Elections 2010 Tuma neno "hapana" kwenda 15016 uone ccm ilivyokuibia bila idhini yako

bwegebwege

JF-Expert Member
Jul 30, 2010
1,068
184
wana jf na watanzania wenzangu!!

tuma ujumbe kwa mtandao wowote ule wenye neno "hapana" kwenda kwenye namba 15016 kuna jibu linalokuja na linaonyesha kwamba watanzania tumeliwa hela nyingi sana kwa ujumbe unaoonyesha kwamba ccm imekuwa na mpango maalum wa kuichangia ishinde, tena bila idhini ya watanzania!!!

tunza ujumbe huo mara utakapoupata, ni silaha ya kuing'oa ccm na kampeni zao chafu!!
 
Nimetuma, nimejitoa na nimetumia rafiki zangu wajitoe! Kuna haja ya kuishtaki mitandao hii kwa wizi huu wa mchana!
 
Halafu hii kitu iko kwenye mitandao ya VodaCom na Tigo. Bado sijajua mitandao mingine! Dkt Slaa awalipue hawa jamaa kwa ufisadi huu!
 
du kweli bwana nimepata ujumbe huo inamana wamekuwa wanakata pesa kwanini watulazimishe kuchangia bila idhini zetu wahy? sheria ifate mkondo wake jamani akuna wanasheria hapa jamni
 
Du!!!!
AISEE namimi nilikuwa nachangia bila kujua!
Labda na Slaa amechangia
 
Jamani kweni kunatokea nini? Hebu tujulisheni wengine tusio na simu kwa sasa tujuwe nini kinaendelea ili tujitowe mapema.

Naomba mtuwekee maelezo yote ili tuwajulishe na wengine nini kimefanyika na ujumbe gani unapata.

Asanteni.
 
Hivi hii habari yenu ina uhusiano na hii hapa chini?

Siku zote nilikuwa nikijiuliza, hivi hawa wenye makampuni ya simu wanapata vipi faida kwa mtindo wa shilingi moja kwa sekunde katika kipindi hiki ambapo karibu kila mtu ana simu (mijini) na cha zaidi Mchina anatengeneza simu zenye line mbili? Na je, kwa mwendo wa vocha za 300, 500, na nipige tafu faida itapatikana wapi?

Baada ya kuzagaa kwa taarifa za ujumbe unaohusu "kuichangia CCM kwa lazima", sasa naweza kujua kwa nini tunadanganywa gharama za kupiga simu zimeshuka. Kuna uwezekano mkubwa kwamba CCM wamewalipa makampuni ya simu pesa ya kutosha kabisa ili makampuni yashushe bei na kwa hiyo, kimya-kimya watumiaji wa mitandao wanakatwa salio bila kujua.

Inakuwaje CCM wanatapatapa namna hii jamani? Siri zote tunazipata kutoka huko huko kwenu CCM. Fanyeni ghiliba zote. Tutazinyaka. Hata mfanyie kuzimu. Tutazinyaka.

Kila nafsi itaonja mauti jamani. Tulieni.
 
Hahahaha Lol!

JF you should think critically. CCM wamechukua fedha ya campaign hazina. Kilichofanyika hapa ni kuongea na hii mitandao ya kifisadi kuweka data kwa simu zote, kuwa zimewachangia hela nyingi sana ndiyo maana wana matumizi ya kufa mtu. Ila ushauri wangu ni mmoja, kwa hili CCM wamejitia kitanzi, Kama wapinzani watakuwa makini wanaweza kuifilisi CCM kwa kuwataka watu wote wadai kurudishiwa hela zao ziliko katwa bila ridhaa yao.

Cha kufanya kwa sasa ni kuhamasisha wananchi wote watume "Hapana" kwenda 15016 ili watumiwe hii message iwe kama stakabadhi yao ya makato ambayo hawakuyaidhinisha kabla majambazi wa IT wa mitandao hii hawajaamriwa kufuta program hiyo. Halafu washitaki mitandao hii kwa ku-disclose information zao kwa third party. Japo Tanzania hakuna haki ila ni bora kuchukua hatua hizi ili CCM waeleze hela za campaign wamezitoa wapi?, siyo tu kutumia mitandao ya simu inayomilikiwa na mafisadi kama uthibitisho.
 
