Tume ya Maboko ni ya kisiasa zaidi haiwezi kuwa na jibu la matatatizo ya wanafunzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume ya Maboko ni ya kisiasa zaidi haiwezi kuwa na jibu la matatatizo ya wanafunzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Njaare, Feb 7, 2011.

 1. N

  Njaare JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama kawaida ya JK, ili kupoteza muda ameteua tume itakayochunguza matatizo ya bodi ya mikopo. Tutakumbuka uteuzi wa tume alioufanya toka ashike madaraka haujawahi kuwa na manufaa kwa watanzania. Kwa mfano tume ya Mtukamazina kuhusu masilahi ya wafanyakazi na tume ya Jaji kuhusu madini. Hata hivyo tume hizo zilikuwa na watu makini ambazo ziliwapa matumaini watanzania kuwa taarifa watakayotoa kama ikifanyiwa kazi.

  Hii tume ya sasa iliyoundwa, inamuweka mmojawapo wa watuhumiwa kuchunguza matatizo ambayo hata yeye ameyachangia.Kwa hili la kumteua Prof. Maboko kuwa mwenyekiti mimi naona ni kuwa JK kachemsha kwani hata juzi bodi imevituhumu vyuo kuwa navyo vimechangia matatizo.

  Na mimi naungana na bodi kwa sababu Vyuo ndo huwa vinapendekeza gharama za mwanafunzi bila kufanya utafiti wa kutosha kuhusu gharama halisi. Bodi pamoja na wadhamini wengine huwa inamlipa mwanafunzi kulingana na vyuo vinavyopendekeza. Hii inaathiri hata wanaojilipia kutoka vyanzo vingine. Angalia prospectus za vyuo hasa UDSM ambapo Prof Maboko ni msimamizi wa taaluma utakuta wamependekeza mwanafunzi apewe 5,000/= wa masters apewe 10,000/= kwa siku. Haya mapendekezo ndo yanapelekwa mpaka kwa wafadhili binafsi. Na hawa wafadhili na bodi ya mikopo inayaamini na kutoa kiasi hicho kilichopendekezwa.

  Pia Bodi ya mikopo inaongozwa na wanataaluma kwani mwenyekiti wake na wajumbe wa bodi ni viongozi na/au waliokuwa viongozi wa vyuo. Sina uhakika lakini ukichunguza unaweza ukakuta kuwa hata Prof. Maboko ni mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Loan Board ambayo nayo wanatafuna hela za sitting allowancies. Hii itamsababisha Prof. Maboko ashindwe kufanya kazi yake na kutoa taarifa za kufunika madude waliyoyafanya.
   
 2. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Badala ya kuunda tume iliyosheheni watumishi wa serikali angetafuta wataalum independent wafanye uchunguzi ili kugundua kuna matatizo gani na waje na solutions.
   
 3. M

  Matarese JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Angalia website ya Loan board, ni kweli Prof Maboko ni mjumbe wa bodi hiyo
   
 4. N

  Njaare JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Asante mkuu. Nimeona ni mmojawapo wa watafunaji wa sitting allowance. Tazama Board Members
   
 5. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Duh,sasa jk anazeeka,board member anachunguza matatizo ya taasisi anayoiongoza
   
 6. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #6
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kama kawaida yake!!!!
   
Loading...