Tuliyekukabidhi ngao, mkuki na katiba shamba la bibi tafadhali jitokeze useme chochote nchi ina hofu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Ni ukweli ulio wazi kuwa Kiuchumi Tanzania kwa hii miezi kadhaa haisogei na yawezekana hata Uchumi nao sasa ukawa ' unadorora ' tu kwa mambo yafuatayo:
  • Wananchi wana hofu kubwa
  • Hawawaamini tena wale walioteuliwa na ambao sifa zao zinaonekana haziendani na Vyeo
  • Matukio ya Ujangili, Mauaji na Utekaji yamewaogofya wengi
  • Watanzania sasa wamewekeza kushinda mitandaoni kuliko mashambani, baharini / ziwani au kufanya Kazi za Kiutendaji za Maofisini
  • Vyombo vya Habari vimegeuka kuwa daraja kuu la kuzidisha hofu kubwa kwa Wananchi
  • Wenye dhamana ya kuhakikisha hofu hii inatoweka ndiyo kwanza wengine wanasajili Wachezaji wao kwa Timu yao iliyopanda Ligi Kuu huku wengine wao badala ya kuzuia, kukamata wahalifu wote sasa na Wao wamegeuka na kutuomba sisi Raia tusio na mafunzo yoyote zaidi tu ya kujua kuvaa Condoms kujikinga na UKIMWI kuwa tuwasaidie kuwafichua hao Wahalifu
  • Viongozi wa Dini nao badala ya kutupunguzia ' Presha ' kwa angalau kutupa neno la Kiroho na wao sasa ndiyo kwanza wanahubiri ' Kimajungu ' na Kiuchochezi ' kama siyo ' Kichuki ' kitu ambacho ni hatari sana.
Ndiyo nasema kuwa Wewe tuliyekukabidhi ile Ngao, Mkuki na Katiba Uwanja wa Uhuru ( Shamba la Bibi ) tafadhali jitokeze ili uweze kutusaidia katika hili kwani yawezekana kauli yako Wewe ikatusaidia sisi wenye hofu kutulia na kuamini kuwa hakuna lolote na tuko salama kuliko kunyamaza kwani sidhani kama kwa aina hii ya hofu ambayo sasa kila kukicha inazidi kuongezeka hapa nchini Watanzania wataweza kujikita vizuri katika Shughuli za Kiuchumi ambazo kimsingi na Wewe ndiyo unawategemea ili waweze kulipa Kodi kisha uendee kutuletea maendeleo mengine na zingine za Kujikimu Wewe na Wasaidizi wako.

Say something Brother!
 
Back
Top Bottom