Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 18,641
- 22,240
Tumekuwa tukitaka nchi iwe na Tume Huru ya Uchaguzi tukidhani ndiyo itakuwa suluhisho la kudhibiti uporaji wa kura, tume huru inaweza ikamtangaza mshindi halali lakini mahakama ikamtengua kwenye kesi ya kupinga ushindi, hivyo ili uwepo utawala wa sheria tunahitaji mahakama huru isiyopewa maelekezo toka nje kama alivyowahi kusema jaji mkuu mstaafu.
Tunapotaka tume huru tutake pia mahakama huru, hata hivyo tukiwa na mahakama huru unaweza ikaidhibiti tume isiyo huru kwa kutengua ushindi uliyotangazwa na tume kinyume cha matakwa ya wananchi.
Tunapotaka tume huru tutake pia mahakama huru, hata hivyo tukiwa na mahakama huru unaweza ikaidhibiti tume isiyo huru kwa kutengua ushindi uliyotangazwa na tume kinyume cha matakwa ya wananchi.