Tume Huru ya Uchaguzi: Kambi Rasmi ya Upinzani ilikuwa wapi muda wote kupeleka Muswada Binafsi bungeni kuhusu jambo hilo?

Wamewahi kuwasilisha Mswada?
Wewe unataka tu kulowa mvua ya matusi, wewe ni mgeni na bunge la Tanzania hasa hili la mungufuli?
Kupelekwa mswada ni jambo jingine na kupitishwa ni jambo jingine.
Kwanza hiyo habari ya kusema walikua wapi haina mashiko sababu kuunda hiyo tume hata ndani ya wiki mbili inakuwa tayari imeshasukwa.
 
Mtoa mada fikilia wewe ndy mojawapo wa waunda serikali je huoni kwamba tume haiko huru?je kama Nia yako ni kutumikia wananchi kwa ueledi na uzalendo je kwanini usiendeshe mchakato wa tume huru?Kwanini usubiri wpinzani waseme ukweli unaoujua? Mwanasheria umejidhalilisha kwenye mada hii..mimi nilitegemea ninyi ndyoo mungekua wakwl kwa maana ndy mnajua sheria nini na katibu nini,na mapungufu yake lakini mumekua kinyume chake!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, Mbunge ana fursa ya kuwasilisha Mswada Bungeni. Yupi amefanya hivyo. Ndiyo hoja yangu
 
Mkuu, Mbunge ana fursa ya kuwasilisha Mswada Bungeni. Yupi amefanya hivyo. Ndiyo hoja yangu
Ni miswaada mingapi mizuri iliyopelekwa na wabunge wa Upinzani tena yenye maslahi makubwa ya Kitaifa lakini ikaishia kuwekwa kapuni.
Ingekuwa walau kufikia hatua ya kujadiliwa Bungeni hata kama isipite ingetia moyo, lakini hata ile hatua tu ya kusajiliwa na ofisi za Bunge hakuna, inakatisha tamaa sana.

Kuanzia ule wa Vijana na ule wa MAJI wa Mh Mnyika.
 
Mkuu, Mbunge ana fursa ya kuwasilisha Mswada Bungeni. Yupi amefanya hivyo. Ndiyo hoja yangu

..THEORETICALLY una hoja.

..lakini PRACTICALLY hauko sahihi.

..hili suala Katibu Mkuu Mh.Mnyika alishalitolea ufafanuzi.

..alieleza kwamba MAZINGIRA ya utendaji wa BUNGE letu, hoja ya Tume Huru ikiwasilishwa kama hoja binafsi na mbunge wa upinzani itakwamisha na Ofisi ya bunge.

..utakumbuka kwamba ofisi ya bunge imekuwa so HOSTILE kwa kambi ya upinzani kiasi kwamba huwakwamisha kwa kila namna na huzuia hata bajeti mbadala zisisomwe ktk vikao vya bunge.

..kwa hiyo pendekezo la Mh.Mnyika na vyama vya upinzani ni kwamba hoja ya Tume huru inapaswa kuwasilishwa na SERIKALI ili ipate nafasi ya kujadiliwa na hatimaye kupitishwa na wabunge.

..Kwa hiyo kambi ya upinzani wanaweza kuwasilisha hoja binafsi just to prove a point, lakini ni ukweli ulio wazi kwamba hoja hiyo haiwezi kupita bila kuwa imewasilishwa na SERIKALI.
 
Walikuwa wapi tangu mwaka 2015 kujenga hoja hii na haya kuwasilisha Muswada binafsi Bungeni kuhusu suala hilo? Kwanini nafasi hiyo ya Muswada binafsi haikutumika hadi sasa kuitaka Serikali kuwasilisha Muswada huu ya suala hilo kwa Hati ya Dharura?
Usiumize kichwa chadema hawajawahi kuwa serious hata siku moja
 
This is another garbage!

Hivi nyie watu hamna macho ya kuona wanayofanyiwa wapinzani na wanaharakati???

Pumba kabisa
Mpaka sasa sioni upinzani wa kweli. Wengi wanatetea maslahi binafsi, huo ndio ukweli. Nilitarajia awamu hii kungekuwa na mapambano ya dhati kabisa kutaka KATIBA MPYA, badala yake wapinzani wanaodhaniwa kuwa wapinzani wakaendekeza viajenda vyao vyepesi tu. Ni kama kikundi cha watu wasio na dira, ila ukiwaambia ukweli wanakuona huwapendi.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hofu yangu ni pale hiyo tume huru ikaundwa alafu bado jama wakashinda sijui upinzani tutaweka wapi uso wetu.
 
Kikatiba, kisheria na kikanuni Muswada binafsi unaruhusiwa kuwasilishwa Bungeni. Huu ni Muswada ambao huwasilishwa na Mbunge tofauti na ile miswada inayowasilishwa na Serikali ili kuwa sheria.

Muswada huweza kuwa katika kutunga sheria mpya au kurekebisha zilizopo. Hata Katiba hurekebishwa na sheria inayoanzia kwenye Mswada. Mswada pia huweza kurekebisha sheria mbalimbali kwa wakati mmoja.

Bungeni kuna Kambi Rasmi ya Upinzani inayoundwa na kuongozwa na CHADEMA. Ina Wabunge wa kutosha na wenye hali za kuwakilisha Miswada binafsi kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa. Na wamechaguliwa tangu mwaka 2015.

