Mr. Politician
Member
- May 16, 2008
- 74
- 7
Jamani mimi sasa nachanganyikiwa na sielewi kabisa nini ni nini nani ni nani na nani anatakiwa awe nani. Lilipotokea suala la EPA ambapo mabilioni ya Watz yamethibitika kuibiwa, serikali yetu iligoma kabisa kwa suala hilo kuchukuliwa na idara zinazohusika yaani mahakama na jeshi letu la polisi kufanya uchunguzi, pia yapo masuala mengine mengi ambayo serikali haitaki kuwashikilia watuhumiwa eti bado uchunguzi unaendele mfano "Marehemu" Ballali. Lakini lilipokuja hili suala la jengo kumomonyoka kisutu tayari watuhumiwa waeshakamatwa na kufikishwa mahakamani. Je hawa si kama hawa wengine wa ufisadi wa pesa zetu za epa? Maana kama ni kuua na wenyewe wanaua wajawazito na watoto kibao kwa kukosa dawa kwenye hospital zetu. Je ni haifai na wenyewe kuwashitaki kwa kuua bila kukusudia?
Ni hayo tu.
Ni hayo tu.