Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,898
Tume ya Haki za binadamu waichunguza Hospitali Mwananyamala
Na Jackson Odoyo
Na Jackson Odoyo
TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, imenza kuchunguza tukio la mama mjamzito alyefariki dunia katika Hospitali ya Mwananyamala Juni Mosi, mwaka huu kwa madai ya kukosa huduma.
Kwa mujibu wa Uchunguzi wa Mwananchi na tume hiyo imeamua kufanya uchunguzi huo ili kufahamu aina ya ukiukwaji wa haki za binadamu uliopo katika hospitali hiyo.
Taarifa zilizothibitishwa na tume hiyo kuhusu hatua hiyo, zimeeleza kuwa kazi hiyo ilianza siku chache baada ya mama huyo kufariki dunia na kwamba hivi sasa inaelekea ukingoni.
Chanzo chetu cha habari ndani ya tume hiyo kimesema kuwa maofisa wao walianza kufanya kazi hiyo mara tu walipopata taarifa za kifo cha mama huyo.
Chanzo hicho kilisema wameamua kufuatilia undani wa suala hilo, baada ya kuwepo kwa taarifa mbalimbali za vifo vya watoto na akina mama wajawazito zinazodaiwa kusababishwa na uzembe na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Alisema mbali na vifo hivyo, pia kumekuwepo na malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa baadhi ya wagonjwa na ndugu zao wanaofika katika hospitali hiyo kwa lengo la kupata matibabu.
''Maafisa wetu wanaendelea na uchunguzi wa suala hilo ingawa wanakumbana na vikwazo kadhaa kutoka kwa uongozi wa hospitali hiyo, lakini kwa kiasi kubwa wameanza kufanikiwa,'' kilieleza chanzo hicho.
Katika hatua nyingine ndugu wa marehemu, wamemuandikia Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa barua ya kuomba wapewe taarifa ya maandishi kuhusu kifo cha ndugu yao na kwamba aunde tume ya kuchunguza suala hilo.
Kwa muujibu wa nakala ya barua hiyo iliyosainiwa na mjomba wa marehemu Teddy Dimoso, Yokonia Gabriel ilisema wao wanaamini kifo cha ndugu yao ilitokana na uzembe wa wauguzi wa hospitali hiyo.