Wakuu kher?
Katika maisha kuna vitu vinasikitisha sana tena sana, Waajiri wengi wamekosa utu hasa linapokuja suala la kutimiza wajibui wao kama waajiri hapa nazungumzia malipo na stahiki za mfanyakazi.
Tatizo kubwa waajiri wanakuwa hawajali maslahi ya wafanyakazi wao na wakikaa vibaya tu wanadhulimiwa.Hali hii tunaiona mpaka katika serikali yetu watu wanadai haki yao lakini mwisho wa siku wanaambulia kejeli na vitisho.
Naamini wengi wenu mtakuwa mnaifahamu TUMAINI HOSPITALI ambayo ipo Upanga opposite na makao ya jeshi.
Kwa lugha rahisi kabisa naweza kusema hii hospitali ni jipu.
Kumekuwepo na malalamiko ya wafanyakazi kutokulipwa mishahara yao kwa Muda sasa.mfano halisi ni kwamba mpaka sasa wafanyakazi wote hasa wale waajiriwa wanadai mishara ya miezi miwili na nusu.Hiyo nusu ilikuja baada ya kulipwa nusu ya mshahara wa mwezi mmoja.
Viongozi wa hospitali hii wamekuwa wababaishaji kupita maelezo yaani wanaweza wasiwape wafanyakazi mishahara hata ya miezi mitatu mfululizo halafu wakija kulipa wanalipa nusu au wanawapa pesa kidogo ili wapunguze njaa HII SIO HAKI.
Mnyetishaji wa taarifa anasema mwaka jana wafanyakazi wa hospital karibu wote walidhumiliwa pesa zao za overtime ambapo yeye mtoa taarifa alikuwa anadai karibu laki sita 600000 hiyo ni overtime ya miezi kadhaa
"Tulipokea taarifa tu kwamba uongozi hautalipa overtime zetu bila kuelezwa sababu ya msingi"Alisema mtoa taarifa
Katika hali ya kushangaza viongozi wa juu wa hospitali hii wamekuwa wababe wa kupindukia linapokuja suala la maslahi ya wafanyakazi
"Viongozi wetu hawatoi taarifa yeyote kuhusu mishahara kuchelewa"Alisema mfanyakazi mmoja
Kuna baadhi ya wafanya kazi waliacha kazi kwa taratibu zote na wakawa wanaidai hospitali mishahara ya miezi miwili lakini cha ajabu Uongozi uligoma kuwalipa watu hao
sidhani kama unyanyasaji huu unakubalika vyombo husika vinavyotetea maslahi ya wafanyakazi inabidi viongeze nguvu kukemea huuu uvunjifu wa haki za wafanya kazi.