Tumaini langu la mwisho lipo humu ninaomba mnisaidie

Naja naja

Naja naja

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Messages
800
Points
1,000
Naja naja

Naja naja

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2016
800 1,000
Nimekwama kuendelea na chuo kutokana na ukosefu wa ada .

Sasa hii hali sitaki tena ijirudie hata nikirudi tena chuoni ,hivyo suluhisho pekee nililoliona ni kufanya biashara.

Biashara ambazo zipo kichwani kwangu ni mbili ambazo ni;

1)Biashara ya grocery ambayo itajumuisha chipsi na nyama choma.

2)Vifaa vya simu,urembo wa kike ikiwemo saa na hereni, pamoja na kuuza vocha za rejareja .

Mtaji wa biashara ya kwanza kidogo ni mkubwa japo niliomba vifaa used ambavyo watu watakuwa hawavitumii wanisaidie nianzie navyo biashara.

Miongoni mwa hivyo vifaa ni pamoja na meza,viti,friji, pamoja na kikabati cha chipsi.

Hii ilionekana ni ngumu hivyo nika opt biashara ya pili ambayo ni vifaa vya simu,vocha na urembo ambapo mtaji wake kwa kuanzia ni laki tatu na nusu ambapo nilipanga kuanza na maboksi matano ya protector kila boksi moja linakaa protectors kumi hivyo maboksi matano inamaana yatatoa protectors hamsini na bei ya boksi moja ni shilingi elfu 7.

Mbali na protector, nilipanga nianze na chaja kumi,usb kumi, makava hamsini ya urembo na makava 20 autofocus.

Mbali na vifaa vya simu nilipanga kuanza na urembo pamoja na vocha.

Kibanda cha kuuzia hivyo vitu kipo nilipewa ofa tangu zamani na rafiki yangu kwa kuwa yeye ana vibanda vitatu kimoja kipo tu hakitumii.

Sina tegemeo jingine lolote zaidi yenu ,ninaomba mnisaidie kunichangia mtaji nifanye biashara nipate ada nirudi chuo pia kupitia biashara hii hii inisaidie tena kulipa ada kwa mihula inayofuatia .

Account yangu ya crdb ni hii 0152557370900 ninaomba unichangie chochote ulichobarikiwa.
 
October man

October man

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2017
Messages
1,688
Points
2,000
October man

October man

JF-Expert Member
Joined Nov 23, 2017
1,688 2,000
Unajua nyinyi vijana mnachukulia mambo kirahisi sana. Kuna mmoja alikuja na business idea mtaji 180,000. Nikamwambia nitakupa hio 180,000 ila niwe shareholder nusu kwa nusu( wala nisingepoteza muda na biashara yake). Unajua alisema? Hawezi kuwa share na mtu biashara ndogo namna hio, kasahau hana hio 180,000 mpaka kaja kuomba mtandaoni. Hana tofauti na wewe unaeona kuuza maji ni kunishusha huku unaomba wauza maji wakuchangie.
I admit it
 
Desire Dizaya

Desire Dizaya

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2015
Messages
6,338
Points
2,000
Desire Dizaya

Desire Dizaya

JF-Expert Member
Joined Feb 16, 2015
6,338 2,000
Kijana mwenzangu naomba nkishauri kitu.jitahidi kutafuta biashara zinazoanzia na mtaji mdogo zaidi.unaweza hata kuuza matunda mchanganyiko kwa laki moja.

Wale mwenzio waliosamama kwenye Mesa stendi za magari unakuta kamenya nanasi kalikata vipandw kama kumi.tikiti,machungwa.wana maisha wanaendesha.
Ni maisha yako hayo.usione aibu.
Tafuta Yale mahitaji ambayo yatakua ya lazima na yanatoka kwa haraka ili ukisanye ada kwa haraka.we unadhani phone covers ni hitaji la kila siku kama chakula?
Biashara ya chips bado utahitajika kitambulisho cha machinga,na itachukua mda kuvuta wateja waje kwako..
 
Anakwambia anaangalia biashara atayofanya itamfikisha wapi baadae, so awezi fanya biashara kama hizo mfano kuuza maji nk....
 
Desire Dizaya

Desire Dizaya

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2015
Messages
6,338
Points
2,000
Desire Dizaya

Desire Dizaya

JF-Expert Member
Joined Feb 16, 2015
6,338 2,000
Kwa hiyo anataka iwe ya moja kwa moja?
Huu nliotaja mie ni mwanzo tu.akifanikiwa kukuza mtaji anahamia huko juu.
Anakwambia anaangalia biashara atayofanya itamfikisha wapi baadae, so awezi fanya biashara kama hizo mfano kuuza maji nk....
 
Forum statistics

Threads 1,313,876
Members 504,678
Posts 31,807,014
Top