Uchaguzi 2020 TUME: Pamoja na kwamba kupiga kura hiari, Serikali imeingia gharama kubwa sana. Tunawasihi Watanzania wakapige kura

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,444
7,808
Mkurugenzi wa tume ya Taifa ya uchaguzi upande wa huduma, Emmanuel Kawishe anaongelea mambo kadhaa kuelekea uchaguzi mkuu na amezungumzia gharama nyingi zilizotumika kutimiza azma ya Mtanzania kupiga kura kama makaratasi, mafuta, kulipa watu wote wanaohusuka na mchakato wa upigaji kura na kadhalika.

Kawishe amesema yote hayo ni kumuwezesha mtanzania kupiga kura hivyo japo inabaki hiari lakini ni muhimu sana kwenda vituoni kupiga kura na kuwasihi baada ya zoezi kila mtu akaendelee na ratiba zake.

Pia ndugu Kawishe amewakumbusha watu wote kuwa kipindi cha uchaguzi sheria za nchi zinaendelea kufanya kazi.
 
Tatizo hapo ninaloliona ni lile la mtu akapige kura kituo alichojiandikishia. Sijui kama kweli tehama imetusaidia nini kwenye hii tume.

Mi nimepewa link tu ya kuangalia kama ni mpiga kura na nimefanikisha.

Sasa inashindikana nini kupiga kura kituo chochote kwani ukitaka kumuona kuwa ni mpiga kura unaona tu kama ni halali au haramu?
 
Waahidi kwanza kuziheshimu hizo kura zetu ndiyo waje watushawishi kupiga kura. Yaani tume yenyewe imejaa mikada kindakindaki ya CCM halafu kirahisi tu tushawishike kupiga kura!

Watuambie kama wako tayari kumtangaza mshindi halali halafu wataona tutakavyo miminika siku hiyo kwenye vituo vya kupigia kura. Hata sisi tuliosafiri, aisee tutarudi kwa kasi ya ajabu ili tu kupigia MABADILIKO.
 
Mkurugenzi wa tume ya Taifa ya uchaguzi upande wa huduma, Emmanuel Kawishe anaongelea mambo kadhaa kuelekea uchaguzi mkuu na amezungumzia gharama nyingi zilizotumika kutimiza azma ya mtanzania kupiga kura kama makaratasi, mafuta, kulipa watu wote wanaohusuka na mchakato wa upigaji kura na kadhalika...
Ninakubaliana na serikali katika suala hili.

Ila najiuliza ina maana Watanzania wote tukipiga kura hizo gharama zitarudi ?
 
Kwa hili ambalo hamtendi haki kuanzia kwa kuengua kwa makusudi makada wa vyama vingine na kusema hatuwezi kuchagua mtu atakayeuza madini yetu inafanya watu wasiwe na mwamko wa kupiga kura. Ni ukweli husiopingika kwamba mmewekwa na CCM na lazima mtendee haki CCM yenu.

Tupo nyuma sana katika kufikia uchaguzi wa haki nchi hii na tusipoangalia huko mbele sijui mambo yatakuwaje. Msipofanya haki mnajenga kizazi cha chuki ndiyo maanaa watu wanaanza kuuana bila sababu.
 
Mkurugenzi wa tume ya Taifa ya uchaguzi upande wa huduma, Emmanuel Kawishe anaongelea mambo kadhaa kuelekea uchaguzi mkuu na amezungumzia gharama nyingi zilizotumika kutimiza azma ya mtanzania kupiga kura kama makaratasi, mafuta, kulipa watu wote wanaohusuka na mchakato wa upigaji kura na kadhalika...
Kupiga kura sio tatizo, tatizo ni kuhesabiwa kura yako. An ndio tunatumia uchaguzi kama njia moja ya Power Laundering (kutakatisha madaraka?
 
Mkurugenzi wa tume ya Taifa ya uchaguzi upande wa huduma, Emmanuel Kawishe anaongelea mambo kadhaa kuelekea uchaguzi mkuu na amezungumzia gharama nyingi zilizotumika kutimiza azma ya mtanzania kupiga kura kama makaratasi, mafuta, kulipa watu wote wanaohusuka na mchakato wa upigaji kura na kadhalika...
'Ballot papers' karatasi za kupigia kura nani anazitengeneza?
 
Wapo wanaotaka kulinda kura baada ya kupiga na
Wapo ambao hawataki kulinda kura.
 
Tume hakikisheni na mchakato mzima unakuwa huru na wa haki, mnaweza kuingia gharama kubwa zaidi ya hii ya sasa.
 
Sisi Watanzania tuko tayari kupiga kura tatizo linalotuudisha nyuma ni hilo litume figisu unaloliongoza.
 
Back
Top Bottom