Tulivyotapeliwa msibani, tapeli alitumia mbinu rahisi sana kiasi kwamba kila nikifikiria nacheka tu

Jamaa katumia akili ndogo sana kutapeli, ila dhuluma kwa mungu ni jambo lisilokubalika ajiandae tu mbele za mungu
 
Na kosa kubwa huwa tunafanya kwa sababu ya STEREO TYPING... Yaani mtu akisema Mbagala, kuna picha inakuja ambayo si ya kweli kwa 100%... Au hata huko Tabata, wapo watu wa aina mbalimbali...

Wewe endelea kutafuta makosa tu, hutaki kujifunza... jikite kwenye ujumbe achana na mifano bwashee.
 
Kama mungu ni mjomba wako sawa
Mungu siyo Magufuli wala Kagame, hawazi kikatili na kishenz Kama wewe uwazavyo, yaani kwako Dhambi umeona ni huo utapeli tu, je? Wewe ni msafi mbele ya Mungu?
Huna dhambi yoyote ya kuhukumiwa?
Ndugu, peponi tutaingia kwa neema tu, Hakuna aliye safi chini ya jua, Pole sana kwa upofu ulionao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ha
Wananzengo, tuendelee kujilinda na kuwaombea wenzetu.

Maisha yanavyozidi kuwa magumu kila siku watu wanafungua ubongo na kuona fursa mpya, hii yote ni ili kuweza ku-survive. Hivyo majanga kwako wewe ni fursa kwa mwingine, hakuna aliye salama.

Basi bwana, yapata wiki sasa tangu tupate msiba [RIP Mzee wetu], ni maeneo fulani ya kijanja ndani ya jiji pendwa, Bongo Dar es Salaam.

Ilikuwa hivi:

Wakati ambao wengi wa wanafamilia wapo kwenye msafara wa kuupokea mwili kutoka hospitali, na kupitia maeneo ya ibada kabla ya kufika nyumbani tayari kwa kusafirishwa mkoa, alitokea mwamba [tapeli] aliyejivika usamaria wema.

Mwamba akiwa ameshachora ramani nzima, aliibuka nyumbani ambapo aliwakuta watu kadhaa, kwa ujasiri mkubwa akahitaji kuonana na mwenyeji mmoja wa familia ile.

Alichofanya ni kumwambia achukue vijana wawili watatu waongozane naye kwenda dukani kuchukua MCHELE, kusikia neema imeshuka naye bila kusita akafanya hivyo na safari ikaanza.

Kufika dukani mwamba akasema na mangi [taarifa za msiba anazo] kuwa yuko pale kwa niaba ya familia, apime mchele kiasi cha kilo 100, naye bila ajizi akafanya hivyo.

Baada ya kupima mangi akamkabidhi, mwamba akaugawa mchele mafungu mawili, kilo 20 vijana wabebe kupeleka nyumbani na kilo 80 zitasafiri mkoa kwa ajili ya msafara wa mazishi, hivyo bodaboda ili kupeleka kunako gari kumbe ndo katokomea nazo anakojua yeye.

Ikawa imeisha hiyoo.

Baada ya siku mbili tatu za nusu mlingoti, mangi analeta bili ya kilo 100 kwenye kikao cha ndugu.

Watu ooh watu eeeh, wanapigwa na butwaa kilo mia zimetumika wapi, wakikumbuka walivyolala njaa huko malaloni.

Ndipo yule kijana mwenyeji akaelezea mkasa mzima, na kushuhudia kuwa nyumbani waliambulia kilo 20.

Bongo Dar es Salaam ni Chuo Kikuu, kila siku kuna cha kujifunza, ukizubaa tu unawapa watu faida.
Hatar sana.
 
Hii ipo sana, tunaamini kifo hakina hodi... na mara nyingi kwa familia zetu bill hutegemea michango.

Iwe msiba au harusi mali kauli hutumika sana, hii filamu ilichezwa vema sana... hata mimi nakiri tu ningejaa mkenge.

Daa aisee Poleni

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Wananzengo, tuendelee kujilinda na kuwaombea wenzetu.

Maisha yanavyozidi kuwa magumu kila siku watu wanafungua ubongo na kuona fursa mpya, hii yote ni ili kuweza ku-survive. Hivyo majanga kwako wewe ni fursa kwa mwingine, hakuna aliye salama.

Basi bwana, yapata wiki sasa tangu tupate msiba [RIP Mzee wetu], ni maeneo fulani ya kijanja ndani ya jiji pendwa, Bongo Dar es Salaam.

Ilikuwa hivi:

Wakati ambao wengi wa wanafamilia wapo kwenye msafara wa kuupokea mwili kutoka hospitali, na kupitia maeneo ya ibada kabla ya kufika nyumbani tayari kwa kusafirishwa mkoa, alitokea mwamba [tapeli] aliyejivika usamaria wema.

Mwamba akiwa ameshachora ramani nzima, aliibuka nyumbani ambapo aliwakuta watu kadhaa, kwa ujasiri mkubwa akahitaji kuonana na mwenyeji mmoja wa familia ile.

Alichofanya ni kumwambia achukue vijana wawili watatu waongozane naye kwenda dukani kuchukua MCHELE, kusikia neema imeshuka naye bila kusita akafanya hivyo na safari ikaanza.

Kufika dukani mwamba akasema na mangi [taarifa za msiba anazo] kuwa yuko pale kwa niaba ya familia, apime mchele kiasi cha kilo 100, naye bila ajizi akafanya hivyo.

Baada ya kupima mangi akamkabidhi, mwamba akaugawa mchele mafungu mawili, kilo 20 vijana wabebe kupeleka nyumbani na kilo 80 zitasafiri mkoa kwa ajili ya msafara wa mazishi, hivyo bodaboda ili kupeleka kunako gari kumbe ndo katokomea nazo anakojua yeye.

Ikawa imeisha hiyoo.

Baada ya siku mbili tatu za nusu mlingoti, mangi analeta bili ya kilo 100 kwenye kikao cha ndugu.

Watu ooh watu eeeh, wanapigwa na butwaa kilo mia zimetumika wapi, wakikumbuka walivyolala njaa huko malaloni.

Ndipo yule kijana mwenyeji akaelezea mkasa mzima, na kushuhudia kuwa nyumbani waliambulia kilo 20.

Bongo Dar es Salaam ni Chuo Kikuu, kila siku kuna cha kujifunza, ukizubaa tu unawapa watu faida.
Nimecheka kama mazuri vile maisha magumu yanaongeza changamoto za utapeli
 
mkuu Watanzania tunaish kama ndugu, sasa linapokuja suala la msiba ni ngumu sana kuchunguzana, kwani kwa kipind hicho kila mtu yupo kwenye taharuki hivyo anapokuja mjanja ni rahisi sana kuwachanganya
Ngoja kidogo? Hao vijana watatu ni wanafamilia na Mangi anawafahamu? Kama Mangi wale vijana watatu walikuwa ni wageni machoni kwake basi yeye ndo katapeliwa na nyie kumlipa kwenu ni basi tu mmehurumia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom