Tume ya madini, kampuni ya meli wapewa bil 17/-

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
SERIKALI kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, imetoa Sh bilioni 10.7 kwa Tume ya Madini nchini na Sh bilioni 5.9 kwa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimkakati, yenye lengo la kuongeza mapato yanayotokana na madini pamoja na kuiwezesha Kampuni ya Huduma za Meli kujiendesha kibiashara.

Haa ya utiaji saini mikataba ya fedha hizo umefanyika Dodoma kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dotto James na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk Leonard Chamriho.

James alisema Sekta ya Madini na Kampuni ya Huduma za Meli, wajifunze kupitia miradi mingine ya kimkakati katika halmashauri zilizopewa fedha, ili kuepuka changamoto mbalimbali zilizojitokeza kwa baadhi ya halmashauri kushindwa kukia malengo.

“Fedha hizi sio za bure tutazifuatilia mpaka shilingi ya mwisho, ili kupata mrejesho wa kuchangia maduhuli katika Mfuko Mkuu wa Serikali, hivyo fedha hizo zinatakiwa kutumika kwa ufanisi kwa lengo lililokusudiwa”, alisisitiza James.

Alisema Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imeunda kikosi kazi maalumu ambacho kitakuwa kinafuatilia maendeleo ya miradi hiyo na kutoa taarifa serikalini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Msanjila aliishukuru serikali kwa kuwapatia fedha hizo na kuahidi kuwa watazitendea haki na kuongeza mapato ya serikali.

“Tumepewa lengo la kukusanya maduhuli ya kiasi cha shilingi bilioni 475 katika mwaka huu wa fedha 2018/2019, nina kuhakikishia kuwa lengo hili tutalikia kwa sababu ya uwezeshaji huu wa serikali na mwitikio mzuri wa wadau wa sekta ya madini katika kulipa kodi kwa hiari,” alisema Profesa Msanjila.

Alisema kuwa sekta ya madini ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa nchi, uwezeshaji huo utawezesha kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiikumba Tume ya Madini kwa lengo la kuongeza ukusanyaji wa mapato yanayotokana na madini.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, alisema kuwa uwezeshaji huo utaiwezesha Tume hiyo kukia lengo na kuahidi kuendelea na juhudi za kuhakikisha maduka ya madini nchini yanaboreshwa. Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk Chamriho, aliishukuru serikali kwa kuipatia Kampuni ya Meli nchini (MSCL) kiasi cha Sh bilioni 5.9 zitakazotumika kukarabati baadhi ya meli zilizopo pamoja na kuweka mifumo ya kielektroniki ya kukusanya maduhuli ya serikali.

Aidha, Osa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli, Eric Hamissi, aliahidi serikali kuwa hawatoiangusha na kubainisha kuwa kampuni hiyo ni ya kimkakati na inaweza kuchangia uchumi wa nchi.
 
Back
Top Bottom