Ni CHADEMA hao hao ndiyo wanaoshikilia hoja ya uwepo wa Time Huru ya Uchaguzi hapa Tanzania. Hoja hii imeanikwa kama vipaumbele vya sasa vya Katibu Mkuu mpya wa chama hicho John J. Mnyika (Mb). Hoja hii inashikiwa bango mwaka huu; mwaka wa Uchaguzi Mkuu. Kwanini?

Walikuwa wapi tangu mwaka 2015 kujenga hoja hii na haya kuwasilisha Muswada binafsi Bungeni kuhusu suala hilo? Kwanini nafasi hiyo ya Muswada binafsi haikutumika hadi sasa kuitaka Serikali kuwasilisha Muswada huu ya suala hilo kwa Hati ya Dharura?
good question.
 
Katiba mpya sio swala la wapinzani ni swala la watanzania wote wanaojielewa, haiwezekan watu watafune mabilion ya fedha na kusiwe na Katiba mpya watanzania ndo hawajielewi
Nani anayeweka agenda hiyo vinywani mwa watanzania? Bila wapinzani kuongoza unadhani wananchi watainuka tu from nowhere? Jifunze kwa Kenya basi kama hujui hilo

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Viajenda vyao vyepesi tu ni vipi mkuu?
Mambo yanayolenga kuimarisha ubunge wao, wasipoteze nafasi. Vijihoja kama watoto waruhusiwe kusoma wakiwa wajawazito ama wakiwa wananyonyesha!! Hii sio agenda ya kufanyia pupa ama kuweza kutengeneza mazingira mazuri kwa wapinzani kukamata nchi.

Ni agenda nyepesi mno, kwani WATOTO watabaki kuwa WATOTO tu na inahitaji mjadala wa kitaifa kama kweli tumefikia mahali turuhusu mabinti zetu watioto watiwe hovyo kwa sababu hawana hofu ya kufukuzwa shule. Ni ishara kwamba tumeshindwa kuwalinda watoto hawa dhidi ya wanaume katili. Sasa wapinzani wameshikilia hoja dhaifu kama hii kuifanya agenda kuu. Kwa nini wamepoteza dira namna hii?

Hoja ya maridhiano inalenga nini hasa? Mnatafuta kuridhiana kwa lipi? Upinzani unashangaza kweli

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Ndiyo ujue kuwa Twaweza waliweza sana kwenye tafiti zao kuwa ccm ni mambumbumbu

In God we Trust
Mimi sina chama ila asante kwa matusi. Upinza wa namna hii usiohitaji mawazo mbadala ni ujuha na ndio maana unakufa tu. Kwa akili zako weww usiye mbumbumbu unadhani wananchi watainuka tu bila kiongozi? Basi endeleeni kuoigania watoto wapigane miti mashuleni wapeane mimba kwa sababu ndio agenda yenu kuu kwa sasa.

Upinzani usiokuwa na uelekeo. Badala ya kujenga juu ya mafanikio yaliyotangulia mnaanzisha mambo mapya eti kwa kigezo katiba ni ya wananchi wote. Kuna haja gani basi ya kuwa na upunzani? Hovyo kweli

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
This is another garbage!

Hivi nyie watu hamna macho ya kuona wanayofanyiwa wapinzani na wanaharakati???

Pumba kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ni mjinga mkuu. Hujui nafasi ya wapinzani sio? This is Africa, mpaka pale mtakapoamka mtabaki mlivyo. Upinzani sio kula keki na kunywa shampeni. Sio marekani hapa mkuu.

True opposition must pay the price. Kaeni hivyo hivyo mkimsubiri masihi, hakuna chama kilicho madarakani kitakuwa tayari kuachia ngazi kwa staili yenu ya UPENDO.

Nadhani hujaona kinachoendelea Uganda kwa wapinzani, ungelijua ungefuta kauli yako.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Kikatiba, kisheria na kikanuni Muswada binafsi unaruhusiwa kuwasilishwa Bungeni. Huu ni Muswada ambao huwasilishwa na Mbunge tofauti na ile miswada inayowasilishwa na Serikali ili kuwa sheria.

Muswada huweza kuwa katika kutunga sheria mpya au kurekebisha zilizopo. Hata Katiba hurekebishwa na sheria inayoanzia kwenye Mswada. Mswada pia huweza kurekebisha sheria mbalimbali kwa wakati mmoja.

Bungeni kuna Kambi Rasmi ya Upinzani inayoundwa na kuongozwa na CHADEMA. Ina Wabunge wa kutosha na wenye haki za kuwakilisha Miswada binafsi kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa. Na wamechaguliwa tangu mwaka 2015.

Ni CHADEMA hao hao ndiyo wanaoshikilia hoja ya uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi hapa Tanzania. Hoja hii imeanikwa kama vipaumbele vya sasa vya Katibu Mkuu mpya wa chama hicho John J. Mnyika (Mb). Hoja hii inashikiwa bango mwaka huu; mwaka wa Uchaguzi Mkuu. Kwanini?

Walikuwa wapi tangu mwaka 2015 kujenga hoja hii na hata kuwasilisha Muswada binafsi Bungeni kuhusu suala hilo? Kwanini nafasi hiyo ya Muswada binafsi haikutumika hadi sasa kuitaka Serikali kuwasilisha Muswada huu ya suala hilo kwa Hati ya Dharura?
Ungekuwa na asilimia ngapi ya kupita?
What a wastage of time would that be!

Hao wa CCM na wingi wao hawawezi kufanya hivyo labda awe mtu katumwa (Nkamia??)
 
Back
Top Bottom