Uchaguzi 2020 Tume iwaapishe mawakala wa vyama vyote bila upendeleo

NCCR Mageuzi

Member
Oct 3, 2007
23
63
Na, Sam Ruhuza,

Leo Mawakala wa vyama vya siasa kwenye uchaguzi Mkuu 28/10/2020 wanatakiwa kuapishwa. Sheria inasema wazi wataapishwa na msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri AU msimamizi msaidizi wa Kata ambaye ni Mtendaji wa Kata.

Malalamiko yameanza kuwa mengi toka Majimboni kuwa Wasimamizi wamewaambia Viongozi wa vyama saa nne asubuhi wakusanye Mawakala wao kwenye Makao Makuu ya Tarafa zao ndipo wataapishwa na wakichelewa hawatapata nafasi ya uwakala.

Vijijini huko sio rahisi kuwakusanya watu kutoka Kata kwenda tarafa kwa muda wa saa moja na usafiri hakuna na tarafa ni zaidi ya kilometa 20. Sehemu nyingine wanafika sehemu ya kuapishwa, msimamizi wa uchaguzi hayupo na hapatikani kwenye simu wala taarifa zake!

Sehemu zingine Mawakala wanakataliwa na msimamizi kuwa hawatambui aidha kwa utambulisho wa barua au kwa yeye mwenyewe! Na msimamizi anatangaza hivyo vituo kutokuwa na Mawakala wa vyama hivyo!

Ajabu ni kwamba kasheshe zote hizo, wanajikuta vyama vya upinzani tu! Chama tawala Mawakala wao hata hawapo kwenye hizo sehemu zenye matatizo, sijui wao wamefuatwa kuapishwa AU waliapa mapema AU hawataapishwa! Haieleweki!

Tume ya Uchaguzi hiki ni kipindi chenu cha kutoa Haki ili amani iwepo na ninyi ndio wa kunyima Haki ili amani itoweke, ni Tume ya Uchaguzi kuamua kufuata njia ipi!!

Nakumbuka Akwilina aliuawa Kinondoni baada ya Mawakala kutembea kwenda kwa msimamizi kudai haki yao ya kuapishwa, matokeo vurugu ya kuwazuia na kufyatua risasi ikamkuta Akwirina Binti aliyekuwa kwenye Daladala ambaye hakuwa kabisa kwenye hayo maandamano, akakatizwa maisha yake ghafla! RIP

Tume ya Uchaguzi kuweni makini na maisha ya watu. Watanzania wanapenda sana Amani, toeni haki na ionekane haki imetolewa. Msiharibu amani waathirika watakuwa wengine!

Tume ya Uchaguzi waapishe Mawakala wa vyama vyote kwa kutoa haki bila upendeleo wowote maana kuna maisha baada ya uchaguzi!

Tanzania ni yetu sote
nccrmageuziofficial_120373799_134461531702653_8990011528190213606_n.jpg
 
Na mchezo ndio unaanzia hapo, mchezo wa pili utakuwa pale kwenye kutumia leseni na vitambulisho vya NIDA kupigia kura.

Nimedokezwa kwanini waliamua kufanya hivyo

Sent from my Infinix X624B using JamiiForums mobile app
 
Nyie NCCR si ndio mliahidiwa kuwa chama kikuu cha upinzani mkaamua kukubaliana na utapeli wa Magufuli. Lengo ilikuwa ni kugomea uchaguzi hadi tume huru, lakini mkakubali kutumika ili mshiriki uchaguzi kuua nguvu ya madai ya tume huru. Sasa mnalia baada ya kuona ahadi mliyopewa mmeachwa kwenye mataa. Ingizeni wanaNCCR mageuzi mtaani madai kuapishwa
 
Back
Top Bottom