Uchaguzi 2020 TUME: Pamoja na kwamba kupiga kura hiari, Serikali imeingia gharama kubwa sana. Tunawasihi Watanzania wakapige kura

Tatizo hapo ninaloliona ni lile la mtu akapige kura kituo alichojiandikishia. Sijui kama kweli tehama imetusaidia nini kwenye hii tume.

Mi nimepewa link tu ya kuangalia kama ni mpiga kura na nimefanikisha.

Sasa inashindikana nini kupiga kura kituo chochote kwani ukitaka kumuona kuwa ni mpiga kura unaona tu kama ni halali au haramu?
Hakuna ambacho haiwezekani bali wanakataa ili kuiba kura kwa urahisi na bila complications...
 
Tatizo hapo ninaloliona ni lile la mtu akapige kura kituo alichojiandikishia. Sijui kama kweli tehama imetusaidia nini kwenye hii tume.

Mi nimepewa link tu ya kuangalia kama ni mpiga kura na nimefanikisha.

Sasa inashindikana nini kupiga kura kituo chochote kwani ukitaka kumuona kuwa ni mpiga kura unaona tu kama ni halali au haramu?
Issue sio tehama peke yake hapa.

Walipotangaza watu wajiandikishe na kuhakiki taarifa mapema walitaka wajue pia idadi ya wapiga kura kwa kila kituo ili waweze kupanga rasilimali zitakazotoshana nao ikiwa ni pamoja na vifaa, wasimamizi, muda na hata majengo pia.

Leo wakiruhusu kila mtu apige kura sehemu yoyote kuna vituo vitakua na wapiga kura wachache au kukosa kabisa huku vingine vikizidiwa na idadi kubwa ya wapiga kura

Kikubwa tarehe inajulikana na siku ya kupiga kura hakuna kazi twendeni tulikojiandikishia tukatimize wajibu
 
Wale ambao madiwani na wabunge wao tayari wameteuliwa na tume watawapigia nani?
 
Waahidi kwanza kuziheshimu hizo kura zetu ndiyo waje watushawishi kupiga kura. Yaani tume yenyewe imejaa mikada kindakindaki ya CCM halafu kirahisi tu tushawishike kupiga kura!

Watuambie kama wako tayari kumtangaza mshindi halali halafu wataona tutakavyo miminika siku hiyo kwenye vituo vya kupigia kura. Hata sisi tuliosafiri, aisee tutarudi kwa kasi ya ajabu ili tu kupigia MABADILIKO.
Sasa kwa nini mnampotezea muda "mbeligiji"!!! Mkuu kura yako muhimu sana, tafadhali tukapige kura 28/10/2020, Tumchague rais asiye na vinasaba vya mabeberu!
 
Mkurugenzi wa tume ya Taifa ya uchaguzi upande wa huduma, Emmanuel Kawishe anaongelea mambo kadhaa kuelekea uchaguzi mkuu na amezungumzia gharama nyingi zilizotumika kutimiza azma ya mtanzania kupiga kura kama makaratasi, mafuta, kulipa watu wote wanaohusuka na mchakato wa upigaji kura na kadhalika.

Kawishe amesema yote hayo ni kumuwezesha mtanzania kupiga kura hivyo japo inabaki hiari lakini ni muhimu sana kwenda vituoni kupiga kura na kuwasihi baada ya zoezi kila mtu akaendelee na ratiba zake.

Pia ndugu Kawishe amewakumbusha watu wote kuwa kipindi cha uchaguzi sheria za nchi zinaendelea kufanya kazi.
Hima Watanzania baada ya Tume kutimiza waji wao sasa ni Haki yetu sisi kuitumia fursa hiyo kujitokeza kwa wingi kwaajili ya upigaji kura. Tukapige kura kuwachagua wale ambao tunadhani watasimamia Ilani na kutekel;eza yale waliyotuahidi kwa manufaa ya taifa letu na vizazi vyetu vijavyo.
 
