Tulitazame hili tukio la kuteswa na kuwa hai kwa dr uli katika sura ya unabii

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
13,266
4,716
Yamesemwa mengi juu ya mgomo wa madaktari unaoendelea. Yamesemwa mengi juu ya kauli za serikali hasa ile ya waziri wa afya kuwa"SASA TUTAPIMANA NGUVU NA MADAKTARI" na hata kauli ya waziri mkuu kuwa " sasa basi". Niko upande unaoamini kuwa ni serikali ndiyo iliyokuwa imedhamiria kumuua DR Uli hasa baada ya kumhoji ili kujua kitu gani kiko nyuma ya huu mgomo mbaya.

Kwa wale mnaoamini katika unabii na kwa wale liobahatika kuangalia ama kusikia ama kuhudhuria ibada ya jumapili iliyopita katika kanisa la Agape mliona na kusikia jinsi mchungaji Fernandes alivyokemea viongozi wanaokalia kujaza matumbo yao na kuacha wagonjwa bila huduma, alionya juu ya madkari kumuogopa Mungu na viongozi wa serikali pia kuacha ufisadi na kumtumikia Mungu. MY TAKE: HAIKUWA SAHIHI KWA SERIKALI KUFIKIRIA KUWA KIFO NA MATESO YA KIONGOZI WA MADAKTARI NDO NJIA SAHIHI YA KUPATA SURUHU.

Tutazame pia yalitokea kule Misri na juu ya utawala wa Talibani kwa jicho la kinabii pia.

1. Siku chahche kabla utawala wa Taliban haijavamiwa na majeshi ya muungano, kulikuwa na wazungu 12 waliokuwa wamefikishwa mahajani na kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa kukutwa na vitabu(biblia) vya dini ya kikristo wakiwa nchini humo. Kosa lao ilikuwa ni kujaribu kueneza dini ya kikristo katika nchi ya kiislam. Baada ya hukumu hiyo, jumuiya nyingi za kimataifa ziliomba watu hao waachiwe huru bila mafanikio. Kabla adhabu yao haijatekelezwa- utawla uliangushwa.

2. Misri: siku chache kabla wananchi wa misri hawajaanza kuandamana kupinga utawla wao, kulikuwa na matukio mengi ya waumini wa dini ya kikristo kuteswa, wasichana kubakwa na kulazimishwa kufunga ndoa za kiislam. Matukio haya yalikuwa yakilipotiwa katika mamlaka za dora bila waathirika kupata msaada. Hatimae utawla ukaanguka.

Angalizo kwa serikali ya Tanzania na mgomo wa madaktari: Chimbuko la mgomo huu ni kuona kuwa sekta ya afya haipewi kipaumbele. Serikali inanunua magari ya kifahari lakini haitoi kipaumbele kwa kununua zana za kutolea huduma za afya. Atleast Mungu ametuonesha kuwa walinzi wa amani ndio waliohusika kujaribu kusimamisha mapigo ya moyo ya Dr.Uli.

Onyo: hii siyo njia sahihi ya kumaliza tatizo.
 
Back
Top Bottom