Tuliyaishi haya zamani yetu, sasa yamebaki kumbukumbu ya kuvutia kama si kuchekesha

Enzi za uchaguzi wa chama kimoja,wahenga mnaikumbuka hii
Screenshot_20220110-030052.jpg
 
Wote waliaga dunia 2 January 2022. Mmoja nje alikua Mwafrika lakini ndani yake alihisi ni mzungu ilhali Mwengine alikua Mzungu nje lakini ndani yake alihisi kuwa Mwafrika halisi. Wengi wamjua Charles Njonjo. Uyo mwengine ni Dr. Richard Leakey alikua mwanaharakati wa mazingira na wildlife conservationist. Dr Leakey alizaliwa Kenya enzi za ukoloni na hata kujua mila za wakenya.
Screenshot_20220110-035044.jpg
 
Tujikumbushe hadithi ya KALUME-KENGE

Kalume-Kenge alikataa kwenda shule, baba yake akamwambia mbwa: je, mbwa, wataka kumwuma Kalume-Kenge? Hataki kwenda shule.
Mbwa akakataa.

Baba yake akasema kwa fimbo: je, fimbo, hutaki kumpiga mbwa? Yeye hataki kumwuma Kalume-Kenge, naye hataki kwenda shule.
Fimbo ikakataa.

Baba kaukamata moto, akasema: je, moto, wataka kuichoma fimbo? Kwa maana haitaki kumpiga mbwa, naye hataki kumwuma Kalume-Kenge, naye hataki kwenda shule.
Moto ulikataa.

Baba akasema kwa maji: je, maji, wataka kuzima moto?
Moto hautaki kuchoma fimbo,
Nayo haitaki kumpiga mbwa,
Naye hataki kumwuma Kalume-kenge.
Naye hataki kwenda shule.
Maji yalikataa

Baba kamwendea mbuzi: je, mbuzi, hutaki kunywa maji?
Kwa sababu hayataki kuzima moto.
Nao hautaki kuichoma fimbo,
Nayo haitaki kumpiga mbwa,
Naye hataki kumwuma Kalume-Kenge.
Naye hataki kwenda shule.
Hata mbuzi alikataa.

Baba akamwendea sultani.
Je, sultani. Hutaki kumchinja mbuzi?
Amekataa kunywa maji,
Nayo hayataki kuzima moto,
Nao hautaki kuichoma fimbo,
Nayo haitaki kumpiga mbwa,
Naye hataki kumwuma Kalume-Kenge,
Naye hataki kwenda shule.

Sultani akakubali.
Akamchinja mbuzi
Naye akanywa maji,
Nayo yakazima moto,
Nao ukaichoma fimbo
Nayo ikampiga mbwa,
Naye akamwuma Kalume-Kenge,
Naye Kalume-Kenge akaenda shule.
Screenshot_20220110-082432.jpg
 
1. Kupakwa dawa ya vidonda iitwayo GV
2. Kung'olewa jino kwa uzi
3. Ubwabwa kupikwa jumapili tu
4. Kidonda kuwekwa unga wa 'rangi mbili' a.k.a tetracycline
5. Kupamba kadi na pamba sebuleni
6. Ukumbi wa sherehe kupambwa kwa toilet paper
7. Kunyolewa kwa mkasi
8. Kufunga pesa kwenye leso au pindo la kanga
9. Wavulana kuvaa nguo ya ndani aina moja nchi nzima (VIP), usiombe ikakatika ukakuta imebana kifua.
10. Ku-rewind kanda kwa peni
11. Nchi nzima Kuangalia Movie ya Commando John, Double Impact, Rambo na Bruce Lee..
12. Watoto Wa Mtaa Mzima Kufahamiana sababu ya kucheza Wote Jioni Kombolela na Kibaba..
13. Kuunguzana na tunda ya Ubuyu baada ya kulisugua chini
14. Kukata ndala, eti ni kifutio
15. Kunyolewa msalaba shuleni kisa nywele ndefu
16. Kuweka Vibox box kwenye Shati la shule Mgongoni..
17. Kuweka Shati la Shule "Blue" eti liwe maridadi.
18. Ubitozi Ulikuwa ni Kusimamisha Kola Ya Shati.
19. Ukiandika Barua kwa Umpendae lazima uchore moyo na Mkuki na lazima upulizie Pafyumu ya "YU".

20. Hata kama Mlikuwa mmegombana January lakini Mtu anakwambia ngoja shule ikifungwa

Kama kuna mengine ongezea
we kweli mhenga mwenzangu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom