Tume mmetudharirisha sana kumdai Tr 110 mwenye mtaji wa tr 2.6!!

Watanzania kama wewe.mnatakiwa mpelekwe kibiti.
Eti acacia wana mtaji wa tr 2.
Hyo ni hela ya masanduku kadhaa ya dhahabj
 
Tuacheni viherehere na ujuaji mwingi.tungoje mwisho wake,
Hzo sheria zenu mlizisomea chini ya miti.haziwezi kufanya kazi kwenye ili.
 
Tatizo kubwa hii serikali ya awamu ya 5 imejaa uwongo asilimia 80% kick ziko very sasa wanasingizia kila jambo... Badilisha hizo policy zako bana aaahh...
 
Elimu ya darasani tumefundishwa na wazungu, hizi phd sijui profesa zote wametwambia wazungu!! Ila unapofikia hatua ukawa profesa ujue unaheshimika dunia nzima!! Lakin nahisi uprofesa wa waafrika hauna thamani sawa na wa wazungu!! Kwa kamati zile za mheshimiwa rais kuandika mahesabu makubwa makubwa ya matrillion inatia shaka usomi wetu.

Kwa mahesabu waliopiga maprofesa wetu wanaihakikishia dunia kwamba Tanzania kuna dhahabu kama mchanga unachota tu!! Kwa mahesabu yao wana maana sisi ndio tunaongoza kwa uzalishaji wa madini dunia nzima. Je , ni ya kweli hayo?? Hawa ACACIA wana mtaji wa trillion 2.6 tzs et tunawadai trillion 110tzs !! Haiji hata kidogo!! Najua mtakuja kuniambia ni hesabu ya miaka karibia 20 sawa! Je huyu unaemdai hiyo mihela si ina maana amevuna zaid ya hizo ziko wap?? Nae alipaswa awe na mihela zaid ya hiyo!!

Kampuni kubwa dunian ya migodi BHP ina thamani ya sh trillion 200, kwa hesabu za hawa wachumi wetu wana maana ACACIA INA ZAID YA TRILLION 300!! Si kutudharirisha huku!! Wazungu wakisikia manamba tunayopiga wanakufa na vicheko na kutuona kama vichaa . Wanaulizana hawa watu wanaijua hiyo hela wanayoitamka?? Tafadhari wasomi wetu hata kama ni kuongeza sifuri sio kwa kiwango hicho . Tunachekwa sana huko dunian wakisikia tunamdai mtu mwenye mtaji wa 2.6 atupe 110!! Wanatucheka kwa dharau!! Na kumbukeni hesabu hizi zinahusu mchanga tu!!

Sasa kama mchanga ambao unathamani ndogo kuliko dhahabu yenyewe tunawadai hela hiyo, je dhahabu yenyewe tumezalisha yenye thamani ya sh ngapi??? Mimi nahisi maprofesa wetu hata figa kwa hela za kwetu wangeshindwa kuziweka !! Maana inazidi trillio elfu moja. Na hapo mkumbuke tunaongelea migodi mitatu tu!!! Inayomilikiwa na ACACIA.

Chonde chonde wasomi wetu msitudharirishe!! Mnapodanganya muwe mnakaribiana na ukweli. Kwa hizi hesabu zenu ni sawa na muuza genge la nyanya kuripoti polisi kaibiwa million 20 wakati kavamiwa na mteja wake huku mtaji wake ulio mezani haufiki hata laki moja!!

Namalizia kwa kusema hivi!! Hata mkeshe kupiga hesabu na hawa ACACIA HATA TRILLION MOJA HATUPATI ng'oooo!!
Uraia wako unatia mashaka!
 
tikatika

= mmetudhalilisha

Wewe nae unajidhalilisha, hata lugha yako ya taifa inakushinda kuandika vizuri.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Back
Top Bottom