Tumaini university Iringa kimesajiliwa na nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumaini university Iringa kimesajiliwa na nani?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by chiriku mpole, Jan 24, 2012.

 1. c

  chiriku mpole Member

  #1
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :bange::bange::bange:Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu Tumaini University-Iringa,fani ya BBA(Human resource). Ukweli inasikitisha sana na inaumiza sana tunayotendewa sisi wanafunzi.
  Angalia mifano hii michache.
  1. Kuna wanafunzi 18 kwa idadi wameshindwa kumaliza chuo mwaka jana baada ya kufeli baadhi ya kozi,hivyo inawapaswa kurudia hizo kozi wengi wao ni wa fani ya uhasibu. Kati ya hawa 18, yupo dada mmoja ambaye amehamia kutoka Burundi,alikuwa akisoma taasisi moja huko Burundi ambayo haina hadhi ya university huko Burundi. Pia hakuwa akisoma fani ya uhasibu. Ametuonyesha vyeti vyake vyote vya hicho chuo,ambacho hawatumii english language as a teaching language,wanatumia kifaransa, ndiyo maana alipohamia Tumaini iringa,akadisco kwa kukosa sifa mbalimbali. Haiwezekani mtu atoke diploma ya kifaransa then ajiunge BBA-accounting,hivi hii ni haki? au kwa vile parent wake ana pesa? lengo has lilikuwa ni nini?
  Kana kwamba haitoshi, pamoja na kudisco, watawala wa chuo wamemrudisha tena third-year fani ya BBA-human resource. Huu ni ujinga na pia ni ubaguzi kwa kiwango cha juu. Inakuaje mtu anadisco BBA-Accounting then anapelekwa BBA-human resource?

  Kama ndo hivyo hata wale wanafunzi 18 wa accounting nao waruhusiwe kugraduate maana hapa hakuna ubora wa elimu kwani huyu binti toka Burundi hana sifa bali anatafutiwa cheti tu, ndo maana wamemwamishia BBA-human resource ambako imepangwa apewe marks ili amalize chuo,walimu wa kozi za Human resources ni wachungaji ambao kila mara wamekuwa wakimwita huyu binti ofisini kwa mazungumzo.(mlungula???).

  2.Pia yupo kijana mwingine ambaye amedisco CBE,advanced dipolma-accountancy:msela::msela::msela:. Naye amerusiwa kujoin degree program ya Bsc-accounting and finance, yupo third year right now,.Kama amedisco advance diploma inakuaje ajiunge ana university mwaka wa tatu? jamani kama Tumaini kuna ubora wa elimu, vipi hili linakuaje? basi ni bora hata hawa 18 wanaorudia kozi wapeni marks waondoke, kuna faida gani hawa 18 warudie kozi halafu hawa wa CBE and Burundi wanapewa nafasi. Huu nu ubaguzi kwa kiwango cha juu. Hapana tumechoka hata sisi wanafunzi.
  Kama ni pesa hata sisi tunalipa japo kwashida sana. Kibaya zaidi wanafunzi hawa wanatamba kwamba wazazi wao wanalipa fee in terms of US dollar,kwamba iwe isiwe watapata vyeti vyao. Pia wamekuwa wakiwadharau hata wakuu wa idara na kuheshimu watawala wakuu. Hii maana yake nini? ina maana watapewa marks za bure na wakubwa wa chuo hiki? Heshima ya walimu wa chuo hiki iko wapi, kama mtu hana sifa stil anapewa sifa bandia ya kumwezesha kuingia class? Hii inamanisha hata wakifeli stil wakubwa wa chuo hiki watamake sure that wanawapa marks za kupika ili wapata vyeti vyao.

  Jamani hayo mambo ni dharau kubwa sana kwa sisi wanafunzi tuliojiunga na hiki chuo tukiamini tutapata elimu bora, tunaomba haki itendeke kwa watu wote, sifa za kujiunga na chuo ziheshimiwe, walimu waheshimiwe, Mungu naye aheshimiwa na kuogopwa!
  Hivi hiki chuo kimesajiliwa na nani? TCU? NACTE? au nani?
  Ninaomba Jamii forum next time waniruhusi niweke attachments zote za hawa wanafunzi kwani ushahidi upo, pia watanzania wenzagu kama una ndugu yako BBA iringa make follo-up on this.

  Najuta kujiunga na hiki chuo.
   
 2. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 868
  Trophy Points: 280
  Degree ya tumain ni sawa na form 4 ya ilboru.
   
 3. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2012
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  hah ah aha ha ha h ah ah Ni BBA peke yao? mbona nasikia kuna kiidara cha wakulima wanoko hapo? Duh chichiem
   
 4. m

  moshingi JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa Tumaini Iringa mambo ni mepesi kiasi hicho basi pasingekuwepo hao 18 waliofeli;
  Ila mwandishi hajatuambia kama yeye ni miongoni mwa hao 18...na kwamba anatamani asaidiwe
  kama binti kutoka Rwanda!? Kaza buti baba kitabu siyo mchezo usisubiri kubebwa...
  Degree za chupi ni jambo la kawaida pale mlimani, sasa limeanza kuingia Tumaini Iringa,
  hayo ni maajabu...Natarajia malalamiko yako yamewafikia walengwa, ninahakika hupitapita humu...
  Watayashughulikia...ni vizuri ulivyopiga kelele kufukuza wezi ili IUCO ibaki salama
   
 5. mbalisana

  mbalisana Member

  #5
  Jan 28, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maksi za chupi zinaweza patikana kwa wapumbavu wachache lkn sio degree, na hii mahali popote sio Mlimani tafadhali, au hujui degree haitolewi na mtu mmoja, kuna lecturers wanawake na wanaume. Mlimani ni chuo Sio Altenative to life kama hivyo vyenu. ndo maana wanaoenda pale ni vipanga kwa asilimia kubwa. nani alidisco tumaini akapata nafasi mlimani?au akapata mlimani na tumaini akaenda tumaini. Mlimani ni chuo vingine bado sana labda 2050.
   
 6. m

  moshingi JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha unafiki!!
  Danganya wale ambao hawajawahi soma UDSM...Nimesoma miaka 3 mfululizo ninapajua vema
  Ni kweli wapo vipanga, lakini ni kweli pia kuwa yapo madudu mengi sana hapo Mlimani
  Hii ni taswira ya Tanzania tuliyonayo kila sekta hivi sasa, viongozi wengi waliopo madarakani
  walipitia hapo UDSM, wanayoyafanya huko yanaangaza waliyojifunza toka kwa
  Wahadhiri wao. Rushwa, Uzembe, Ubadhirifu, wizi, udini/ukabila/ undugunaizesheni, na mengine mengi
  yanaonekana waziwazi serikalini, walijifunza wapi kama siyo Mlimani??
  Ku-disco chuo kimoja na kufaulu kingine ni mchango wa mambo anuai, kama vile ukaribu wa mwalimu na mwanafunzi,
  mwanafunzi mwenyewe wakati huo alikuwa ana matatizo ya kisaikolojia/kifamilia, mara nyingi watu hutumia vema second chance...
  Wahadhiri wengi wa UDSM hawana muda wa kuwa karibu na mwanafunzi, hasa pale sheria wako bize mahakamani kutetea
  kesi za wateja wao kwao kufundisha ni "subsidiary" ni vipi wataweza kugundua shida za mwanafunzi na kumsaidia???
   
Loading...