Tume ya Maendeleo ya Ushirika imechangia upotevu wa matrilioni ya fedha za umma, Kassim Majaliwa kwepa mtego huu

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,014
8,364
Nawasalimu kwa salamu ya mama yetu:

Kwa wale msiopenda kusoma nyuzi ndefu ntajitaidi kuwakwepa mapema.

Taifa la Tanzania lipo katika mtanzuko mkubwa hasa pale Taaluma inapogaragazwa na kundi la WANASIASA tena wanasiasa wachumia tumbo ambao ndio waliojaa kwenye vyombo vya maamuzi.

Mfano,mwaka 2018,Bunge chini ya Ndungah lilitunga sheria ndogo ya fedha,nikili wazi nilikuwa mmoja wa wadau walio toa maoni kwenye sheria hiyo.

Kimsingi sheria hiyo haina tatizo kubwa ni nzuri na kwakweli ingetekelezwa na wasomi tulio waamini ingesaidia taifa ila sasa wasomi wetu wanaogopa wanasiasa kwa kweli niseme WASOMI wetu waliopo tume ni waoga sana.

Kupitia sheria hiyo ilielekeza usajiri wa wa taasisi za kifedha mathalani VYAMA VYA AKIBA NA MIKOPO( SACCOS) zisajiliwe na kupewa Leseni kupitia Tume ya maendeleo ya ushirika nchini.

Ili vyama viweze kupewa leseni kuna vigezo vilivyowekwa hapo na wataalamu wety, VIGEZO hivyo vimepelekea vyama zaidi ya 5000 kukosa sifa za kupewa leseni

Twakwimu hizi ni kwa mujibu wa data base ya Tume ya maemdeleo ya ushirika,ya mwaka 2016_17 ilionesha yakuwa kuna jumla ya vyama vya Akiba na mikopo zaidi ya 6000 leo hii ukiingia kwenye orodha ya SACCOS zilizopewa leseni ni saccos 349 HAPO unajiuliza je ni asilimia ngap ya orodha waliyonayo?

JE, SERIKALI ITAPOTEZAJE FEDHA ZAKE?

katika ili nianze kwa kutoa angalizo kwa Mh Waziri Mkuu ambae atakuwa Mgeni Rasmi katika siku kufunga siku ya USHIRIKA DUNIA AMBAPO KWA TANZANIA INAFANYIKA MKOANI TABORA.

kutokana na mashariti au sifa zilizowekwa na watumishi wa Tume pamoja na Bunge lilirotunga sheria hiyo,Asilimia kubwa ya vyama vya Akiba na mikopo kwa maana ya SACCOS zilizokopeshwa MABILIONI YA JAKAYA VIMEJIKUTA HAVINA SIFA HIZO NA VYOTE VIMEKOSA LESENI KUTOKA TUME.

Maana yake ni kuwa MABIIONI hayo yote ndo yamepotea kusiko julikana ilihali walio zichukua fedha hizo wapo na wengine ni watumishi wa umma.

Moja ya sifa iliyopeleka vyama hivyo kukosa leseni ni MTAJI, kimsingi vyama hivi si kwamba havikuwa na mtaji bali mtaji wa vyama hivi upo na unashikiliwa na BENK ya ushirika kwa maana ya CRDB, IKUMBUKWE mabilioni ya Jakaya yalipitia benk hiyo na,benk ya kilimo.

Benk hizo kwa kipindi kile zilielekezwa kuweka Akiba kwenye Mabenki hayo tajwa ili viweze kupewa mkopo, vingi viliweka fedha nyingi uko na kupewa mkopo, Akiba walizo weka zilikuwa sehemu ya Dhamana ya mikopo yao.

Baada ya vyama vingi kushindwa kurejesh kwa wakati mabenki tajwa hapo juu yalizikomba Akiba za vyama hivyo mwishowe sasa vinakosa sifa.

YAWEZEKANA nisieleweke, ebu labda nitoe mifano halisia.

MKOA WA MWANZA;

Kuna saccos inaitwa WADOKI sacco Limited,ipo maeneo ya ccm kirumba Saccos hii kwa mujibu wa mikataba ilikpeshwa BILIONI 3,ILA kwenye akaunti za chama iliingizwa BILIONI MOJA NA NUSU, ILIYOBAKIA ILIPIGWA NA WATUMISHI WA TAASISI TAJWA HAPO JUU PAMOJA NA NSSF ili linajulikana wazi,pesa zilitoka crdb,TIB , NA NSSF, Shangazo mkoa ulikuwa na mrajisi hapo alitoa ukomo wa madeni kila alipofatwa,uzuri ni kuwa yeye amekufa na 40,000,000/= ni kaela kadogo haka.

Chama kimenyimwa leseni ili mabilioni yote yale yapotee serikali kweli mmeamua hivo au kuna mkonio wa walio tafuna mabilioni haya nyuma yake?

MWANZA SACCOS LTD,pale kuna mkopo wa zaidi ya 1.2 BILIONI kutoka kwa wadau tajwa hapo juu, chama kimenyimwa leseni na hakitakiwi kufanya kazi yoyote ikiwemo kufatilia madeni.

