Tume jumbe hizi kwa simu na emaili kwa ajili ya kumpigia chapuo dr. Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume jumbe hizi kwa simu na emaili kwa ajili ya kumpigia chapuo dr. Slaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MULANGIRA, Oct 11, 2010.

 1. M

  MULANGIRA Member

  #1
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimetumiwa jumbe hizi na mtu mmoja juu ya ndugu yetu Dr. Wilbroad Slaa na kupambana na kampeni chafu za teja Miraji Kikwete na wenzake. Anaomba zisambazwe kwa emaili na ujumbe wa CCM moja moja ili ziwe na nguvu na mguso mkubwa. Kazi kwetu!

  @font-face { font-family: "Times New Roman"; }p.MsoNormal, li.MsoNormal, div.MsoNormal { margin: 0in 0in 0.0001pt; font-size: 12pt; font-family: "Times New Roman"; }table.MsoNormalTable { font-size: 10pt; font-family: "Times New Roman"; }div.Section1 { page: Section1; }ol { margin-bottom: 0in; }ul { margin-bottom: 0in; }
  1. Kuzuia Tanzania isiwe nchi ya kifalme, au ya kichifu na ya wachache, mchague Dr. Slaa na Chadema.


  1. Tanzania ni yetu sote si ya Kikwete, Salma, na Ridhiwani, Mchague Dr. Slaa ili tuilinde Tanzania yetu!


  1. Kikwete amesema hajui kwa nini nchi yetu ni maskini sasa atauondoaje umaskini wetu? Mpumzishe kwa kumchagua Dr. Slaa kiongozi ajuaye namna ya kuuondoa.


  1. Tanzania nilikukosea kwa kukupa viongozi wabovu na mafisadi, Nisamehe. Sasa nitamchagua kiongozi makini anayestahili jina lako, Dr. Slaa!


  1. Watoto wa Tanzania ni watoto wetu sote hivyo wanastahili elimu bora tutakayoilipia kwa kodi zetu, tumchague Dr. Slaa anayesimamia hilo.


  1. Mtanzania mwenzangu Mungu alikupa kila aina ya utajiri: madini, maziwa, mito, ardhi na maliasili mbona unaruhusu viharibiwe kwa kuchagua na kutawaliwa na viongozi mafisadi? Mchague Dr. Slaa kwa uongozi bora na makini.


  1. Mwalimu Nyerere alisema “kumchagua Raisi hatuchagui sura, na kama suala ni uzuri wa sura basi nenda kanywe naye chai!” tumchague Dr. Slaa asiyeuza sura!


  1. Madini yetu yanaendelea kuchukuliwa na wachukuaji kutoka nje huku Kikwete na CCM wakichekelea kama mazuzu! Dr. Slaa na Chadema watakomesha ufisadi huu tuwachague!


  1. “Ili tuendelee twahitaji watu, siasa safi na uongozi bora”, Mwalimu alisema. Hatujaendelea kutokana na siasa na uongozi mbaya na wa kifisadi wa CCM, tuchague uongozi bora wa Dr. Slaa na Chadema.


  1. Zuia wizi wa kura za Dr. Slaa na Mbunge wa Chadema kwa kuwapigia kura, kulinda kura na kuzuia vurugu na uchakachuaji kura vituoni.
  2. [FONT=&quot]Uraisi si kubembea kwenye BEMBEA bali ni kuwatumikia na kuwapigania watu wako. Dr. Slaa si mbembeaji au mtalii kama Kikwete, tumchague. [/FONT]
   
 2. R

  Rugemeleza Verified User

  #2
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Asante Mulangira na karibu kwenye ukumbi wa watu makini. Nimeziona na nitasambaza ili mwaka huu kieleweke.
   
 3. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #3
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  hofu na shaka ondoa, watazisoma watz.
   
Loading...