Tume ya kuchunguza kifo cha mwandishi mwangosi yaundwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume ya kuchunguza kifo cha mwandishi mwangosi yaundwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ELFU-ONEIR, Sep 6, 2012.

 1. ELFU-ONEIR

  ELFU-ONEIR Senior Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 183
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ameunda kamati ya watu watano kuchunguza mauaji ya Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel Ten, Daudi Mwangosi. Akitangaza kamati hiyo Dar es Salaam jana, Dk Nchimbi aliwataja wajumbe wake kuwa ni Jaji Mstaafu, Steven Ihema ambaye atakuwa Mwenyekiti na Mwakilishi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga.

  Wajumbe wengine ni Mwakilishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Pili Mtambalike, Mtaalamu wa milipuko kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kanali Wema Wapo na Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Isaya Mngulu. Mwangosi alifariki Septemba 2, mwaka huu baada ya kupigwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu wakati polisi walipokuwa wakiwadhibiti wafuasi wa Chadema. “Kamati hii nataka inipe majibu ndani ya siku 30 na kama utaalamu utakuwa hautoshi tutaomba msaada nje,” alisema Dk Nchimbi.


  SOURCE: HABARI ZA MITAA: KAMATI YA KUCHUNGUZA KIFO CHA MWANGOSI YAUNDWA
   
 2. Lastname

  Lastname JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 925
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Niliposikia yule jaji kilaza nikakata tamaa kabisa, kumbuka hajawahi kuandika hukumu hata moja kwa miaka yote aliyofanya kazi. ni mtu wa system system tu
   
 3. kivyako

  kivyako JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 8,858
  Likes Received: 4,239
  Trophy Points: 280
  Kweli sie watanzania ni mabingwa wa tume!! Hata hili tunahitaji tume!? mi nilifikiri ina hitajika hukumu tu kwa vile wauaji wanafahamika.
   
 4. D

  Danniair JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tume tafadhali msisahau kuwa askari anapotangaza hali ya hatari, he is ready to kill. kama ukitaka kufa nenda kabishane naye wakati huo. hata kama ni mwanao hakika atakutenda sawa na haki ya wakati huo.

  Pia msisahau kuzichunguza picha za marehemu pamoja na nguo alizo kuwa amevaa kama ziliandikwa PRESS/ mwanahabari.

  Halafu ktk taarifa yenu msisahau kuwakumbusha wanahabari kuwa,
  1.kama mwenzio akikusanywa ktk fujo kama hizo za Iringa, wewe mpige picha kisha baada ya vurugu nenda kampe dhamana na si kubishana wakati polisi walisha tangaza hali ya hatari.
  2. Wao si lolote si chochote wakati polisi wakiwa ktk hali ya vita. kwenda kwao ktk uwanja wa vita ni mapenzi yao ya kuuza habari na si vinginevyo. Its ones business.
  3. Tija yao ingekuwa kuwaelimisha wananchi kujiepusha na mikutano ambayo serikali ilishapiga marufuku.

  Pia, iwepo sheria ya kuwalipa fidia waathirika. Fidia hiyo ilipwe na chama husika. Kwani bila wao wananchi wasingeliuawa.
   
Loading...