Tume ya katiba imesahau kundi muhimu sana nchini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume ya katiba imesahau kundi muhimu sana nchini!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mukaruka, Jul 18, 2012.

 1. M

  Mzee Mukaruka JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 254
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Napenda kuchukua nafasi hii kwanza kuikumbusha Tume ya Kukusanya Maoni kuhusu uandikaji wa Katiba Mpya ya nchi yetu kuwa pamoja na utaratibu waliojiwekea kufuatana na Sheria inayowaongoza, napenda kuwa wafanye juu chini, na kwa uwezo wao wote (najua uwezo wa kifedha wanao kwani wana mahela mengi tu) watembelee wasomi wetu, na hapa sibagui, watembelee wanafunzi mashuleni kwenye shule za msingi, sekondari na kwenye vyuo vyetu vyote! Nashauri hili kwa sababu ukiangalia ratiba za Tume, wanazungumzia mikutano ya hadhara kama venue pekee ya kukutana na wananchi ili kuwasikiliza na kukusanya maoni yao. Hao wananchi wengine niliowataja hapo juu watapata hiyo fursa wakati gani?! Hasa ukizingatia kuwa kwenye mikutano hiyo, Tume haichukui zaidi ya saa tatu (3) kwa kila mkutano. Tume ikutane na wasomi hawa katika makundi makundi; binafsi nasisitiza hili kwa sababu hawa ndio watakao ishi na hii Katiba Mpya for a good time to come. Hii ni ya kwao wapeni nao fursa ya kuchangia maoni yao.

  Pili niwashauri wananchi waachane na hizi propaganda ya kuambiwa kuwa utachangiaje maoni kwa ajili ya Katiba mpya wakati ile ya zamani huijui!? Nadhani huu ni upotoshaji kwa nia na lengo la kutaka kuwatoa watu kwenye hoja ya msingi - ambayo ni kutoa maoni ili tupate Katiba Mpya. Sidhani unahitaji kujua mchoro wa nyumba unayotaka kujenga in detail kivile kama architecture. Wewe mpe outline muhimu na yeye kama mtaalamu atakutolea mchoro, mtaujadili na kama mkikubaliana basi anaendelea na ujenzi. Hii ndiyo approach katika mchakato huu in a simple layman's language.

  HAYA TUJADILI WANA JAMII FORUM
   
 2. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,755
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  Baadhi ya vyuo tayari wamekutana navyo sijui kwa shule za msingi na sekondari.
   
Loading...