Tume huru ya uchaguzi wa ndani CHADEMA


Fungo N.

Fungo N.

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Messages
252
Points
170
Fungo N.

Fungo N.

JF-Expert Member
Joined May 20, 2011
252 170
Hili ni wazo langu_KAMA inawezekana CHADEMA kiunde tume itakayokuwa inaandaa;kuratibu na kusimamia chaguzi mbalimbali za ndani ya CHADEMA.Democrasia ikianzia ndani ya chama itahamia pia katika ngazi ya taifa.

NAWASILISHA/mawazo yenu yawe ya kujenga zaidi
 
PhD

PhD

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2009
Messages
3,908
Points
2,000
PhD

PhD

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2009
3,908 2,000
Iwapo zitto angegombea na mbowe last time alikuwa na dalili zote za kumshinda Bwana mbowe, ushahidi wa kimazingira na kinadharia unathibitisha hoja hii
 
Kurunzi

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Messages
4,607
Points
2,000
Age
39
Kurunzi

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2009
4,607 2,000
Ni wazo zuri sana tume huru ambao wajumbe wake si lazima wawe wajumbe wa halmashauri au mkutano mkuu.
 
Kibanga Ampiga Mkoloni

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2007
Messages
16,712
Points
2,000
Kibanga Ampiga Mkoloni

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2007
16,712 2,000
Iwapo zitto angegombea na mbowe last time alikuwa na dalili zote za kumshinda Bwana mbowe, ushahidi wa kimazingira na kinadharia unathibitisha hoja hii
Ndio mchango wako au umeamua makusudi kuharibu mada?
 
AdvocateFi

AdvocateFi

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Messages
11,344
Points
2,000
AdvocateFi

AdvocateFi

JF-Expert Member
Joined Jan 15, 2012
11,344 2,000
Una uhakika gani ndani ya CHADEMA hakuna tume huru ya uchaguzi?
Subiri nikueleze w zumbukuku kuwa kila chama kina tamaduni zake mbali na uwepo wa demokrasia, Nipe mfano wa chama kimoja tu unachokijua duniani, kuzimu na mbinguni ambacho kina demokrasia ambayo haina utamaduni wake.
Hata wagiriki wenyewe kule mpaka leo bado definition ya demokrasia ni kitendawili alafu we juha mmoja uje hapa na utumbo huu eti oooh..!demokrasia.
 
M

majebere

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
4,648
Points
2,000
M

majebere

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
4,648 2,000
CDM ni mali ya Mtei,yeye ndio muamuzi.
 
Fungo N.

Fungo N.

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Messages
252
Points
170
Fungo N.

Fungo N.

JF-Expert Member
Joined May 20, 2011
252 170
Una uhakika gani ndani ya CHADEMA hakuna tume huru ya uchaguzi?
Subiri nikueleze w zumbukuku kuwa kila chama kina tamaduni zake mbali na uwepo wa demokrasia, Nipe mfano wa chama kimoja tu unachokijua duniani, kuzimu na mbinguni ambacho kina demokrasia ambayo haina utamaduni wake.
Hata wagiriki wenyewe kule mpaka leo bado definition ya demokrasia ni kitendawili alafu we juha mmoja uje hapa na utumbo huu eti oooh..!demokrasia.
jaribu kujenga hoja na siyo kukimbilia matusi hakika nyie ndo mnao rudisha nyuma harakati za cdm
 
Havizya

Havizya

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Messages
1,676
Points
1,500
Havizya

Havizya

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2012
1,676 1,500
Ccm ndiyo yenye domokorasia, ndiyo maana mwenyekiti hana mpinzani. Huteuliwa, kisha huchaguliwa, NYAMBAF.
 
Nanyaro Ephata

Nanyaro Ephata

Verified Member
Joined
Jan 22, 2011
Messages
997
Points
250
Age
41
Nanyaro Ephata

Nanyaro Ephata

Verified Member
Joined Jan 22, 2011
997 250
Ndani ya CHADEMA kuna kurugenzi ya uchaguzi na kampeni,ndio inaratibu shughuli zote za uchaguzi na kampeni
 
D

Dawa ya Mjinga

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Messages
382
Points
195
D

Dawa ya Mjinga

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2009
382 195
Hili ni wazo langu_KAMA inawezekana CHADEMA kiunde tume itakayokuwa inaandaa;kuratibu na kusimamia chaguzi mbalimbali za ndani ya CHADEMA.Democrasia ikianzia ndani ya chama itahamia pia katika ngazi ya taifa.

