Tume ya Mawasiliano: Wizi wa Makampuni ya simu hadi lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume ya Mawasiliano: Wizi wa Makampuni ya simu hadi lini?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by kukomya, Dec 23, 2011.

 1. kukomya

  kukomya JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 344
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Mimi naishi Mkoani Kigoma umbali wa kilometa zaidi ya 200 toka moja ya wilaya za Mkoa huo na ni mtumiaji mzuri tu wa huduma za mitandao yetu hii. Mitandao miwili ndiyo inayopatikana hapa ninapoishi; yaani Airtel ninayoitumia pia kwenye mawasiliano ya internet na Vodacom kwa mawasiliano ya kawaida na mara chache kwa mawasiliano ya internet.
  Nimehuzunishwa mno na wizi wa waziwazi unaofanywa na Makampuni haya kwa wateja wao. Kwanza nianze na Vodacom. Kipindi fulani kilichopita nilikuwa na utaratibu wa kununua vocha kupitia NMB Mobile lakini niliacha mara moja baada ya kugundua wizi wa waziwazi, kwani unapoanzisha muamala wa kutaka huduma ya kununua vocha kupitia Mobile ATM hawakuhudumii hadi uwe na salio si chini ya 200/=, sasa siku niliyoumia zaidi ni pale simu yangu ilikuwa na salio la 2000/=. Nilipojaribu zaidi ya mara tano kutaka kununua sh. 2000/= kwa matumizi ya dharura toka eneo ambalo hakukuwa na huduma za kununua vocha na mara zote niliambiwa nijaribu tena kutokana na makosa kwenye mtandao. Mara ya mwisho niliambiwa sina salio la kutosha huduma ninayotaka! Alas, kuangalia salio nilibakia na Sh 4/=! Niliwapigia 100 ambapo baada ya kunizunguusha sana mpokeaji aliniomba tu radhi na kuniambia wengi tu wanalalamika lakini ule ndiyo ulikuwa utaratibu. Alimaliza kwa kunishukuru kwa "Kuendelea kuitumia huduma ya Vodacom" Je ni halali kukatwa fedha kwa huduma waliyoshindwa kunipa? zipo pia kero nyingi toka kwa wezi hao ambazo si rahisi kuziorodhesha.
  Na sasa twende kwenye dhulma ya Airtel. Nao kama Vodacom wanatoza fedha kwa huduma hewa ila wao wanakata moja kwa moja Benki yaani hata kama huna salio "Watakupa" huduma lakini ukienda kuchukua Bank Stetement utaamua kuachana nao. Kilichoniuma zaidi kwa hawa Airel ni kwa zaidi ya mara tano sasa napoteza fedha kwa vocha zao kushindwa kuingia na kuwapigia wanisaidie kuziingiza ikibidi kwa kucheki na namba za 'Control' zinazoandikwa pembeni mwa vocha; jibu lao ni "Nenda kwa wakala aliye karibu ili akuingizie". Jibu hili ni la kihuni na kishenzi kwa mtu kama mimi ninayetumia huduma yao nikiwa zaidi ya kilometa 200 toka kituo chao cha "karibu" cha huduma ambako hata hivyo ukienda watakwambia mawasiliano na maopereta wa Airtel ni magumu, huchukua muda mrefu mno - hadi nusu saa kuweza kujibiwa hivi kumaliza chaji zao. Je ni mantiki kumshauri mteja kama mimi eti nifunge safari ya nauli ya zaidi ya 20,000/= kufuata huduma ya kuingiziwa vocha ya Sh. 500/=, 1000/=, 2000/= au hata 5,000/=?
  Naandika mada hii nikiamini tuko wengi tu tunaonyanyasika nao na ndiyo maana nimeweka jamvini tuijadili na kama wapo wanaotoka tume ya mawasiliano au serikalini wanaopita humu watusaidie.
  Je ni nani anayechukua dhamana ya mabilioni ya fedha yanayoshikiliwa na watu hawa ambao uaminifu wao ni wa kutiliwa shaka?

   
 2. i

  iMind JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Pole sana ndugu. Kimsingi yapo mambo mengi tu yanayokera katika huduma hizi za makampuni ya mawasiliano. Bahati mbaya sana TCRA ni kama wako likizo. kazi yao ni kutoa leseni tu na kugawana $ tu
   
Loading...