Tuliwambia hii Nchi bila wapinzani kuitetea ni kazi bure. Mmeona wenyewe. Msilie sasa kaeni kwa kutulia.

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
33,905
44,011
Ni miaka mingi sana wapinzani tumekuwa tukipigania maslahi ya taifa kwa udi na uvumba. Kwa miaka yote tumekuwa na matokeo chanya ikiwemo kuzipinga bajeti nyonyaji kwa wananchi. Ilifika mahali bajeti pendekezwa za Mbadala kutoka kambi ya upinzani Bungeni zinachanwachanwa kwenye makamera ili kutudhalilisha. Huku vitendo hivyo vya aibu vikiungwa mkono na wanaccm na wafuasi wa mfumo nyonyaji, wanufaika wa uasi

Haikuishia hapo. kupiga kelele kwetu ili kupata mifumo sawia itakayoleta viongozi waadilifu ktk chaguzi za viongozi wa umma ukanza kuingia shubiri. Tukawa tunawindwa kama dubu. Kwa riasi na mabomu. Hatimaye wakafanikiwa kwa mbwembwe kutuengua kwenye level zote za utawala kuanzia serikali za mitaa, madiwani wa kata na wahunge majimboni. Kazi hii ilifanikiwa kwa ufanisi mkubwa ulioungwa mkono na wasaliti wa taifa hili.

Baada ya hapo matokeo yake tumepata Serikali ya CCM pure. Wamewageuka manyumbu yao.

Kwa hili wapinzani tuko clean. Hatuna Doa. Sisi tozo tutalipa.

Wafuatao nadhani hawamo kwenye orodha ya kulipa tozo na makodi kodi

1. UVCCM
2. Umoja wa wanawake ccm
3. Baraza la wazee ccm
4. Wanaccm wote
5. Polisi wote waliokuwa wakizuia haki kutendeka
5. Mahakama na waandamizi wote waliochangia dhulma
6. Watumishi wote wa tume ya uchaguzi

7. Mataga woote.

Msilielie wala msitulilie. Tuliwaonya. Kazi iendelee tulipe kodi na tozo tujenge nchi.

Mama anaupiga mwingi sana😅😅😅
 
Majitu ya ccm hawajui waanzie wapi..
Wao wakisikia katiba mpya ndio wanapanua midomo kupinga..
Lakini hili la maumivu ya bajeti wanaona nyota tu..
Ngoja dawa iwaingie..
Mama anaupiga sanaaa.
Tukizungumzia tume huru ya uchaguzi na katiba mpya hii ndio maana yake. Tunataka Tume na uchaguzi huru utupatie viongozi waadilifu na wenye uwezo utu na uzalendo kwa Taifa sio hawa waliojazwa na Jiwe wachumia tumbo.
 
Lakini ili wapinzani wafanikiwe ilitakiwa wawe wanaingilia kati masuala kama haya ya miamala huku wakiambatanisha na hoja za katiba mpya.

Lkn wakikaa kimya wanaonesha wazi kabisa kwamba wanapambania Mambo yanayolenga maslahi yao ya kisiasa moja kwa moja.
 
Issue ya miamala ilikuwq ngumu kueleweka pale Bungeni maana Mwigulu alidai itakatwa Tsh 100 kila muamala matokeo yake kumbe Tsh 100 inategemea unatuma Tsh ngap!
 
Lakini ili wapinzani wafanikiwe ilitakiwa wawe wanaingilia kati masuala kama haya ya miamala huku wakiambatanisha na hoja za katiba mpya.

Lkn wakikaa kimya wanaonesha wazi kabisa kwamba wanapambania Mambo yanayolenga maslahi yao ya kisiasa moja kwa moja.
Wamekuwa wakiingilia mambo makubwa zaidi ya haya. After all kodi ni kwa ajili ya maendeleo yantaifa.

Wakisema jamani tuandamane kwa ajili ya kupigania haki kuna watu wanabeza wanasema We Mbowe kaandamane na familia yako🤣🤣
 
Ni mtu mjinga tu anayedhani MAENDELEO hupatikana kirahisi na kwa kupita NJIA ZA MKATO ?!!!!

MAENDELEO binafsi yanapatikana kwa kufunga mkanda......

MAENDELEO ya nchi hupatikana kwa wananchi kuifunga mikanda.....

Dr.Mwigulu yuko sahihi....
Bunge liko sahihi.....
 
🤣🤣🤣kweli kabisa. Naona wanalialia
 
Ni mtu mjinga tu anayedhani MAENDELEO hupatikana kirahisi na kwa kupita NJIA ZA MKATO ?!!!!

MAENDELEO binafsi yanapatikana kwa kufunga mkanda......

MAENDELEO ya nchi hupatikana kwa wananchi kuifunga mikanda.....

Dr.Mwigulu yuko sahihi....
Bunge liko sahihi.....
Nchi itajengwa na wenye moyo. Waongeze na vyanzo vingine vya tozo tutalipa tu
 
Acha dawa iwaingie kabisa
waliwaona akina
John Heche
G Lema
P msigwa
Pendo Pendeza
JJ Mnyika

kuwa hawana akili acha waipate fresh kabisa tena na bado iongezwe zaidi na zaidi in Kigogo's Voice wakija kushtuka kwisha habari kabisa
 
Haya yote ni ushabiki na ujinga walionao baadhi ya watz,tunalipia huo ujinga, mpaka utakapo tutoka
 
Back
Top Bottom