Tume ya Chifu Mang'enya: Kwanini Ripoti yake Haijulikani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume ya Chifu Mang'enya: Kwanini Ripoti yake Haijulikani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 16, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Watu wengi hawakumbuki kuwa miaka ya 60 Nyerere aliunda Tume ya Chifu Mang'enya ambayo iliundwa kuangalia mojawapo ya matatizo makubwa ya kitaifa. Kuundwa kwa tume ile kulionesha kuwa Nyerere hakuwa na hofu ya kulikabili jambo lolote na ripoti yake iliwekwa hadharani. Wazee wengi ambao wamestaafu katika utumishi na wengine ambao labda walikuwa ndio wanaingia kwenye utumishi wanaweza kuikumbuka tume hii na umuhimu wake kwa taifa.

  Hata hivyo watu wengi hawajui hata uwepo wake na umuhimu wake kwani yale yale ambayo Tume ya Chifu Mang'enya iliyashughulikia yanarudia tena leo hii na Rais Kikwete na serikali yake hawana ujasiri wa kufanya kile ambacho Nyerere alikifanya wakati ule. Je, unajua nini kuhusu Tume hii? Je ungependa wanahistoria wetu walikumbushe taifa juu ya matokeo ya tume hii? Je unajua kurudishwa kwa hoja zilizoangaliwa na tume hii zitabadilisha kabisa upepo wa kisiasa ambao unaenezwa sasa hivi kama ilivyokuwa karibu miaka hamsini iliyopita.

  Wanasema usipojua historia utajikuta unairudia; well, tumesahau historia yetu na sasa tunairudia wenyewe tukiamini tunafanya kwa mara ya kwanza.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  May 16, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,183
  Trophy Points: 280
  Watanzania hatuna utamaduni wa kujikosoa wala kukosolewa.
  Taarifa nyeti kama hizo hata maktaba hauzikuti, zimwekwa lkulu.
  Inabidi tubadilike na serikali yetu ianze kufanya mambo yake kwa uwazi zaidi.
   
 3. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #3
  May 16, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Bwana wee, mambo yalivyo hapa kijijini ni sawa na bandiko lile maarufu la kitabuni lililojaa hekima la MHUBIRI.. kwamba ubatili ubatili ubatili..mambo yote ni ubatili...kujilisha upepo... UNATEGEMEA KUIFIKIRISHA AKILI WAKATI UNAFIKILIA ULAJI KILA BAADA YA MIAKA MITANO...? Imekula kwetu..tukubali maumivu hadi hapo akili zikitukaa sawa na kuvaa kaptula zenye Vilaka matakoni..
   
 4. umkhonto

  umkhonto Member

  #4
  May 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  @MM,tafadhali tujuze..ni vema tukajifunza historia...kama hujui ulipotoka..waweza kuwa unazunguka hapo hapo...
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  May 21, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Tume ya Kudumu iliyokuwa chini ya Chifu Mang'enya ilikuwa tume huru iliyokuwa inapokea malamiko ya raia kuhusu viongozi pamoja na watu wengine maarufu na kuyafanyia uchunguzi. Ilipojiridhisha kuwa kiongozi au mtu anayelalamikiwa kweli alitumia madaraka au nafasi yake vibaya kujineemesha au kumwonea raia, basi ama tume ilipendekeza kwa rais kuwa kiongozi mhusika avuliwe madaraka na kuadhibiwa, au kama mhusika siyo kiongozi wa serikali basi akamatwe na kufikisha mahakamani. Tume hii ilikuwa na nguvu sana wakati wa Nyerere ambapo mapendekezo yake yalikuwa hyapuuzwi, lakini nadhani madaraka yake yalififia sana wakati wa utawala wa Mwinyi aliyeanzisha mikutano ya kila mwezi Lumumba na baadaye kutoweka kabisa. Sina uhakika na nguvu za kisheria za tume ile kwani sijaisikia tena tangu nyerere aondoke.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  May 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kichuguu, kitu kimoja ambacho kilikuja kufanywa na Tume ya Mang'enya ni kuchunguza malalamiko ya Udini na Ukabila ambayo yalikuwa yameenea huku Wahaya, Wachagga na Wanyakyusa (ambapo pia walikuwa predominantly ni Wakristu) walilalamikiwa na baadhi ya watu. Hii ilikuwa ni katika nafasi za kiserikali na za kisiasa. Ripoti yake iliwekwa hadharani.. ningependa kweli kujua kama inaweza kupatikana maana ni kama tunarudia kwenye historia ile ile tu. Tume yake ilikuwa ni kama Ombudsman wa Serikali na utawala bora.

  Nadhani mbadala wake ni tume karibu tatu zilizoko sasa - Tume ya Haki za Binadamu, Tume ya Maadili ya Viongozi na Ofisi ya Utawala Bora (wizara).
   
 7. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  I am the one of those who belive in History as the basic foundation of life as one sees it today. I'm learning about Mang'enya commitee for the first time but have been fascinated by the fact that it existed. I too want to see its findings and relate to the current commitees you have mentioned. I promise to get back then. For now thanks for an historic highlight.
   
Loading...