VICTORI saccos LTD; zaidi ya 1.5 BILIONI, chama kimekosa leseni pesa inapotea hii,

SENGEREMA SACCOS LTD; zaidi ya MILIONI 800,000,000/= chama kimekosa leseni pesa inapotea hiyo.

Huu mfani wa vichache,mkoa wa Mwanza

MKOA WA GEITA

1. GEITA SACCOS LTD; MILIONI 900,000,000/= zipo mikononi mwa wadaiwa sugu, chama kimekosa leseni wadaiwa WAMECHINJA wanaserebukA.

2. USHIROMBO SACCOS LTD; chama kinadaiwa zaidi ya MILIONI 800,000,000/= chama kimekosa sifa na kimekosa Leseni PESA zinapotea hizi.

3. MASUMBWE SACCOS LTD; DENI ni zaidi ya milioni 600,000,000/= wakopeshaji ni taasisi za serikali pesa zinapotea hizi kisa chama hakina leseni na hakiruhusiwi kutoa huduma yoyote.

Hapa ni mifano tu, ba ndungu hali inatisha

MKOA WA MOROGORO:

1. UDZUNGWA SACCOS LTD, BILIONI 1.5 Kutoka TIB N CRDB, chama hakina leseni na kimeambiwa kisiendelee na kazi yoyote ya kiushirika,pesa zinapotea,pia iki chama kinajengo la ofisi wananchi wanataka jengo liuzwe wadaiwa wagawane chao mapema.

MKASU SACCOS LTD; hapa kuna kamchezo kazuri chama kilikopeshwa na TIB kilikopa MILIONI 600,000,000/= ILA MIA MBILI alikula mshikaji mmoja mhasibu wa Tib Liko wazi hata mimi sifileo nalijua ili chama kimekosa leseni, chama hakitakiwi kutoa huduma yyte fedha zipotee potelea kote.

KIMAKIMU SACCOS LTD, hapa kuna zaidi ya MILIONI 300,000,000/= OFISI zilizhafungwa wadaiwa wapo na ni makada.
TURIANI SACCOS LTD ZAIDI YA BILIONI 1.4B.chama hakina leseni kinatakiwa kuacha mara moja kutoa huduma yoyote kwani hakina leseni.

MKOA WA PWANI

1. MLANDIZI SACCOS LTD, hapa kuna zaidi ya BILIONI moja, chama kimekosa leseni, chama kina jengo la ofisi, na mashamba ekari zaidi ya 300, wadaiwa baada ya chama kukosa leseni wanataka vyote viuzwe wagawane chao mapema.

Kwa upande wa mkoa wa DSM naomba nisiandike lolote hali ni mbaya sana mkoa kwa ujumla unazaidi ya TIRIONI 4, zipo kwenye vyama vya akiba na mikopo, na waliokula pesa hizo ni MAKADA tusiwaguse kabsa Mh Waziri Mkuu hapo ni pamoto sanaaàa.

PONGEZI KWA HAYATI MAGUFULI vs KASSIMU MAJALIWA NA SAMIA SULUHU HASSANI ENZI ZILE.

Kimsingi Mh Rais ambaye sasa ni hayati, alitambua kabsa kuwa kuna fedha nyingi mikononi mwa wanachama wa vyama hivi vya akiba na mikopo, na yeye alitilia mkazo fedha hizo zilipwe, kwa maana ya wadaiwa wazirejeshe na kwakweli suala la MADENI KATIKA VYAMA VYA USHIRIKA alilipigia chapuo,huku akisaidiwa na MH kassimu Majaliwa.

Na ninaimani hata sheria ndogo ya fedha ilitungwa ili kuwezesha fedha hizi zisipotee changamoto watekelezaji wa sheria hiyo ndo kuna changamoto tena changamoto inayoonesha kidogo ukosefu wa uchungu wa fedha za umma.

RAI YANGU KWA WAZIRI MKUU KASSIMU MAJALIWA:

Nimwombe yeye awaulize watumishi wa Tume ya maendeleo ya ushirika ni vyama vingapi ambavyo vimepewa LESENI NA VINAFEDHA ZA UMMA? najua swali ili ni chungu kwao ila ni muhimu sanaaa vinginevyo,mabilioni ya fedha za umma yatapotea.

CHANGAMOTO YA KUTOKUTOA LESENI KWA VYAMA:

1. Vyama vingi vilivokosa leseni na vinamali zisizohamishika vingi wanachama wanataka MALI ZAO ZIUZWE wagawane,chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa wadaiwa SUGU.mifano hapo ni mingi sanaa.

2. Vyama havina leseni, na havitakiwi kutoa huduma yoyote ile hii ni kwa mujibu wa barua nzito iliyoandikwa kutoka tume.imepelekea wadaiwa kushangalia sanaaaaa.

Swali tunduzi: JE, SERIKALI IMEKUBALI KUPOTEZA FEDHA HIZI?

JE, WAZIRI MKUU, MBONA UMEPOTEA HUONEKANI,UKISISITIZA FEDHA ZIRUDI, KAMA AMBAVYO ULIKUWA UNAFANYA HAPO NYUMA?

Nawatakia kila la kheri.

Sifileo kutoka Marangu.
 
Ahsante Sifi leo umetekeleza wajibu wako kizalendo, ujumbe utawafikia wahusika na wao watatizama nini na wapi pa kuanzia.
 
Back
Top Bottom