Tume ya maadili yazungumzia ripoti ya mali za watumishi


MrFroasty

MrFroasty

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2009
Messages
740
Likes
46
Points
45
MrFroasty

MrFroasty

JF-Expert Member
Joined Jun 23, 2009
740 46 45
Fredy Azzah

TUME ya Maadi ya Utumishi wa Umma, imesema ripoti ya mali ya watumishi wa umma, itakamilika baada ya wiki mbili zijazo.

Akizungumza na Mwananchi jana, Ofisa habari wa tume hiyo, Ally Mataula, alisema ripoti kutoka katika mikoa yote zitatumwa makao makuu ya tume hiyo yaliyopo jijini Dar es Salaam, baada ya kukaguliwa.

Alisema wiki mbili kuanzia sasa, taarifa kutoka katika ofisi za kanda mbalimbali nchini, zitakuwa zimekwisha kamilika na kupelekwa makao makuu.

Ofisi za tume hiyo zimegawanyika katika Kanda ya Kaskazini (Arusha), Kanda ya Kati (Dodoma) na Kanda ya Kusini (Mtwara).

Hali kadhalika Kanda ya Ziwa (Mwanza), Kanda ya Juu Kusini (Mbeya) na Kanda ya Mashariki ( Dar es Salaam).

"Kutokana na uchache wetu, zoezi la kukagua ujazaji wa taarifa hizi utachukua muda kama wiki mbili hivi, ukaguzi huo utahusisha kuangalia kama kiongozi amejaza kama ilivyotakiwa kisheria.Taarifa zilizopo katika ofisi zetu mbalimbali za kanda, zitaletwa hapa baada ya kukaguliwa huko katika kanda," alisema Mataula.

Alisema kwa wale ambao hawatarejesha fomu hizo, watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi, kushauriwa kustaafu, kushushwa cheo ama kuonywa.

Alisema baadhi ya masharti yanayopaswa kutimizwa na mwananchi anayetaka kukagua ripoti hizo kwanza ni kutoa taarifa kwa kamisha kuhusu malalamiko yake juu kiongozi husika.

Hali kadhalika kulipa ada ya Sh1,000.

Alisema endapo kamishina hatoridhika na sababu zilizotolewa na mwananchi anayetaka kukagua mali za kiongozi huyo, anaweza kukataa ombi hilo.

Kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na.3 ya mwaka 1995 (pamoja na marekebisho ya mwaka 2002), kiongozi wa umma anatakiwa kutangaza mali zake katika kipindi cha siku 30 baada ya kupewa wadhifa, kila mwisho wa mwaka na mwisho wa kutumikia wadhifa wake.

Sheria inamtaka kiongozi wa umma kumpelekea kamishna tamko la maandishi katika hati rasmi, linaloorodhesha mali zake.

Sheria hiyo pia inabainisha kuwa masharti katika sheria hiyo yatakuwa ni sehemu ya maadili ya viongozi wa umma kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Chanzo:mwananchi
 
Facts1

Facts1

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2009
Messages
308
Likes
5
Points
0
Facts1

Facts1

JF-Expert Member
Joined Dec 23, 2009
308 5 0
Alisema kwa wale ambao hawatarejesha fomu hizo, watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi, kushauriwa kustaafu, kushushwa cheo ama kuonywa.

Watuondolee usanii wao naona wamekosa kazi kwani wakiorodhesha mali ndiyo itamsaidia nini mkulima wa mboga mboga kule Kisarawe hivi nani kwanza anataka ajue mali zao naona hawa jamaa wanataka kutuzidishia machungu zaidi tukijua mali zao.

Amekuambia nani atafukuzwa kazi kama si kuonywa tu, halafu ni kweli wameorodhesha mali zao zote? SHAME ON YOU Tume ya Adili na nduguze.
 

Forum statistics

Threads 1,238,129
Members 475,830
Posts 29,311,425