Tume ya Haki Binadamu na Utawala Bora yaangukia vyombo vya habari

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji mstaafu Mathew Mwaimu, amesema tasnia ya habari kuwa ndio wadau wakubwa wa haki za binadamu nchini.

Jaji Mwaimu alisema hayo jana katika mkutano uliofanyika Zanzibar wa kuwajengea uelewa wa pamoja makamishna wa tume walioteuliwa hivi karibuni na Rais John Magufuli.

Alisema katika kutekeleza jukumu walilopewa la kulinda, kuhifadhi na kutetea haki za binadamu nchini, wanawategemea sana vyombo vya habari kuelimisha jamii kuhusu haki zao.

“Vyombo vya habari ni wadau wetu wakubwa sana. Wao ndio waelimishaji, wao ndio wamekuwa wakati wote wakiibua matukio mbalimbali ya uvunjifu wa haki za binadamu kwa lengo la kuujulisha au kuelimisha umma,” alisema.

“Nyie ndio mtakaoitangaza tume. Kwa msingi huo, niseme kuwa tutaendelea kuwashirikisha katika yale yote tutakayokuwa tunayafanya ili kupitia ninyi wananchi watafahamu kuhusu tume inachokifanya,” aliongeza.

Mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa tume haiwezi kufanya kazi peke yake bila kushirikiana na wadau wengine kama vyombo vya habari, idara za serikali, asasi za kiraia na taasisi za kimataifa.

“Ni lazima tujenge uhusiano mzuri wa kazi baina yetu. Hatuwezi kufanya kazi peke yetu, hivyo ni muhimu kufanya kazi na idara mbalimbali wakiwamo wadau wa maendeleo,” alisisitiza.

Naye Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi Zanzibar, Assaa Ahmad Rashid, ambaye alifungua mkutano huo, alimweleza Jaji Mwaimu kuwa dhamana waliyopewa ni kubwa kwa kuwa haki za binadamu ndio msingi katika nchi na kwamba wameaminiwa hivyo hawana budi kulitekeleza jukumu hilo kwa ufanisi ili kuwasaidia wananchi.

“Jukumu mlilopewa serikali ni kubwa. Tunawaahidi kuwa tutaendelea kutoa ushirikiano katika kuifanya tume kutekeleza majukumu yake vizuri,” alisema

Rashid pia alisema kuteuliwa kwa viongozi hao kunatoa fursa kamili na ya wazi kwa mwananchi kupeleka malalamiko yake na kwamba serikali imejenga mazingira mazuri ya kufanya kazi kwa wadau wote hususan asasi za kiraia na wakati wote serikali itaendelea kushirikiana na taasisi zote zikiwamo za kimataifa ili kuhakikisha yale malengo yaliyowekwa yanafikiwa.

“Tunatambua kuwa katika kutekeleza majukumu yenu kuna changamoto mnazo kutana nazo, ikiwamo uelewa mdogo wa wananchi kuhusu haki zao lakini mwendelee kueneza elimu hiyo kwa kushirikiana na taasisi zingine,” alisema.


Chanzo: IPP Media
 
They were told by Jiwe that l quote, " you're not free to that extent " Then some years later Azory Gwanda disappeared and is nowhere to be found. Free media in this regime is highly risky
 
Now days ITV and Other Media looks like TBC. The only News am watching is only BBC News that starts 21.00 Hours and end 21.30. After that I go to Bongo star search. I cant waste my time watching rubbishes.
 
Back
Top Bottom