NAWASILISHA/mawazo yenu yawe ya kujenga zaidi


Inabidi kwanza utoe tafsiri inayokubalika ya baadhi ya maneno uliyotumia. Kwanza demokrasia maana yake nini? Tume huru ya uchaguzi ni kitu gani? Je, una maana kuwa usimamizi wa sasa wa uchaguzi ndani ya CHADEMA si wa kidemokrasia?

Binafsi sina tafsiri halisi ya neno demokrasia. Lakini nadhani ni uatawala wa watu, uliowekwa na watu kwa ajili ya watu. Hata hivyo ninafahamu kwa uhakika zaidi kuwa demokrasia ina misingi miwili. Mosi ni wengi kusikiliza mawazo ya wachache na pili ni wachache kutii maamuzi ya wengi. Hivyo basi ili demokrasia itawale lazima misingi hii miwili muhimu izingatiwe na ishamiri. Hapo ndipo kinapokuwa kitendawili cha tume huru ya uchaguzi ndani ya chama. Itapata wapi uhuru kwa misingi ya kidemokrasia? Maana pamoja na kuwa wachache watasikilizwa lakini mwisho wa siku wengi ndio watakaoamua namna na hali ya tume hiyo. Kwa misingi ya kidemokrasia haiwezi kuwa huru dhidi ya uamuzi wa wengi. Itaundwa na itabebwa na maamuzi ya wengi. Kwa mantiki hiyo hakuna tume huru labda katika mfumo wa kidikteta ambao nao ni mashaka makubwa kupata tume ya namna hiyo. Unapataje tume huru (isiyofungamana na maamuzi ya kidemokrasia?)
Kama kweli unazungumzia demokrasia, sina shaka kuwa mfumo wa uchaguzi uliopo CHADEMA hivi sasa ulitokana na maamuzi ya wengi ndani ya chama - ambao ni msingi wa demokrasia. Pia ninaamini kuwa wachache ambao hawakubaliani na mfumo huo walipata fursa waswaa ya kusikilizwa na hatimaye uamuzi ukafanyika na unastahili kuheshimiwa ili kutunza demokrasia.
Baada ya kueleza haya, kila chama lazima kiwe makini kwenye masuala ya uchaguzi hasa baada ya kufahamika kuwa FISI WENU siku zote wana njama ya kuchakachua uchaguzi (ambao si msingi wa demokrasia) ndani ya vyama vya upinzani na hasa CHADEMA ili kuvuruga. Hii wala sio siri tena kwa watu wanaofuatilia nyendo za kisiasa nchini mwetu. Kuweka tume huru, tujiulize iwe huru dhidi ya nini? Dhidi ya chama, viongozi au wanachama? Kwa maoni yangu tume ikiwa huru dhidi ya FISI WENU inatosha na ni muhimu zaidi kuliko jambo lolote lingine.
Kwa upande wa taifa ni tofauti. Tunahitaji tume huru mbali na FISI WENU. Tume huru mbali na dola (serikali na vyombo vyake), mbali na uchakachuaji na isiyofungamana na chama chochote cha siasa au kikundi cha watu bali ifungamane na wapiga kura. Kwa maana kuwa baada ya kuwasikiliza wenzetu wachache wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi, tume hii iheshimu maamuzi ya wengi tunapopiga kura zetu kwa kuzihesabu kikamilifu bila kuchakachua wala kumuwezesha mmoja wa hao wanaowania nafasi kushinikiza awe mshindi. Huu ndio uhuru ninaoujua. Uhuru pia uwepo kwenye uwazi wa shughuli yenyewe ya uchaguzi na hasa kutangaza matokeo kwenye vituo vya kupiga kura. Hakuna sababu (zaidi ya kutaka kuchakachua kura) eti kura za uraisi zisitangazwe vituoni. Hii ni sheria ya kihayawani kabisa. Kura ni zetu sisi tuliopiga halafu tusijue tumemchagua nani?
Mwisho, hoja yako kuwa mfumo huo wa tume huru kutoka kwenye chama utahamia kwenye ngazi ya taifa, sio kweli. Sababu ni kuwa kwenye taifa watu wote sio wanachama wa vyama vya siasa ambapo kwenye chama kila mmoja ni mwanachama. Hivyo ni rahisi kuweka vigezo vya namna ya kumpata mshiriki wa tume huru ya uchaguzi ndani ya taifa kuliko katika chama. Hata kama ikibidi wanatume huru ya uchaguzi ya taifa wawe wanachama wa vyama vya siasa ni rahisi kuweka uwiano (ingawa hapo uchakachuaji unapata gate la kuingilia) wa vyama mbalimbali ambapo sijui namna ya kuweka uwiano wa aina yoyote ndani ya chama. Hivyo tume huru ndani ya chama cha siasa ni wazo zuri na ndoto njema lakini utekelezaji wake unabaki kuwa ndoto.
 
