Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
Tume ya Katiba mbinu kuteka mjadala-Lissu
Na Reuben Kagaruki
MBUNGE wa Singida Magharibi, Bw. Tindu Lissu, amesema Tume ya Maalumu ya Katiba itakayoundwa na Rais Jakaya Kikwete, ni mbinu ya miaka yote ya
kuteka mijadala hatari kwa CCM na serikali na kuielekeza palipo salama.
Katika maoni yake kwenye mtandao wa Wanabidii jana na baadaye kulithibitishia gazeti hili kuwa hayo ni maoni yake binafsi na si msimamo wa chama, Bw. Lissu amesema mara mjadala unapoanzia nje ya chama au dola ni hatari kwa watawala, hasa pale ukiachwa ujiendee wenyewe bila kuingiliwa.
"Hapa ndipo watawala wanaingia kwa 'gear' ya Tume ya Katiba. Tume hiyo inajengewa hoja yenye maneno matamu na rais, inakolezwa utamu kwa kuwekwa mtu mmoja au wawili (kwa mfano 'mwanasheria aliyebobea)," alisema Bw. Lissu na kuongeza;
"Kwa hiyo, maneno kama 'Tume yenye uwakilishi wa makundi mbalimbali ya kiraia' ni chumvi tu inayopakwa kwenye mhogo mchungu ili ulike kirahisi."
Alisema wananchi wanaambiwa tuwe na subira hadi Tume ya Rais itakapomaliza kazi yake.
"Tunaaswa tuwe wavumilivu ili tule mbivu na katu tusiwe na jazba, munkari au kelele wakati mjadala unauawa pole pole kwa kupitia tume," alisema Bw. Lissu.
Alisema watu wachache wanaoendelea kupiga kelele kuwa mjadala umetekwa nyara, wanashambuliwa kuwa wanaonea wivu wale walioteuliwa kwenye Tume ya Rais, au wanaitwa walalamikaji tu wasiokuwa na lolote la kujenga au ni wakosoaji wa kila kitu kinachofanywa na mtukufu Rais hata kama kina maslahi kwa nchi.
Bw. Lissu alitoa mfano wa tume nyingi ambazo ziliwahi kuundwa, lakini ripoti zake hazijawahi kutekelezwa.