Tume Huru ilikuwa njia ya kuja na kuondoka madarakani kwa amani

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
CCM mliambiwa lakini mkakataa! Si mnaona kinachoendelea hapa nchini kwa sasa? Je, hivi ndivyo mnavyopenda itokee kila baada ya miaka mitano?

Sasa kama uchaguzi ni uadui tutakuja kuendelea kweli?
Yaani kila kona ni mipasuko tu kwa kwenda mbele!

Matamko mengine ni hatari hata kuyasikiliza.

Hilo nalo linahitaji shahada ya uzamifu ili lionekane kwetu? Laiti ingelikuwa amri yangu, kwa ajili ya maslahi mapana ya amani ya taifa hili; uchaguzi huu ungesimama kwanza ili iundwe tume huru ya uchaguzi.

Tume itakayoaminika na pande zote.

Yenye uwakirishi wa makundi yote.
Naam, chombo ambacho kitasimamia haki itakayozaa amani ya watanzania kwa vizazi vingi vijavyo.

Sikilizeni ndugu zangu tume huru si ya wapinzani kama mnavyodhani, bali kwa ajili mustakabari wa taifa hili.

Marehemu mzee Mkapa hakuwa mjinga maana baadaye naye aliliona kama linavyoonekana na wengi sasa.

Watanzania wenzangu watu werevu huwa wanajifunza kwenye makosa ya wenzao, bali wapumbavu ni kwa yao wenyewe! Napo huwa ni kwa maumivu makali.

Mimi naona ipo haja ya kuwepo maridhiano ya kitaifa. Vinginevyo tuendelee mbele huku tukijua hatufiki kule tuendako.

Mungu yabariki makusudio yako Mwenyewe, maana ya wanadamu yalishashindikana kitambo.

Niwatakie Jumatano ijayo iliyo njema.
 
Tanzania tume ya Uchaguzi ni huru

Yule msaliti wa Nchi kutoka ubeligiji ndiye anaichafua tume baada ya Watanzania kumkataa
 
Back
Top Bottom