Tume ya maadili haihusiki na matumizi mabaya ya madaraka na mali za umma?

Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
2,662
2,000
Wana Jf wote,
NAWASALIM
Kipindi hiki kuna mjadala kuhusu Tundu Lissu kuvuliwa ubunge kwa kutojaza fomu za Tume ya maadili kuhusu mali na madeni yake.
Kwangu mimi sijaelewa kwanini Tume ijikite kwenye mali na madeni tu kwa viongozi wote wahusika!
Kwasababu suala la maadili ni pana zaidi ya umiliki halali wa mali binafsi za kiongozi, bali hata matumizi mazuri ya madaraka na mali za umma.
Kwamfano:
1. Kiongozi anapotumia fedha ya umma nje ya utaratibu kwa makusudi hii si kukiukwa maadili ya uongozi?
2. Mkuu wa Mkoa au wilaya anapomsweka ndani mtumishi wa umma bila kufuata utaratibu si ukiukaji wa maadili?
4. Kiongozi anapotumia cheo chake kujilimbikizia mali au majukumu nje ya cheo, eneo au mamlaka yake huu sio ukiukaji wa maadili?
5. Kiongozi anaetumia mamlaka yake kumlinda mtu aliyetenda kosa la jinai au kimaadili sio ukiukaji wa maadili?
6. Kiongozi anapotumia madaraka yake kupindisha sheria ili kumuundia raia kesi au kumtia hatiani kinyume na Katiba ya nchi sio ukiukaji wa maadili?
Mifano ipo mingi lakini hiyo niliyotaja inatosha.
Pili, Tume ya Maadili na TAKUKURU hufanya kazi pamoja kuhusu uhalali wa mali za kiongozi anazojaza katika fumu ya tamko la mali na madeni yake? Mbona tunasikia baadhi ya watu waliotajwa hapo juu wana majumba, magari na mali nyingi isivyoeleweka jinsi walivyopata?
Au ujazaji wa hizo fomu ni kama ubatizo au leseni ya biashara tu?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom