Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania: Kweli itaweza kuwa suluhisho kukubali matokeo ya uchaguzi?

Kikiwo

JF-Expert Member
Nov 30, 2017
1,967
1,046
Wana JF, nimejaribu kuwaza sisi Tanzania katika nchi za Africa tunaosemekana kwamba ni "Third World Countries" mara nyingi tumekariri kwamba ili matokeo ya uchaguzi yakubalike na vyama vyote vinavyokuwa vinashiriki uchaguzi, ni lazima kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi

Wenzetu wazungu (USA, U.K etc) waliotuchorea mstari kwamba sisi Africa ni Dunia ya Tatu - Third World Countries wao wakajiweka First World Countries nikafikiri wao issue ya kuheshimu Demokrasia na Uhuru wote katika uchaguzi kwa kuweka hizo Tume za Uchaguzi nikadhani wao wameshafaulu huo mtiani - Exams.

Uchaguzi uliofanyika kule America ukiambatana na mabishano ya wizi wa kura katika wagombea Urais kati ya Donald Trump na Joe Biden, nimegundua kwamba kumbe wote (Africa - Third World Countries na First world Countries) bado hatujaweza kuwa na uhakika kwamba solution ya kuondoa mabishano katika chaguzi zetu ni kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi.

Lakini ngoja tusubiri tuone huko America - US hiyo tarehe 20 January 2020 nani ataapishwa kama Rais halali wa nchi ya First World .

Yetu macho twendelee kujifunza hadi tufikie huko kwa wenzetu walioendelea.

By JF Member
 
Wana JF, nimejaribu kuwaza sisi Tanzania katika nchi za Africa tunaosemekana kwamba ni "Third World Countries" mara nyingi tumekariri kwamba ili matokeo ya uchaguzi yakubalike na vyama vyote vinavyokuwa vinashiriki uchaguzi, ni lazima kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi...
Swali zuri sana; jibu lake ni kuwa hakuna. Inategemea sana wagombea wenyewe wana mapenzi gani kwa nchi; wasiokuwa na mapenzi kama vile Trump na Lissu watakimbilia kudai wameibiwa kura ili wajiridhishe matakwa yao binafsi, na wale wenye mapenzi kama George H.W. Bush na Queen Sendiga watakubalina na matokea kutoa ushirikiano kwa aliyeshinda.
 
Umeona USA wagombea wanakamatwa na kubambikwa kesi? kuna mtu amepita bila kupingwa Marekani?
 
TUME HURU YA UCHAGUZI itasaidia sana, maake haitapokea maagizo kutoka juu au kutoka kwa Raisi aliyepo madarakani. Itakuwa na uwezo wa kutumia wasimamizi wa uchaguzi jimbon wa ajila za mda sio wakurugenz ambao mi wateule wa raisi.

Mbunge au Raisi mpk apatikane atakuwa amepitia tanuru la kweli kweli. Angalia Kenya hawana ujinga huo. Angalia USA raisi aliyepo madarakan hana cha kufanya, hiyo ni MIFUMO YA UCHAGUZI inambana haipokei maagizo.
 
Sidhani kama Tume huru pekee ni suluhisho la haya mambo ya kipuuzi ya uchaguzi.

Suluhisho la kudumu badiliko la kifikra kwa watu wote badala ya hali tuliyonayo hivi sasa.

Hatupaswi kwenda mbali aliyeharibu uchaguzi huu ni Tume ya Uchaguzi kwa kuweka kanuni kandamizi na zinazowezesha wizi wa kura.
 
Swali zuri sana; jibu lake ni kuwa hakuna. Inategemea sana wagombea wenyewe wana mapenzi gani kwa nchi; wasiokuwa na mapenzi kama vile Trump na Lissu watakimbilia kudai wameibiwa kura ili wajiridhishe matakwa yao binafsi, na wale wenye mapenzi kama George H.W. Bush na Queen Sendiga watakubalina na matokea kutoa ushirikiano kwa aliyeshinda.
WaTanzania wanashida kubwa sana vichwani mwao, unaweza kuta wewe ni kiongozi flani hapa Tanzania. Mwenye akili timamu hawezi kusapoti ujinga wa Tume yetu ya Uchaguzi.
 
