Tulivyoibiwa na Serikali Wakazi wa Bunju Beach kwa Mkanada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tulivyoibiwa na Serikali Wakazi wa Bunju Beach kwa Mkanada

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mgt software, Jan 3, 2011.

 1. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,728
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  Sisi wakazi wa Bunju beach maeneo yaliyopimwa na Serikali Mradi wa Viwanja Elfu Ishirini(20,000.00) tulipokuwa tunachukua form pale Mwananyamala tuliambiwa kuwa kuanza Mradi wa Viwanja vipya vya Makazi Bora, tulienda kuviona na kuchua kila mtu awezavyo, kwenye kulipa sasa tuliaambiwa vianaanzia million 1, mpaka laki 6 lakini baadaye tuliambiwa kuwa fidia ya waliokuwepo ni kubwa kwa hiyo basi vitakuwa kuanzia millioni 1.5 mpaka million NNe(4 ) kufuatana na ahadi kuwa vitakuwa na kila kitu tukajikomba tukanunua, njoo basi kwenye ahadi ndio utaumia.
  1. Tuliambiwa tutaletewa maji sehemu zote.
  2. Tutapewa huduma ya Barabara kwa kiwango cha lami.
  3. Huduma ya Umeme.
  4. Drainege system itaunganishwa na ya serikali,
  5. Kujengewa mashule na Huduma ya Afya,
  6. kituo kikuu cha Police.

  baada ya hapo kinyume chake basi,
  1. Barabara walizoandaa zote walimwaga molamu alafu sehemu nyingi azipitiki vilibaki vichaka.
  2. Huduma ya maji tunaomba kwa wakazi wa mpiji kuunganishwa ni mpaka millioni mbili alafu bomba dogo na mgawao wa kila jumamosi. Bomba la maji linapita kwetu ambalo lilijengwa zamani lakini wakazi tunategemea maji kutoka mpiji kwa wanakijiji.
  3. Huduma ya Umeme - umeme umebadirishiwa kwa watu wa Bunju A na Bunju B, tukienda kuomba umeme wanatukejeri Tanesco kuwa tulizubaa ukachakachuliwa na CCM kuombea kura na Ushirikiano na Anjera aliyeshindwa kwa Kishindo. Ukienda bunju kuna matransforma matatu wakati watumiaji wachache sana (ukitaka data ninazo) huyu mama alisema kuwa wakazi wa Bunju beach sio wapiga kula kwa sababu wakati wa kujiandikisha walikuwa hawajaamia, ambavyo ilikuwa ni kweli kabisa.
  4. Baadhi ya maeneo yaliyoandaliwa kwa ajiri ya shule na Zahanati yamevamiwa na vijana wamejenga vibanda vyao, na ndio makazi ya vibaka na wavuta bangi(ushaidi hupo police Bunju A).
  Tunaomba Mama Tibaijuka awakumbushe ahadi ya makazi mapya na Bora waliosema kuwa Mradi Utakuwa wa mfano Tanzania sasa umekuwa wa Mfanano na nairobi magengeni!!!
   
 2. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,728
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  kama kuna miradi mingine yenye longolongo kama hii tuwe makini, serikali inapima viwanja kwa bei ghari alafu huduma mbovu, na hasa viongozi wengi wanajigawia kwa ajiri ya kupatia mikopo benki , au wanafanya malimbikizo ndio maana vichaka vinakuwa vingi, watu wamepewa miaka mitatu kuwa umejenga lakini viwanja vingi vina miaka kumi, ukiuliza eti ni cha balali au mwapachu . Mama Tibaijuka mulika viwanja vyote visivyo endelezwa utakuta ni vya wajukuu wa Rostam wanasubiri wakue,Utakuta ni vya meghji, au Sophia S, Anjera (mshidwa Ubunge aliyechakachua nyaya za umeme na transforma bungu beach kupeleka Bunju A, tunakumaind) na wengineo, jamani wanatiaribia maeneo badal ya maeneo bora yanakuwa vichaka bora
   
Loading...