Tume ya "KATIBA" na Wananchi Lazima TUPIGE KURA KUKUBALI TAIFA JIPYA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume ya "KATIBA" na Wananchi Lazima TUPIGE KURA KUKUBALI TAIFA JIPYA

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by niweze, Jan 1, 2011.

 1. n

  niweze JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama Tulivyosikia Mwenendo wa Mapambano ya Katiba kwa Ajili ya TAIFA Letu. Kinachofuata Sasa ni Utaratibu Jinsi ya Kuundwa kwa Hii Tume. Kama Kawaida ya CCM, Hawata Toa Utaratibu Ili Wananchi Tuujue. JK na CCM Watataka Kuonyesha Mabavu Yao na Kuteua Watu wa Karibu na Fikra Zao Kuongoza Huu Uundaji wa Katiba. Kitu Kikubwa Hapa Tupate Utaratibu wa Kuundwa kwa Hii Katiba na Dead Line Lazima Itolewe Kumalizika kwa Zoezi Hili. JK Lazima Ajue Kwamba Serikali Yake Itakuwa Haitambuliki Tena Baada ya Katiba Mpya. Wananchi Hasa Chama Kikubwa Nchini CHADEMA Wasikubali Tume Hewa. Wananchi Tunataka Tume Iongozwe na Kofi Annan au Thabo Mbeki. Hawa Viongozi Wamehusika Kusimamia Uundwaji wa Katiba za Kenya na Zimbabwe na Mpaka Sasa Credibility Zao Tunaziona Dunia Nzima. Thabo Mbeki (Former S. Africa President) Tayari Ameanzisha Fountation ya Leadership na Leadeship Accountability in Africa (Kuundwa kwa Serkali ya Ushirikiano Zimbabwe ni Matunda ya Mbeki) http://www.thabombekifoundation.org.za/about.php Tukizungumzia Kofi Annan (Former Successful UN Secretary) Ameshafanya Kazi Kubwa Africa na Hivi Karibuni Kenya. Kazi ya Katiba ya Kenya Ilifanikiwa kwa Ajili ya Koffi http://dev.kofiannanfoundation.org/
  Wajumbe Wengine Kwenye Hii Tume Watoke Chuo Kikuu, Kitengo cha Sheria, Wafanya Biashara na Vijana na Wanawake. Wawakilishi wa Tume Watoke Sehemu Zote za Nchi.

  Wananchi Tukumbuke Kwamba Katiba Haiwezi Kuwa Katiba Mpaka Ipigiwe Kura na Wananchi Wote. Wananchi Tusikubali Bunge au Ofisi ya Raisi Ipewe Madaraka Tena, HatutawezaKujenga Hili Taifa Letu. Uzito wa Katiba ni Sisi Wananchi Tunaujua na Unyimwaji wa Haki Tumeuona. JK Sio Raisi Kimadaraka Kama Ilivyo Sasa. Ofisi ya Raisi Itapunguziwa Influence Yake Katika Jamii Yetu. Kazi Ndio Imeanza...Tunawahitaji Watanzania Wote.

  "Wananchi Mapambano Yetu Yanazaa Matunda na Tusianze Kusheherekea Bado Jukumu Lipo Mikononi Kwetu"
   
Loading...