Tulitegemea Sheikh wa Mkoa wa Dar awasemee Masheikh walio Korokoroni miaka zaidi ya 5 si kubishana na Mange, JamiiForums

Tee Bag

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
7,200
5,553
Kwa sentensi chache niseme nionavyo mimi kuhusu hii "vita mpya" kati ya dada Mange na Sheikh mkuu Dar, Alhad Mussa Salum. Kwanza nieleze tu kuwa nauheshimu sana Uislamu kama navyoheshimu imani za watu wengine. Pia nawaheshimu viongozi wa kiislamu wakiwemo masheikh kama navyoheshimu viongozi wa imani na madhehebu mengine.

Lakini nadhani Sheikh Salum hakuwa na sababu ya kumjibu Mange. Kuna mambo ambayo tunategemea kuona Sheikh Mkuu wa mkoa akifanya, sio kufuatilia mambo ya instagram na kujibu. Tunategemea kuona akipambana kupigania haki za waislamu ktk namna itakayoleta matokeo chanya kwa waislamu na taifa kwa ujumla.

Tunategemea kumuona akiwasemea masheikh waliokamatwa miaka zaidi ya mitano iliyopita na mpaka leo wapo tu mahabusu bila kujua hatma yao. Aombe kesi zao zisikilizwe haraka (JPM anasema chapchap) ili kama wana hatia wahukumiwe, na kama hakuna ushahidi wa kuwatia hatiani basi waachiwe HURU, kuliko kuendelea kuteseka tu mahabusu miaka zaidi ya mitano kwa madai kwamba upelelezi haujakamilika.

Hivi wakikaa mahabusu miaka 10 halafu bado ushahidi wa kuwatia hatiani usipatikane itakuaje? Au wakakaa mahabusu miaka 30 halafu wakaja kuachiwa huru kwa kuonekana hawana hatia itakuaje? Sheikh Salum haoni kama wenzake watakua wameteseka bila sababu? Sasa kwanini asiwasemee? Wanasheria wanasema "Justice delayed is justice denied", yani haki inayocheleweshwa ni haki iliyopotezwa.

Hawa masheikh wakiendelea kukaa mahabusu kwa miaka mingine zaidi na wakaja kukosekana na hatia it is justice denied. Ndio maana nilimpongeza Rais JPM alipomwambia Jaji Mkuu kwamba anapenda kuona kesi zikisikilizwa chapchap. Naamini na hii ya Masheikh itasikilizwa chapchap kama alivyoshauri Rais wetu mpendwa (japo wameshasota miaka mingi sana ndani).

Je Sheikh Salum anajua kuna wenzie wanaoteseka huko magerezani? Wapo wanaodaiwa kudhoofika sana kiafya, wakiwemo akina Sheikh Fareed, Mselem na wengine. Nilitegemea kuona Sheikh Salum akipambana kwa ajili ya HAKI na USAWA kwa watanzania wote (wakiwemo masheikh walioko gerezani) na sio kupambana na Mange Kimambi. I stand to be corrected.!!

By G. Malissa

22a0f2ecf3bc75403db62fdbfd692837.jpg
 
Unoko upi? Huyo shehe kutwa anashinda Ofisini kwa Maliyamungu Bashite kumpelekea waganga wa kienyeji na ndumba, hafai kutetewa huyo BAKWATA mfukuzeni haraka, wapo mashehe wazuri waadilifu kibao wanafaa kuchukua nafasi yake.

Usitupangie Mbona Wenu anashinda Na Wachawi atusemi

Acha kushikwa akili
 
Back
Top Bottom