Wana JF, nimejaribu kuwaza sisi Tanzania katika nchi za Africa tunaosemekana kwamba ni "Third World Countries" mara nyingi tumekariri kwamba ili matokeo ya uchaguzi yakubalike na vyama vyote vinavyokuwa vinashiriki uchaguzi, ni lazima kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi

Wenzetu wazungu (USA, U.K etc) waliotuchorea mstari kwamba sisi Africa ni Dunia ya Tatu - Third World Countries wao wakajiweka First World Countries nikafikiri wao issue ya kuheshimu Demokrasia na Uhuru wote katika uchaguzi kwa kuweka hizo Tume za Uchaguzi nikadhani wao wameshafaulu huo mtiani - Exams.

Uchaguzi uliofanyika kule America ukiambatana na mabishano ya wizi wa kura katika wagombea Urais kati ya Donald Trump na Joe Biden, nimegundua kwamba kumbe wote (Africa - Third World Countries na First world Countries) bado hatujaweza kuwa na uhakika kwamba solution ya kuondoa mabishano katika chaguzi zetu ni kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi.

Lakini ngoja tusubiri tuone huko America - US hiyo tarehe 20 January 2020 nani ataapishwa kama Rais halali wa nchi ya First World .

Yetu macho twendelee kujifunza hadi tufikie huko kwa wenzetu walioendelea.

By JF Member
Mkuu,

Hakuna kitu kinaitwa tume huru iwapo itaundwa na wajumbe kutoka wajumbe wa vyama mbalimbali vya siasa, taasisi mbalimbali, mashirika yasiyo ya kiserikali, watalaamu mbalimbali wenye mtizamo wa kisisa hiyo inaitwa 'TUME SHIRIKISHI'

Tume huru inateuliwa au kuundwa na chombo kisicho na nasaba na serikali lakini kikihusisha watalaamu maalumu wanaoongozwa na sera ya Taifa. Tanzania hakuna sera ya jumla ambayo chama chochote cha siasa kikishika madaraka kitatekeleza hivyo hicho kinachodaiwa hakiwezekani kutokea mpaka katiba itamke hivyo.

Mabadiliko ya katiba kwa kufuata matakwa ya wanasiasa sio suluhuhisho la kupata tume huru zaidi ya kuunda kikundi cha zogo na malumbano yasiyo na tija.

Utaratibu mpya shirikishi ndio unaotakiwa kuwekwa baada ya kuwashirikisha kikamilifu wananchi na kuridhia bila kupindisha kilichokubaliwa kwa utekelezaji.
 
CCM haiwezi kushinda uchaguzi wowote wa halali
Sasa tukiwa na mawazo kama haya kwamba ccm haiwezi kushinda uchaguzi kama kuna Tume huru ikafika mahala tukawa na Tume huru ya uchaguzi alafu wa CCM wakashinda sasa hapo tutabaki kusingizia nini?
 
Sasa kule America ile tume mbona ni Tume Huru na rais aliyoko madarakani anadai kaibiwa kura zake na mpinzani wake?
Hicho ndo kichekesho cha mwaka wa 2020 kusikia Rais aliyoko madarakani kulalamika kuibiwa kura na mpinzani. Hapo Mh.Trumph katuachia kioja cha mwaka.
 
Wana JF, nimejaribu kuwaza sisi Tanzania katika nchi za Africa tunaosemekana kwamba ni "Third World Countries" mara nyingi tumekariri kwamba ili matokeo ya uchaguzi yakubalike na vyama vyote vinavyokuwa vinashiriki uchaguzi, ni lazima kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi

Wenzetu wazungu (USA, U.K etc) waliotuchorea mstari kwamba sisi Africa ni Dunia ya Tatu - Third World Countries wao wakajiweka First World Countries nikafikiri wao issue ya kuheshimu Demokrasia na Uhuru wote katika uchaguzi kwa kuweka hizo Tume za Uchaguzi nikadhani wao wameshafaulu huo mtiani - Exams.

Uchaguzi uliofanyika kule America ukiambatana na mabishano ya wizi wa kura katika wagombea Urais kati ya Donald Trump na Joe Biden, nimegundua kwamba kumbe wote (Africa - Third World Countries na First world Countries) bado hatujaweza kuwa na uhakika kwamba solution ya kuondoa mabishano katika chaguzi zetu ni kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi.

Lakini ngoja tusubiri tuone huko America - US hiyo tarehe 20 January 2020 nani ataapishwa kama Rais halali wa nchi ya First World .

Yetu macho twendelee kujifunza hadi tufikie huko kwa wenzetu walioendelea.

By JF Member
Tunahitaji tume huru na mahakama ya kikatiba ambayo kazi yake ni kuthibitisha matokeo. Tume huru ni nini, Tume hii hutokana na watu wanaoomba kazi kwa ushindani wa misingi ya ajira, hawa hawateuliwi na rais. Ushindi wanaoutangaza lazima uthibitishwe na mahakama ya kikatiba, sisi watu wanapiga kura tume imekwisha mtangaza mshindi! Hapa hakuna kubisha.
 
