kutafuta maeneo ya kuwekeza nje ya nchi na kuwapatia fursa wafanyabiashara wa kitanzania. Tuangalie wenzetu Kenya,walitafiti nchi kama Sudani,wafanyabiashara wao walianza kwenda huko, baadae KCB bank ikawafuata na Kenya Airways ikawafuata pia.Mikopo wanapata KCB,wananchi wao zaidi ya 30,000 walipata ajira Sudan. walikuwa na vision hiyo.Serikaliinaweza kuwafungulia milango wananchi wake sehemu kama hizo mfano Congo,Comoro nk.

Kilimo
Katika kilimo kuna maeneo makubwa sana Tabora hadi Kigoma ambayo yanafaa sana kwa kilimo.Ipo mito ya kumwagilia.wajengeeni vijana uwezo wapeni mikopo ya kuanzia,wapeni yale matrekta yanayoozea pake JKT wakayatumie kule, Mifereji inaweza kujengwa watalima mpunga,matunda na vyakula vingine.wawekeeni miundo mbinu mizuri kama umeme na barabara na makazi...inawezekana sana..Mipango tu.

Estates
Kuhusu makazi Tanzania tumelegea sana katika kuanzisha estates..Ukiangalia muda mwingi wa wafanyakazi wanautumia barabarani, Kwanini sekta binafsi wasipewe uwezo na wakapewa maeneo wakajenga estates watu wakanunua kwa malipo ya miaka 30 na kuendelea kama nchi za wenzetu au wakapanga? maeneo kama sinza,msasani,masaki,upanga maeneo yote wanayoishi mtu mmoja moja waondoshwe wenye uwezo wa kujenga estates wawe joint venture na NHC ili kuwaleta watu karibu na mji na kuwawekea miundo mbinu kama barabara,umeme na maji na maduka ya vyakula...wenzetu kenya wameweza kwanini isiwe sisi?

serikali haiwezi kila kitu,mipango tunayopanga haitekelezeki kwa kuwa hatuko makini,tumebaki kuwa wanasiasa.
Tuwe na mipango michache kila mwaka na tuwe na uhakika wa kuitekeleza.Inawezekana sana tukiwa na watu makini.

Mwenye nyongeza ya mipango gani serikali itoe kipaumbele tushirikishane hapa tuiamshe hiyo Tume ya Mipango ili waache kufanya kazi kwa mazoea tuone matokeo


 

Deo Corleone

JF-Expert Member
Jun 29, 2011
15,718
2,000
Inapanga mipango mikakati na upembuzi yakinifu a.k.a feasibility study na michakato
 

Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,108
2,000
Mpwa ukiuliza sana utaishia kupata uchizi. Jiulize ni kazi gani PCCB au Presidential Delivery Unit...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom