Tume ya katiba kufanya mikutano 56 katika kata 60 mkoani Mtwara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume ya katiba kufanya mikutano 56 katika kata 60 mkoani Mtwara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by HUNIJUI, Oct 15, 2012.

 1. HUNIJUI

  HUNIJUI JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 10, 2012
  Messages: 1,441
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  timu ya tume ya mabadiliko ya katiba, inatarajiwa kufanya jumla ya mikutano 56, katika kata zipatazo 60, ikiwemo mkutano mmoja katika kila kata 10 za wilaya za mkoa wa mtwara.

  akitoa tathimini kwa waandishi wa habari wilayani masasi mkoani mtwara, baada ya mikutano katika wilaya za nanyumbu na masasi, mwenyekiti wa timu ya tume inayoratibu ukusanyaji wa maoni kwa mkoa wa mtwara, muhhamad mshamba, amesifu mwitikio wa wananchi waliokutana nao katika siku za kwanza za mikutano ya tume hiyo.
  amesema kuwa mikutano hiyo iliyoanza oktoba 06 mkoani mtwara katika wilaya ya nanyumbu, amesifu wananchi hususani wilayani masasi kwa kutoa maoni yao kwa dhati na kwa uwazi wa hali ya juu, bila kuwepo kwa mivutano ya itikadi za dini na siasa.
  mshamba amesema kuwa tofauti na mikoa ya kusini pemba, kusini unguja na manyara walikopita, mkoa wa mtwara, hususani wilaya ya masasi imevunja rekodi kwa wananchi wengi kujitokeza na kutoa maoni yao binafsi, tofauti na maoni ya mikoa mingine waliyopita ambayo aidha walisemewa au walifundishwa cha kuongea.

  hata hivyo mmoja wa wajumbe wa tume hiyo, kibibi amani hassani, amewataka akinamama wengi kujitokeza kwa wingi na amewatoa hofu kushiriki kutoa maoni yao mbele ya tume hiyo, na si kutegemea kutoa maoni kwa kujaza fomu pekee, ili kuweza kupata maoni yao halisia mbele ya tume hiyo.

  kwa upande wake mjumbe mwingine katika timu hiyo, dk.sengondo mvungi ametanabaisha kuwa lengo la tume hiyo kuuliza maswali wananchi wanapochangia maoni yao, ni kupata uhalisia wa kujua lengo la mtoa maoni, hivyo amewatoa shaka wananchi kuwa huru na kushiriki kikamilifu katika utoaji wa maoni

   
 2. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Wasisahau kutaja mgao wao kwenye raslimali ya gesi na mafuta kwenye Katiba.
   
Loading...