Tume ya Katiba Mpya, yenye Mapungufu Makubwa, yasiyoonekana Makubwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume ya Katiba Mpya, yenye Mapungufu Makubwa, yasiyoonekana Makubwa

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Yericko Nyerere, Apr 12, 2012.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  Apr 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Tume ya Katiba Mpya, yenye Mapungufu Makubwa, yasiyoonekana Makubwa, lakini yenye Kuhatarisha Umoja*wetu:

  Mnamo tarehe 6/4/2012, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Jakaya M. Kikwe alifanya uteuzi wa tume ya katiba mpya.

  Orodha ya wajumbe hao nini:

  UONGOZI WA JUU

  1. Mhe. Jaji Joseph Sinde WARIOBA – Mwenyekiti

  2. Mhe. Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino RAMADHANI – Makamu Mwenyekiti

  WAJUMBE KUTOKA TANZANIA – BARA

  1. Prof. Mwesiga L. BAREGU

  2. Nd. Riziki Shahari MNGWALI

  3. Dr. Edmund Adrian Sengodo MVUNGI

  4. Nd. Richard Shadrack LYIMO

  5. Nd. John J. NKOLO

  6. Alhaj Said EL – MAAMRY

  7. Nd. Jesca Sydney MKUCHU

  8. Prof. Palamagamba J. KABUDI

  9. Nd. Humphrey POLEPOLE

  10. Nd. Yahya MSULWA

  11. Nd. Esther P. MKWIZU

  12. Nd. Maria Malingumu KASHONDA

  13. Mhe. Al-Shaymaa J. KWEGYIR (Mb)

  14. Nd. Mwantumu Jasmine MALALE

  15. Nd. Joseph BUTIKU

  WAJUMBE KUTOKA TANZANIA – ZANZIBAR

  1. Dkt. Salim Ahmed SALIM

  2. Nd. Fatma Said ALI

  3. Nd. Omar Sheha MUSSA

  4. Mhe. Raya Suleiman HAMAD

  5. Nd. Awadh Ali SAID

  6. Nd. Ussi Khamis HAJI

  7. Nd. Salma MAOULIDI

  8. Nd. Nassor Khamis MOHAMMED

  9. Nd. Simai Mohamed SAID

  10. Nd. Muhammed Yussuf MSHAMBA

  11. Nd. Kibibi Mwinyi HASSAN

  12. Nd. Suleiman Omar ALI

  13. Nd. Salama Kombo AHMED

  14. Nd. Abubakar Mohammed ALI

  15. Nd. Ally Abdullah Ally SALEH

  UONGOZI WA SEKRETARIETI

  1. Nd. Assaa Ahmad RASHID – Katibu

  2. Nd. Casmir Sumba KYUKI – Naibu

  Nimpongeze*Mh Rais kwa kufanya uteuzi huu, lakini niitazame ktk jicho la tatu tume hii.

  Hii ni nchi ya Tanzania yenye kila aina ya changamoto za ndani na nje, yenye watu weledi na wasio weledi na yenye watu walio na imani zao zisizofungamana na dola.

  Binafsi naamini uteuzi wa tume hii umezingatia vigezo alivyokuwa navyo Mh Rais, na ameridhishwa kuwa hiyo ndiyo tume shahiki, nimponge tena na tena.

  Ningepewa mimi jukumu la kuiteua tumi hiyo, nami ningeweka vigezo vyangu, vigezo hivyo naamini vingepunguza kama si kuondoa kabisa mtazamo hasi wa wananchi juu ya tume hii.

  Mimi ningezingatia mambo matatu muhimu juu ya wa*upataji*tume hii.

  Weledi wa wajumbe

  Uwiano sawia wa kiimani nikitumia jiografia halisi ya nchi

  Muungano

  Nikiiangalia tume tajwa hapo juu, ni tume halisi iliyoteuliwa kwa kufuata mizania ya weledi. Ukiipinga tume hii kwa egemeo la weledi hulitakii mema taifa letu linalotaraji kuzaliwa upya.

