Tume ya Katiba Mpya yaongezewa muda

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameiongezea Tume ya Mabadiliko ya Katiba siku 14 zaidi kuanzia Desemba 16, mwaka huu, 2013, ili kuiwezesha kukamilisha kazi yake.

Rais Kikwete ameiongeza Tume hiyo muda zaidi kufuatia maombi ya Tume yenyewe na kwa mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu cha 8(3) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ameongeza muda wa Tume hiyo kufanya kazi kuanzia Desemba 16 hadi Desemba 30, 2013.

Hii ni mara ya pili kwa Rais Kikwete kuiongezea Tume hiyo muda wa kufanya kazi yake. Kufuatia maombi ya kwanza, Rais Kikwete aliiongezea Tume hiyo muda wa siku 45 kuanzia Novemba Mosi hadi Desemba 15, mwaka huu, 2013.

Chini ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Tume hiyo inatakiwa kufanya kazi kwa miezi 18. Aidha, sheria hiyo inampa Rais mamlaka ya kuiongezea Tume hiyo muda wa kufanya kazi usiozidi siku 60.

Kwa uamuzi wake wa kuiongezea Tume hiyo siku nyingine 14, Rais Kikwete atakuwa ameiongezea Tume hiyo muda wa kufanya kazi wa jumla ya siku 59 kati ya 60 ambazo anaruhusiwa kisheria kuiongezea Tume hiyo.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu. Dar es Salaam.
27 Novemba, 2013
 
!
!
watu katika mambo muhimu kama haya akuuu huwakuti, utawakuta wamekazana mara kapuya, mara zitto, mara chadema mara sijui nini agrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameiongezea Tume ya Mabadiliko ya Katiba siku 14 zaidi kuanzia Desemba 16, mwaka huu, 2013, ili kuiwezesha kukamilisha kazi yake.

Rais Kikwete ameiongeza Tume hiyo muda zaidi kufuatia maombi ya Tume yenyewe na kwa mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu cha 8(3) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ameongeza muda wa Tume hiyo kufanya kazi kuanzia Desemba 16 hadi Desemba 30, 2013.

Hii ni mara ya pili kwa Rais Kikwete kuiongezea Tume hiyo muda wa kufanya kazi yake. Kufuatia maombi ya kwanza, Rais Kikwete aliiongezea Tume hiyo muda wa siku 45 kuanzia Novemba Mosi hadi Desemba 15, mwaka huu, 2013.

Chini ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Tume hiyo inatakiwa kufanya kazi kwa miezi 18. Aidha, sheria hiyo inampa Rais mamlaka ya kuiongezea Tume hiyo muda wa kufanya kazi usiozidi siku 60.

Kwa uamuzi wake wa kuiongezea Tume hiyo siku nyingine 14, Rais Kikwete atakuwa ameiongezea Tume hiyo muda wa kufanya kazi wa jumla ya siku 59 kati ya 60 ambazo anaruhusiwa kisheria kuiongezea Tume hiyo.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu. Dar es Salaam.
27 Novemba, 2013
Tutegemee tusiyo yategemea ila kwa nia njema. Kwakuwa wengi wako busy na harakati za uongozi wa juu wavyama vyao na nafasi za uraisi na ubunge, nadhani tume itapata pumzi na nafasi ya kutosha kumaliza muda wake. Wasiwasi wangu ni kama sheria hii ya mabadiliko ya katiba itakidhi haja ya kazi za tume na mchakato mzima wa kufikia katiba ya mwisho. Ninawatakia wajumbe wa tume afya njema na waweze kumaliza kazi yao kwa hekima ileile. Pia Rais wa JMT kuweza kuimarisha hekima zilezile na busara katika kipindi hiki kigumu cha mpito. Mungu ibariki Tanzania bara na visiwani.
 
Rais amebakiwa na siku 1 tu ya kuongeza tena kati ya 60 anzoweza kuziongeza. Tunaomba hao wanatume wafanye kazi isijetokea wakaongezewa siku 1 tena.
 
HAPO MH. RAIS AMEFANYA LA MAANA SANA!
HUENDA BAADA YA MKUU HUYU NCHI IKAWA NZURI KWA KUPITISHA KATIBA INAYOJALI MASLAHI YA WANYONGE TULIOWENGI AU IKIWA BALAA KWA KUPITISHA KATIBA INAYO ENDELEA KUWANYANYASA WAKULIMA NA WANANCHI WENGINE! Hivyo ndg mkuu usiangalie maslahi ya chama wala watu fulani angalau nasi tukukumbuke kwa hili na mengine mengi umesha fanya!
 
Back
Top Bottom