Cryptographer
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 376
- 730
Unazikumbuka kucheza gololi kwa watoto wa kiume? Kipindi hicho mtoto akiwa na gololi nyingi alikuwa kama tajiri fulani hivi. Nakumbuka zilikuwa zinauzwa madukani lakini kupata fedha ya kununulia ilikuwa ni issue kubwa. Namna pekee ya kuzipata ni kwa kucheza ili ''uwale'' wenzako.
Dah hapo bi mkubwa anaenjoy kinoma.
Makabati ya video kufungwa na funguo
- Kuvaa Mashati yaliyochorwa "Eagle" nyuma....
- Sherehe za harusi kufanyika kwenye majumba ya watu; halafu baadae zikawa kwenye kumbi za mashule (Kama Azania)
Banko
Hahaha...Kuna mchezo ulikuwa unaitwa "tobo dunda" unachezwa kama mpira wa miguu ila hakuna magoli halafu unachaguliwa mti mmoja wa kukimbia kushika ikitokea mpira umepita katikati ya miguu yako "tobo", inapotokea unapigwa ngumi pona yako ni mbio zako kwenda kushika mti. Ulikuwa mchezo wa kishujaa sana wakati ule
Kweli kabisaKusoma shule za kayumba na watoto wa Mkurugenzi, Afisa Elimu, DC, RC, Waziri etc ilikuwa ni kawaida.
Siku hizi, thubutuu!!!!!!!
Hapa ndio palipoanzia methali ya "ukiona mwenzio ananyolewa wewe kichwa kitie maji" nini?
Kwenye mchakamchaka tulikuwa tunaimba, ''jua lile literemke mama", lakini halikuteremka, kwa joto la sasa hivi, yawezekana ndo limeteremka. Labda sasa tuimbe '' jua lile lipande juu mama'', halafu tusubiri kidogo, pengine litapanda na kupunguza joto.1. Kupakwa dawa ya vidonda iitwayo GV
2. Kung'olewa jino kwa uzi
3. Ubwabwa kupikwa jumapili tu
4. Kidonda kuwekwa unga wa 'rangi mbili' a.k.a tetracycline
5. Kupamba kadi na pamba sebuleni
6. Ukumbi wa sherehe kupambwa kwa toilet paper
7. Kunyolewa kwa mkasi
8. Kufunga pesa kwenye leso au pindo la kanga
9. Wavulana kuvaa nguo ya ndani aina moja nchi nzima (VIP), usiombe ikakatika ukakuta imebana kifua.
10. Ku rewind kanda kwa peni
11. Nchi nzima Kuangalia Movie ya Commando John, Double Impact, Rambo na Bruce Lee..
12. Watoto Wa Mtaa Mzima Kufahamiana sababu ya kucheza Wote Jioni Kombolela na Kibaba..
13. Kuunguzana na tunda ya Ubuyu baada ya kulisugua chini
14. Kukata ndala, eti ni kifutio
15. Kunyolewa msalaba shuleni kisa nywele ndefu
16. Kuweka Vibox box kwenye Shati la shule Mgongoni..
17. Kuweka Shati la Shule "Blue" eti liwe maridadi.
18. Ubitozi Ulikuwa ni Kusimamisha Kola Ya Shati.
19. Ukiandika Barua kwa Umpendae lazima uchore moyo na Mkuki na lazima upulizie Pafyumu ya "YU".
20. Hata kama Mlikuwa mmegombana January lakini Mtu anakwambia ngoja shule ikifungwa
Kama kuna mengine ongezea