  Ninasikitika sana uteuzi wa tume hii haujazingatia usawa wa kiimani, hii ni hatari zaidi kuliko hatari waionayo wanasiasa juu ya mageuzi kwao. Watafiti wa kiimani wanaamini kuwa 99.9% binadamu hutawaliwa na imani yake, hilo hata raisi anatambua umuhimu wa imani.

  Kwakutumia majina yaliyo kwenye orodha ninabainisha mapungufu makubwa ya uteuzi wa tume hii, ama yamefanywa kwa makosa ama yamefanywa makusudi, lakini niseme kuwa yameweka reheni imani ya mtanzania juu ya weledi wa tume kwa ujumla.

  Tume inawajumbe 30, lakini kwa kutumia jiografia halisi ya Tanzania natambua kwa majina, kuwa tume hii ina waislamu 21 na wakristu 9, *hili halihitaji utetezi zaidi ya busara za mteuaji (rais)

  Nikiangalia kwa mizania ya kiumungano, sijaona mantiki ya uwakilishi sawa wa wajumbe 15 Zanziber na 15 Bara (Tanganyika mufu)* Tz Bara ina watu milioni 42 na Zanziber ina watu miloni 2. Naamini kabisa kigezo kilichotumika ni kile kile cha miaka yote kisicho na manufaa kwa Wazanziber na Watanganyika cha kulinda muungano tata.

  Haiingii akilini mimi niwe na hisa 90% kisha tuwe na gawio sawa na wa hisa 10%. Hii ni dharau kwa wa Tanganyika na Wazanziber, tukae chini tukubaliane aina mpya ya muungano sio hii ya kulazimishana.

  Ninamshauri Mh raisi atumiea mamlaka tuliyompa* kuondoa mitazamo hasi juu ya tume hii kwa UDINI anaoupinga kila leo ndio huo alioutenda ndani ya tume hii. Natambua nguvu ya hisia za kidini na mh rais kwa tume hii itaamsha hisia zilizo lala na kuleta mtafaruku utakao haribu dhana nzima ya kupata katiba mpya.

  Nimpongeze sana Mzee Mtei kwa kuliona hilo na kulisema mapema japo WADINI wameinuka na kumpinga bila tafakuri ya kina.

  Ili kuona zaidi tembelea www.yerickonyerere.wordpress.c om

  MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRIKA

  (Katiba ni uhai wa taifa huru)
   
 2. K

  KAMBAKO Member

  #2
  Apr 12, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Wajumbe toka zanzibar (15) wote ni waislamu, wajumbe wengi toka Tanzania Bara ni Wakristo. HIvi kweli Zanzibar kuna wakristo wangapi??? mimi nadhani udini hapa haupo. Mimi ni Mkristo lakini hoja ya udini siioni. NInachoona mimi ni kumfanya Augustino Ramadhani kuwa Makama Mwenyekiti, hasa ukikumbuka kwamba huyu ndiye Hakimu aliyewakatalia watanzania haki yao ya kuzaliwa ya kugombea Ubunge au Urais bila kupitia ndani ya vyama. Kama itakuja hoja ya kubadili Katiba ili haki hii iandikwe, ni Wazi msimamo wa Jaji Ramadhani tunaufahamu.
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Apa hoja ni kama alivyosema Mtei haiwezekani watu 42mil mupewe watu 15 na wenzetu 1.5mil nao wapewe 15 people!
  Hesabu za wapi izo.
  Kuna haja ya kulifikilia ilo!
   
 4. driller

  driller JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 1,119
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  hiyo ni kweli mkuu
   
 5. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #5
  Apr 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Naumiza kichwa mpaka sasa sijui mh rais ametumia kigezo gani kupata hii tume?
   
 6. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #6
  Apr 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu!
   
 7. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #7
  Apr 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Tuwe makini sana tunapo jadili jambo hili,
  Nichukue fursa hii kukufahamisha kuwa Zanziba wapo wakristu, dhana kuu hapa si wakristu wa Zanziba, bali uwakilishi sawa wa kiimani tukitumia orodha ya majina ya wajumbe hapo juu!
   