Hicho ndo kichekesho cha mwaka wa 2020 kusikia Rais aliyoko madarakani kulalamika kuibiwa kura na mpinzani. Hapo Mh.Trumph katuachia kioja cha mwaka.
Hicho si kioja ni jambo la kawaida, na huko alikodai kaibiwa kura zimehesabiwa tena, wenzetu wanahesabu kwa mashine na mkono na marudio wamehesabu kwa mkono tu, sisi marufuku kurudia kuhesabu na polisi watasimamia hilo.
 
Tunahitaji tume huru na mahakama ya kikatiba ambayo kazi yake ni kuthibitisha matokeo. Tume huru ni nini, Tume hii hutokana na watu wanaoomba kazi kwa ushindani wa misingi ya ajira, hawa hawateuliwi na rais. Ushindi wanaoutangaza lazima uthibitishwe na mahakama ya kikatiba, sisi watu wanapiga kura tume imekwisha mtangaza mshindi! Hapa hakuna kubisha.
Mkuu,

Mawazo yako ni ya mlengo mmoja na yameathirika na itikadi yako uliyo nayo pamoja kukatishwa tamaa na mifumo iliyopo.

Umedai tume huru inapatikana kwa watu wenye sifa navigezo kuomba ajira kwa kushindanishwa;

Swali:
1. Tume ya ajira itakuwa chini ya serikali ipi?
2. Sheria hiyo itakuwa ni dhaifu kama katiba haijatamka hivyo
3. Tume inawajibika kwa nani
4. Vigezo na sifa zipi ambazo ungependelea viwekwe katika uundaji wa tume hiyo na vitapimwaje kuthibitisha mwombaji anastahili na wala sio mamluki wa taifa shindani au lenye nia OVU dhidi ya Tanzania na watu wake?
4. Katiba iliyopo ilitungwa na wawakilishi wa wananchi wenyewe na kuandikwa kwa lugha ya kisheria kwa kuzingatia mazingira ya kisiasa, kijamii na kiuchumi ya wakati huo na pengine hadi sasa maana iliyokuwa inapendekezwa ilikwamishwa na wanasiasa wenyewe sio wananchi
5. Watu wenye shida ni wanasiasa sio wanananchi, maana mwananchi akituma bungeni umwakilishe kumsemea kwamba anatakiwa asikilizwe maoni yake katika ushiriki wa ujenzi wa nchi na wewe ukapeleka blah blah nyingi ambazo kwenye lugha ya kisheria haiwezekani kutungiwa sheria utakuwa umeshiriki kumdhulumu mwananchi haki yake, ya kueleza nini kifanyika na kipi kisifanyike kwa sababu zipi

Hakuna kitu kinaitwa tume huru popote pale chini ya jua ila kuna tume shirikishe, tume elekezi na tume mwongozo

Tume ikiwa na wajumbe wenye mlengo wowote wa kiisiasa hata kama ikitenda haki kwa kuzingatia taratibu zilizokwe upande mwingine kinzani utahisi haki haikutendeka na hata ukijumuisha wajumbe kutoka kwenye watu wote wenye milengo tofauti ya kisiasa patakuwepo na msigano tu inapofikiwa kufanya uamuzi, rejea maamuzi kutoka bungeni, maamuzi ya wengi yanakubalika na mawazo ya wachache wanasikilizwa tu bila kuathiri uamuzi wa mlengo wa pili

Mpaka sasa hapa duniani hakuna mfumo sahihi, bora na wa kuaminika ambao unasimamia chaguzi za viongozi wa kisiasa.

Marekani hapana, maana inawezekana watu wengi wakakuchagua ambao ni raia wa kawaida lakini kikundi cha watu wachache wenye nguvu katika jamii, kiuchumi, kisiasa na kiusalama ndio wanaamua ni nani awe kiongozi hivyo hivyo kudhulumu maamuzi ya wengi

As an upcoming JF member with focussed and constructive opinions to the policy and decision makers appeals to the country administration deliberate pooling in a diversity of patriotic views recommending on how to docket our own african hybrid democratic administration that upholds cultural, customs, environmental geopolitics integrating the community advantageous to the stakeholders vying for leadership at different levels and abstain importing western democratic text which ruins unity, causes economic disparity through nuisance resistance that denies development to innocent citizens.
 
Back
Top Bottom