Pumbaf wananiambia "asante kwa ukumbe wako, utatolewa kwenye huduma hii ya changia ushinde na CCM" Nawatafuta customer care wanieleze hili suala lina kuwaje!
 
Hata Zain nimewatumia message hii, wamenikubalia kunitoa katika huduma ya kuchangia CCM
 
Duh! Hii kali,kwanza namshukuru aliyetoa hiyo taarifa vinginevyo tusingejua uhuni unaofanywa na ccm pamoja na makampuni ya simu.

Cha kufanya ni kulipigia kelele,wananchi wengi wajue kuwa mafisadi hawachukui kodi zetu tu bali hata ile hela ndogo tunayobaki nayo mifukoni.Pia ni kuwashitaki wahusika wote,ikibidi kuyagomea makampuni ya simu husika.
 
wana jf na watanzania wenzangu!!

tuma ujumbe kwa mtandao wowote ule wenye neno "hapana" kwenda kwenye namba 15016 kuna jibu linalokuja na linaonyesha kwamba watanzania tumeliwa hela nyingi sana kwa ujumbe unaoonyesha kwamba ccm imekuwa na mpango maalum wa kuichangia ishinde, tena bila idhini ya watanzania!!!

tunza ujumbe huo mara utakapoupata, ni silaha ya kuing'oa ccm na kampeni zao chafu!!
Kama wako katika kampeni wanadiriki kuwaibia wananchi bila huruma . je wakishika madaraka itakuwaje? mtanzania think about it.
 
kweli, hawa ni mafisadi, hivi hii push mobile ni ya nani cause hawa ndio wanalisimamia hili zoezi la kuchangia
 
Jamani watanzania tukimbilie wapi? Tunaujumiwa kila kona. Jaman mi nashindwa kuelewa la kufanya. Watanzania jiondoe katika kuchangia ccm,tuma 'HAPANA' kwenda 15016 .Ccm ni chama cha matapeli jaman mwambie Slaa akiingie ikulu aifilisi Ccm,afute mitandao yote ya simu ili tuanze upya. Ufisadi hautakubalika.
 
Duh! Hii kali,kwanza namshukuru aliyetoa hiyo taarifa vinginevyo tusingejua uhuni unaofanywa na ccm pamoja na makampuni ya simu.

Cha kufanya ni kulipigia kelele,wananchi wengi wajue kuwa mafisadi hawachukui kodi zetu tu bali hata ile hela ndogo tunayobaki nayo mifukoni.Pia ni kuwashitaki wahusika wote,ikibidi kuyagomea makampuni ya simu husika.
Hii kashfa inatakiwa iwekwe wazi mpaka katika vyombo vya habari ili kila Mtanzania ajue. Nimejaribu kuwatumia waliopo sms waliopo kwenye contacts wangu na e mail, lakini kuna haja ya umma mzima kufahamu hili.
 
ni wahuni,hata msg zenyewe zinz typing errors,mfano msg inasomeka ukumbe badala ya ujumbe
 
Jamani watanzania tukimbilie wapi? Tunaujumiwa kila kona. Jaman mi nashindwa kuelewa la kufanya. Watanzania jiondoe katika kuchangia ccm,tuma 'HAPANA' kwenda 15016 .Ccm ni chama cha matapeli jaman mwambie Slaa akiingie ikulu aifilisi Ccm,afute mitandao yote ya simu ili tuanze upya. Ufisadi hautakubalika.
Kimbilio letu ni tarehe 31-10-2010...baada ya kuwa garagaza tunafungua kesi ya madai....
 
Leo asubuhi rafiki yangu alinunua voucherya tigo ya 500 aliongea dakika 5 tu akawa anashanga imekuwaje na aliempigia alikuwa natumia tigo pia wakati tigo kwenda tigo senti 50 baada ya dakika ya kwanza sasa nimegudua kwanini inawezekana CCM walichukua kiasi ya pesa...CCM hukumu yenu 31/10/2010
 
Back
Top Bottom