 8. k

  kibunda JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Inaonekana watu hawakuwa wameisoma ile sheria. Mimi nashangaa kwanini yale ambayo yalipitishwa kwenye sheria hivi sasa yanatekelezwa watu wanashangaa. Kitu ambacho kiko wazi ni tume hii kukosa uwiano mzuri wa imani na jiografia kama mhe. Rais alivyoweza kufanikiwa kuweka uwiano kwenye weledi.
   
 9. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Katumia mswada wa sheria ya katiba uliopitishwa bungeni.huo ndio wenye matatizo
   
 10. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #10
  Apr 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Upo sahihi kabisa mkuu!
   
 11. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #11
  Apr 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Watanzania tulifanya makosa sana kuruhusu mjadala ule wa mwanzo wa mchakato utekwe na wanasiasa! Namkumbuka sana Prof Shivji pale Chuo kikuu alishauri vema kuwa ni hatari ikiwa rais ataachiwa mamlaka ya kuteua tume, kupokea maoni,kupokea hadidu za rejea,na mengine!

  Sasa ndio kwanza asubuhi hii tunaona kasoro je tuendako Katiba ya kweli itapatikana au ndio KUHUISHA kama rais anavyotaka kuwaaminisha watu kila azungumiapo katiba mpya?

  Nimejitahidi kumsikiliza rais, sijawahi kusikia toka kinywani mwake kuwa "kuandika katiba mpya" bali huita kuhuisha jambo ambalo ni tofauti na watanzania wanavyo amini!

  HUISHA = Boresha,Rekebisha,Sahihisha, Rembesha,Osha!

  Tafakari, Chukua hatua!
   
 12. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #12
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kugundua kasoro hiyo kama wewe leo hii unapata fursa ya kumshauri Rais; ni nani ungependekeza atolewe na aongezwe nani?

  Tuassume naye ni mdau humu JF bila shaka pendekezo lako laweza msaidia kufanya chaguzi yenye kufaa zaidi"
   
 13. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #13
  Apr 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Ukisoma vema hapo nimeeleza mizania halisi ya kupata wajumbe!
  Hivyo tayari nishamsaidia mh rais, kimaadili na kiweledi sio busara kumwambia raisi kuwa fulani na fulani, bali njia halisi za kupata wajumbe hao tu!

  Ili kuona zaidi tembelea www.yerickonyerere.wordpress.com
   
 14. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #14
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Nimefurahishwa sana kuona wapo watanzania wanaotamka wazi kuupinga mchakato wa katiba mpya ulivyo sasa, M.M Mwanakijiji ni alama ya mang'amuzi huru na ametoa somo kubwa sana! Watanzania tuunge mkono kuielimisha jamii juu ya ubatili na ubakwaji wa haki ya mwananchi ktk mktadha wa Katiba mpya!
   
 15. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #15
  Apr 13, 2012
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Yericko Nyerere na wenzako ni masanamu ya Michelini.. nguo ikishonwa begani inachanika ubavuni. Yaani Dr Salim kwa sifa zote za kiuongozi na utumishi uliotukukuka kwa nchi ya Tanzania leo hii mnaanza kumtazama kwa jicho la Uislam.. kabisa jamani? Kabisa jamani? This is SHIT!! (In capital letters). THIS IS SHIT YERICKO NYERERE!!

  Mimi ni Mtanzania na ni Mkatoliki hadi dakika hii (Naunga mkono kuwepo kwa Tanganyika). Maslahi ya Zanzibar katika katiba ni sawasawa na Tanganyika. Zanzibar ni inashare nusu ya heshima na identity katika Muungano, wanachama wa tume ya katiba siyo wabunbge kwamba "tuligawanye jimbo la Ukonga liwe Segerea na Ukonga kwa kuwa kuna watu wengi sana". Hivi pakiundwa EAC tuanze kuangalia uwakilishi kwa vigezo vya idadi ya watu? Uimara au unyonge wa Zanzibar katika Muungano hautakiwi kujengwa kwa misingi ya idadi ya watu. Zanzibar ni "state" hata kama ingekuwa na idadi ya watu wawili. Tanzania iliundwa kwa signatures za pande mbili na si Signature ya Tanganyika na robo signature ya Zanzibar. Ucheni uzoba... ninyi ndo mnatuambia mmesoma, elimu yenu inawasaidia nini ikiwa manawaza chini ya level ya kuku?

