Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora yatoa Tathmini ya Mchakato wa Uchaguzi 2020

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,291
24,167

Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mhina Mwaimu wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora - THE COMMISSION FOR HUMAN RIGHTS AND GOOD GOVERNANCE (CHRAGG) anazungumza kuhusu uchaguzi huu wa 2020.

Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mhina Mwaimu aliteuliwa na Mh. Rais John Pombe Joseph Magufuli mwezi Oktoba 2019 Retired Judge Mwaimu appointed new Chair of CHRAGG kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala.

Jaji mstaafu Mathew Pauwa Mhina Mwaimu anamwambia mwandishi wa habari na waTanzania kuwa mchakato wa uchaguzi unaenda kwa taratibu na sheria zilizowekwa.
Jaji mstaafu Mwaimu angaongeza kuwa suala la kuwa na mashaka kuwa uchaguzi utakuwa wa haki na huru si tu la Tanzania tu bali lipo dunia nzima hata nchi zilizoendelea bila kusahau nchi zinazoendelea za Afrika na Latin Amerika.

Serikali iliyopo madaraka na chama chake tawala chenye wabunge wengi mara nyingi hudhaniwa hawatatenda haki kwa vyama vyenye wabunge wachache wanaofahamika kama wapinzani. Mfano Tanzania kuenguliwa kwa wabunge wengi wa vyama vyenye wabunge wachache yaani upinzani pamoja na kuwepo kwa nafasi ya kupinga kuenguliwa kwa kuruhusiwa kupeleka rufaa kwa Tume ya Uchaguzi wa Taifa bado kuna mashaka kama kuenguliwa huko ni kwa haki na uwazi kutokana na mazingira ya teuzi za wasimamizi kuonekana ni makada. Jaji Mathew Pauwa Mhina Mwaimu pia alijibu masuala yanayohusu hoja hizi zifuatazo:

  1. Waangalizi wa uchaguzi wa ni pamoja Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Waangalizi toka Ndani na Nje ya Nchi
  2. Tamko la nchi za Jumuiya ya Umoja wa Ulaya European Union kuhusu kuzorota kwa hali ya Haki za Binadamu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020m
  3. Vyombo vya Ulinzi na Usalama kama Polisi wameelimika zaidi ndiyo maana katika mchakato wa kuelekea October 2020 hakuna matumizi ya mabavu kama mwaka 2015
  4. Wananchi kuelekea uchaguzi wa 2020 inaonekana wagombea wanasikiliza sana sera katika uchaguzi huu wa 2020
  5. Wagombea wa CCM pamoja na kuenguliwa na Wajumbe wa Mikutano yao ya ndani ya CCM wanaelekea wamekubali hilo na kupunguza mikwaruzano yao kuwafikia wananchi wapiga kura
  6. Mwaka huu 2020 lugha ya matusi imepungua sana na Tume ya Uchaguzi ya Taifa NEC walikemea tofauti na uchaguzi wa 2015
 
Chama tawala wanapotaka kurudi au kusalia madarakani wanatumia vyombo vilivyopo kwa uwezo hata hila ili kusalia, jaji mstaafu anaongea kwa kigugumizi maana anajua fika haki kwa serikali za kiafrika ni ngumu pale uchaguzi unapokuwa haufuata njia stahiki.

Anasema baada ya uchaguzi unaweza kwenda mahakamani kudai HAKI labda apo aliposema kwa wakoloni ndipo inawezekana ila kufuatia katiba hii hii tunayotembe nayo kwenye mabegi hakuna uswa na haki.

This is Afrika.
 
Uhuru ambao CHADEMA tunawaelezea kwa upana wake, ndiyo huu tunaoutaka ikiwemo kwa Tume kama hii na nyingine ziwe huru kweli yaani isiwe na mwenyekiti aliyeteuliwa na Rais.
 
Kama kilichoandikwa ndio statement ya tume yenyewe Kuna. Shida kubwa Sana.

Anareport Kama vile yeye ni msemaji wa serikali au CCM

Tulitegemea atoe mwenendo wa uchaguzi kwa kusema
Je tume imefanya majuku yake kwa mujibu wa Sheria? Hivyo hivyo vyama? Je wananchi? Polisi? Wadau wengine?

Vipi viashiria vinavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani na haki za binadamu?

Nini kifanyike kuzuia uvunjifu wa haki za binadamu a amani?

Hatujasikia ahadi zitolewazo na baadhi ya wagombea kinyume na maadili ya uchaguzi na Nini kifanyike
 
Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mhina Mwaimu wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora - THE COMMISSION FOR HUMAN RIGHTS AND GOOD GOVERNANCE (CHRAGG) anazungumza kuhusu uchaguzi huu wa 2020.

Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mhina Mwaimu aliteuliwa na Mh. Rais John Pombe Joseph Magufuli mwezi Oktoba 2019 Retired Judge Mwaimu appointed new Chair of CHRAGG kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala.

Jaji mstaafu Mathew Pauwa Mhina Mwaimu anamwambia mwandishi wa habari na waTanzania kuwa mchakato wa uchaguzi unaenda kwa taratibu na sheria zilizowekwa.
Jaji mstaafu Mwaimu angaongeza kuwa suala la kuwa na mashaka kuwa uchaguzi utakuwa wa haki na huru si tu la Tanzania tu bali lipo dunia nzima hata nchi zilizoendelea bila kusahau nchi zinazoendelea za Afrika na Latin Amerika.

Serikali iliyopo madaraka na chama chake tawala chenye wabunge wengi mara nyingi hudhaniwa hawatatenda haki kwa vyama vyenye wabunge wachache wanaofahamika kama wapinzani. Mfano Tanzania kuenguliwa kwa wabunge wengi wa vyama vyenye wabunge wachache yaani upinzani pamoja na kuwepo kwa nafasi ya kupinga kuenguliwa kwa kuruhusiwa kupeleka rufaa kwa Tume ya Uchaguzi wa Taifa bado kuna mashaka kama kuenguliwa huko ni kwa haki na uwazi kutokana na mazingira ya teuzi za wasimamizi kuonekana ni makada. Jaji Mathew Pauwa Mhina Mwaimu pia alijibu masuala yanayohusu hoja hizi zifuatazo:

  1. Waangalizi wa uchaguzi wa ni pamoja Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Waangalizi toka Ndani na Nje ya Nchi
  2. Tamko la nchi za Jumuiya ya Umoja wa Ulaya European Union kuhusu kuzorota kwa hali ya Haki za Binadamu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020m
  3. Vyombo vya Ulinzi na Usalama kama Polisi wameelimika zaidi ndiyo maana katika mchakato wa kuelekea October 2020 hakuna matumizi ya mabavu kama mwaka 2015
  4. Wananchi kuelekea uchaguzi wa 2020 inaonekana wagombea wanasikiliza sana sera katika uchaguzi huu wa 2020
  5. Wagombea wa CCM pamoja na kuenguliwa na Wajumbe wa Mikutano yao ya ndani ya CCM wanaelekea wamekubali hilo na kupunguza mikwaruzano yao kuwafikia wananchi wapiga kura
  6. Mwaka huu 2020 lugha ya matusi imepungua sana na Tume ya Uchaguzi ya Taifa NEC walikemea tofauti na uchaguzi wa 2015

A well fed slave
 
Back
Top Bottom