Mkurugenzi wa tume ya Taifa ya uchaguzi upande wa huduma, Emmanuel Kawishe anaongelea mambo kadhaa kuelekea uchaguzi mkuu na amezungumzia gharama nyingi zilizotumika kutimiza azma ya Mtanzania kupiga kura kama makaratasi, mafuta, kulipa watu wote wanaohusuka na mchakato wa upigaji kura na kadhalika...
Ni kweli kabisa gharama za uchaguzi ni kubwa Sana kwa hiyo tukifanya mzaha uchaguzi ukaharibika ni upotezaji wa pesa za watanzania
 
Pia ambao wanadhamana ya usimamizi was mchakato huu wahakikishe wanatenda haki vinginevyo.Yote yaliyofanyika yatapoteza maana mbali na kuwa gharama kubwa imetumika.
 
Mkurugenzi wa tume ya Taifa ya uchaguzi upande wa huduma, Emmanuel Kawishe anaongelea mambo kadhaa kuelekea uchaguzi mkuu na amezungumzia gharama nyingi zilizotumika kutimiza azma ya Mtanzania kupiga kura kama makaratasi, mafuta, kulipa watu wote wanaohusuka na mchakato wa upigaji kura na kadhalika.

Kawishe amesema yote hayo ni kumuwezesha mtanzania kupiga kura hivyo japo inabaki hiari lakini ni muhimu sana kwenda vituoni kupiga kura na kuwasihi baada ya zoezi kila mtu akaendelee na ratiba zake.

Pia ndugu Kawishe amewakumbusha watu wote kuwa kipindi cha uchaguzi sheria za nchi zinaendelea kufanya kazi.
Asitufokee
 
Mwambie mahera, uchaguzi huu hautamuacha salama akileta useng.e
 
Tatizo hapo ninaloliona ni lile la mtu akapige kura kituo alichojiandikishia. Sijui kama kweli tehama imetusaidia nini kwenye hii tume.

Mi nimepewa link tu ya kuangalia kama ni mpiga kura na nimefanikisha.

Sasa inashindikana nini kupiga kura kituo chochote kwani ukitaka kumuona kuwa ni mpiga kura unaona tu kama ni halali au haramu?
Mkuu inaruhusiwa ku-share hiyo link?
 
Sawa tumekusoma. Pamoja na kutumia hizo gharama kubwa. Ninyi mhakikishe vitendea kazi vya kupigia kura vinafika maeneo yote husika mapema. Sio kituo kinafunguliwa box zinafika saa nane mchana na pili kuhakikisha kuna umeme au generator kiuweza kuhakiki uhesabuji wakura. Polisi hawahusiki maswala ya kupiga kura zaidi ya usalama wa watu nje ya kituo wasipigane.
Tanesco waache kukata umeme na wasimamizi wawe smart na kuharakisha zoezi la upigaji kura. Sio mpiga kura anafika anaambiwa jina halipo! Upangwe utaratibu wa hatua kwa hatua na haki itendeke..
 
Mkurugenzi wa tume ya Taifa ya uchaguzi upande wa huduma, Emmanuel Kawishe anaongelea mambo kadhaa kuelekea uchaguzi mkuu na amezungumzia gharama nyingi zilizotumika kutimiza azma ya Mtanzania kupiga kura kama makaratasi, mafuta, kulipa watu wote wanaohusuka na mchakato wa upigaji kura na kadhalika.

Kawishe amesema yote hayo ni kumuwezesha mtanzania kupiga kura hivyo japo inabaki hiari lakini ni muhimu sana kwenda vituoni kupiga kura na kuwasihi baada ya zoezi kila mtu akaendelee na ratiba zake.

Pia ndugu Kawishe amewakumbusha watu wote kuwa kipindi cha uchaguzi sheria za nchi zinaendelea kufanya kazi.
Ujinga mkubwa wa NEC mnachezea uchaguzi, mnawachagulia watu kwa kuwaengua wagombea halafu mnasema watu wajitokeze kwa wingi kupiga kura?! Inaudhi sana.
 
Back
Top Bottom