  Yaani akili yoooooooote inaona Mkristo Jaji Warioba "ataburuzwa na Waislam kibao" kudadadeki! ****!! Ikiwa ninyi "wasomi" mnawaza kimasaburi hivi basi CCM (Chama Cha Majambazi) kitaendelea kutuibia mpaka kesho. Kwenye tume kuna walemavu wangapi? Ulemavu wao ni wa aina gani? HIvi Tanzania ina wanawake wangapi? Wanaume wangapi? Ratio yao kwenye tume ikoje????

  Acheni use.. bana!!! Kwa midude yenye kuwaza kama Yericko Nyerere hatutapata katiba bora. Haiwezekani.

  Nampa pole Dr Salim, alikuwa Mtanzania, akawa Mwarabu, akawa Hizbu, akamuua Karume sasa ni Mwislam. Oh Lord!!! Huu ni uzoba mkubwa kabisa!!

  Bado nasimamia pale pale Waafrika wana/tuna akili kidogo. Alishasema P. W. Botha na Dr James Watson. Hovyooooooo!!!
   
 16. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #16
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Ni vema sana itokeapo mikingamo ya kimtazamo hasa tujadilipo jambo nyeti kama hili!

  Tofauti za kimawazo ktk mchakato huu ndizo zitakazo zaa katiba mpya na yenye mafaa kwa mtanzania!

  Andiko langu umelisoma kihoro mno, nasikitika lakini kisha nafurahi, kwa kuwa niwakati mnasibu kwa kukuomba uyarejelee kimang'amuzi maandiko yangu pasina kukengeuka!

  Zama zaidi ktk mfano nilioupendekeza ambao ungetumika kupata wajumbe stahiki wa tume hii.

  Katika maelezo yangu nimesema wazi kuwa tume hii imezingatia WELEDI pasina mawaa! Makunyanzi katika tume hii na ambayo ni hatari kuliko hatari waionayo ccm kuondolewa magogoni ni UWIANO wa KIMANI na MUUNGANO

  Waweza kuiona hoja dhaifu na ya kipuuzi, lakini ni kujuze tu kuwa "Hakuna Upuuzi ulio Upuuzi Mtupu"

  Ninaamini kwa vikinza hivi, Katiba mpya itapatikana tu,
  Swali ni je Itakuwa katiba ya Wananchi au katiba ya CCM?

  Jibu lipo kwa Jakaya Mrisho Kikwete!
   
 17. C

  Che-lee JF-Expert Member

  #17
  Apr 14, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umemjibu kwa hekima na busara sana! Nilidhani utaropoka kama yeye!

  Safi sana mkuu naunga mkono hoja yako!
   
 18. C

  Che-lee JF-Expert Member

  #18
  Apr 14, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umeona ehee! Yani jk anasema hakuna kujadili muungano?? Kweli hili tuliache??
   
 19. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #19
  Apr 14, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Matusi na kejeri sio asili ya mtanzania, mapokeo na mmomonyoko wa maadili ndivyo vilivyotuharibu na kukosa staha!

  Asante kwa kuunga mkono hojo!
   
 20. Karikenye

  Karikenye JF-Expert Member

  #20
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wakristo 11 bana: 1. Mhe. Jaji Joseph Sinde WARIOBA,2. Mhe. Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino RAMADHANI 3. Dr. Edmund Adrian Sengodo MVUNGI 4. Nd. Richard Shadrack LYIMO,5. Nd. John J. NKOLO 6. Nd. Jesca Sydney MKUCHU 7. Prof. Palamagamba J. KABUDI 8. Nd. Humphrey POLE POLE 9. Nd. Esther P. MKWIZU 10. Nd. Maria Malingumu KASHONDA 11. Nd. Joseph BUTIKU
   
Loading...