Tumaini la kupata dawa ya UKIMWI laongezeka baada ya 4% ya watu kugundulika kuwa na kinga ya asili nchini DRC

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Ugunduzi wa kundi kubwa la watu ambao miili yao inaweza kupambana na kudhibiti Virusi vya UKIMWI nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo unaleta matumaini ya kupata tiba ya virusi hivyo.

Utafiti umebaini kuwa asilimia 4 ya watu waliokuwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI nchini humo wameweza kukabiliana na kuvishinda virusi hivyo, wakati kwa kawaida ni chini ya asilimia 1 ya watu ndio wenye uwezo huo.

Watafiti sasa wana matumaini makubwa kuwa baada ya utafiti wao wanaweza kutengeneza chanjo au tiba mpya itakayoweza kukabiliana na virusi hivyo.

Matokeo ya utafiti huo uliofanywa na wanasayansi kwa pamoja kutoka vyuo vya John Hopkins, Kampuni ya Dawa ya Abbott, Chuo Kikuu cha Kiprotestanti cha Kongo na vyuo vingine, umechapishwa katika jarida la kitabibu la eBioMedicine umehusisha sampuli za watu waliokuwa wakiishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI tangu mwaka 1987 hadi mwaka 2019.

Dkt. Mary Rodgers, Kiongozi wa Programu ya Utafiti wa Magonjwa ya Virusi kutoka Kampuni ya Dawa ya Abbott amesema kundi hilo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni kubwa zaidi, ikihusisha asilimia 2.7 hadi 4.3 ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI, huku akitaja pia asilimia 1 ya watu wote wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI nchini Cameroon wameweza kupambana na kuvishinda virusi hivyo bila msaada wa dawa za kufubaza makali ya UKIMWI.

Watafiti hao wanasema hawafahamu ni kwa jinsi gani watu waliofanikiwa kupambana na kuvishinda virusi hivyo nchini DRC walivyoweza kufanya hivyo, lakini wanasema kuwa walifanikiwa kuwa na kiwango kidogo cha virusi katika miili yao hivyo kuweza kupambana navyo kikamilifu.

Hata hivyo wamesema kuna haja ya kuendelea kufanya utafiti zaidi, kwani kuna utafiti unaoonesha kuwa kinga za watu waliofanikiwa kuvishinda virusi hivyo huishiwa nguvu baadaye na kuvifanya virusi hivyo kurejea.

Tangu kugundulika kwa virusi hivyo katika miaka ya 1980, watu milioni 76 wamekwisha ambukizwa huku wengine milioni 38 wakiishi na virusi hivyo. Takriban watu milioni 37 wamefariki kutokana na virusi hivyo tangu kugunduliwa kwake.

Chanzo: BBC
 
Aiseee, endeleeni kuvaa kinga kwenye mechi zenu😁 hii kitu ni hatari sanaaaaa mpaka ije igundulike dawa si leo ndugu zangu😁😁😁
 
Back
Top Bottom