G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,591
- 36,004
Mimi ni miongoni mwa walioapa kutokutoa rambirambi yangu kupitia serikali hii ya Magufuli na wadau wake mara baada ya kuona utapeli mkubwa sana uliofanyika kule Kagera. Nashukuru sana Mungu alinikumbusha kiapo changu kule Arusha kwenye vifo vya watu 35.
Baada ya kuona sakata la rambirambi za kule Arusha likishikiwa bango na mwana siasa mwingine wa aina ileile ya wanasiasa wengi wa serikali hii, niliamua kukaa pembeni na kusubiri mwisho wake.
Ni aibu tena sana kwa serikali kutumia michango inayoitwa kwa jina la "rambirambi" kugharamia shughuli yoyote ile inayoisimamia. Nini maana ya mfuko wa maafa ndani ya ofisi ya waziri mkuu? Kwanini tutumie rambirambi za wafiwa kugharamia mazulia ya kutembelea viongozi? Kutengeneza majukwaa ya viongozi? Kukodi vipaza sauti vitakavyotumiwa na viongozi kwa mbwembwe kujitwalia majina mapya?
Hizi fedha zilitakiwa zote zielekezwe kwa wafiwa tena wakipewa mgao sawa kwa wote! Siyo kutumia eti sehemu ya fedha kugharamia shughuli za mazishi! Shughuli zipi? Kupamba uwanja? Ingejulikana kama itakuwa hivyo basi ni heri kila mmoja angekuja kimyakimya kuchukua marehemu wake na kwenda kumzika pengine tungeokoa hizo gharama za kupamba uwanja na kukodi vitu mbalimbali na kuelekezwa kwa wafiwa? Tunagawa kwa shughuli? Rambirambi?
Serikali hii kwa kweli imeonyesha picha nyingine mbaya baada ya ile ya Kagera. Ni picha ya kutokujali na kutumia matukio haya kujijenga. Siyo sahihi hata kidogo.
Tumetumia sehemu ya michango kugharamia mazishi? Pole kwa wale waliotoa kwa moyo wakijua kuwa wafiwa walau watapata faraja na kupona maumivu kwa kuondokewa na wapendwa wao!