Trust None
JF-Expert Member
- Feb 12, 2018
- 1,260
- 4,415
Wapinzani wanajifariji tu lakini kwa Katiba ya sasa na Tume ya uchaguzi iliyopo pamoja na hali ya kisiasa iliyopo hivi sasa, hawawezi kupata viti hata robo ya vile walivyopata mwaka 2015 achilia mbali uraisi hawawezi kuuunusa kabisa.
Nashauri uongozi uliopo sasa hivi ujiuzuru mwezi Octoba 2020 halafu iundwe Serikali ya Mpito itakayohusisha vyama vyote vyenye uwakilishi Bungeni ili Serikali hiyo iwe na jukumu kuu la kuhakikisha inasimamia mchakato wa uundwaji wa katiba mpya na taasisi zake.
Hilo likiwezekana, nashauri ile RASIMU YA KWANZA YA WARIOBA ndiyo ifanyiwe kazi, ni nzuri na inayozingatia uzalendo tofauti na rasimu ya pili iliyochakachuliwa kwa maslahi ya wachache.
Kusema ukweli tungekuwa na katiba huru yenye kutambua taasisi huru, kusingekuwa na tabia ya mhimili mmoja kujichimbia chini zaidi huku mihimili mingine ikisifia tu kama ilivyotokea huko Ufaransa miaka ya 1600 pale King Louis xiv aliposema, "I Am The State And My Words Are Law"