T

tenende

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2012
Messages
6,556
Points
1,195
T

tenende

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2012
6,556 1,195
CCM wana tume huru inaongozwa na fungo, Ritz na majebere. Mwaka 2015 watahamia CUF kuongoza tume. Akishinda kugombea urais membe, magufuli, mzee 6 au luwasa watasema CCM hakuna demokrasia!
 
M

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
13,355
Points
2,000
M

Molemo

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
13,355 2,000
Peleka hoja yako Magambani kwanza.
 
Alfred Daud Pigangoma

Alfred Daud Pigangoma

Verified Member
Joined
Mar 30, 2009
Messages
1,792
Points
1,250
Alfred Daud Pigangoma

Alfred Daud Pigangoma

Verified Member
Joined Mar 30, 2009
1,792 1,250
Mleta mada anafanyakazi ya kutoa-dog au kupala-sugarcane.
 
Aggrey86

Aggrey86

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2011
Messages
855
Points
195
Aggrey86

Aggrey86

JF-Expert Member
Joined Jun 26, 2011
855 195
Una uhakika gani ndani ya CHADEMA hakuna tume huru ya uchaguzi?
Subiri nikueleze w zumbukuku kuwa kila chama kina tamaduni zake mbali na uwepo wa demokrasia, Nipe mfano wa chama kimoja tu unachokijua duniani, kuzimu na mbinguni ambacho kina demokrasia ambayo haina utamaduni wake.
Hata wagiriki wenyewe kule mpaka leo bado definition ya demokrasia ni kitendawili alafu we juha mmoja uje hapa na utumbo huu eti oooh..!demokrasia.......
Kwani ugomvi mkuu?mdau katoa mawazo ya kujenga na si kubomoa jenga hoja bwana na si kutukana tukana!
 
Fungo N.

Fungo N.

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Messages
252
Points
170
Fungo N.

Fungo N.

JF-Expert Member
Joined May 20, 2011
252 170
ni ujinga kudhani kila anaetoa maoni juu ya cdm au kuikosoa cdm ni pandikizi la nape.Uchaguzi mkuu wa viongozi wa chama ujao utakuwa na changamoto sn kwa chama pengine kuliko wakati wowote.JAMANI TUFUATILIE HISTORIA YA NCCR MAGEUZI
 
Mimibaba

Mimibaba

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2009
Messages
4,559
Points
0
Mimibaba

Mimibaba

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2009
4,559 0
ni ujinga kudhani kila anaetoa maoni juu ya cdm au kuikosoa cdm ni pandikizi la nape.Uchaguzi mkuu wa viongozi wa chama ujao utakuwa na changamoto sn kwa chama pengine kuliko wakati wowote.JAMANI TUFUATILIE HISTORIA YA NCCR MAGEUZI
Nimeelewa hoja yako unataka Tume Huru inayosimamiwa na CCM maana mfumo wa CDM siyo huru. Nakuomba pendekeza Tume Huru unayotaka maana sisi wengine tunaridhika na mfumo na taratibu za uongozi kwa sababu zimeweza kutupa viongozi bora kupita wa CCM
 

Forum statistics

Threads 1,283,751
Members 493,810
Posts 30,799,802
Top