Tulipotoka, tulipo na tunapoelekea miaka 57 ya Uhuru

Dec 13, 2018
30
140
TULIPOTOKA, TULIPO NA TUNAPOELEKEA,MIAKA 57 YA UHURU 1961-2018.

Leo 13:15pm,9/12/2018.

Hongera Taifa letu na pongezi nyingi ziwafikie Watanzania tunapofanya Jubilei ya miaka 50 ya Uhuru wetu, tunapofikisha miaka 57 ya Uhuru ni mwanzo mzuri wa kuelekea kutimiza miaka 50 mingine ya Maendeleo makubwa ya kiuchumi.

Maadhimisho haya ya miaka 57 ya Uhuru wa Taifa letu la Tanzania tangu kumalizika kwa utawala wa kikoloni mnamo mwaka 1961.Tunakumbuka safari ndefu tuliyopitia Watanzania hadi kufikia Tanzania ya Viwanda na uchumi wa kati, hii ndiyo Tanzania iliyokusudiwa na awamu zote tano,tukianza na awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere, Awamu ya pili ya Mzee Ali Hassan Mwinyi, Awamu ya tatu ya Benjamin Mkapa,Awamu ya nne ya Jakaya Kikwete na Awamu ya hii ya tano ya Dr John Pombe Magufuli.

Niweke bayana ya Sherehe za Kitaifa ambazo zinatukumbusha maangaiko yetu tulipotoka, tulipo na tunapoelekea,kuna Sherehe ya siku ya Uhuru wa Tanganyika,Sherehe ya Mapinduzi ya Zanzibar na kwa mjumuisho tunayo Sherehe kubwa ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaani siku rasmi ambapo taifa la Tanzania lilizaliwa.

Tanzania yetu hii ya leo,
Tangu imezaliwa mwaka 1964 imepitia vipindi tofauti tofauti ambavyo kwa namna moja au nyingine vimeweza kuathiri sana mwelekeo wake wa kiuchumi, Kisiasa na Kiutamaduni. Leo, hii tumepata Uhuru lakini bado hatuwezi kabisa kujitoa kwenye masalia ya Ukoloni (Colonial Legacies) wa mataifa makubwa ambayo yamewahi kututawala kama Muingereza na Mjerumani. Pia upande wa pili wa shilingi ndugu zetu wazanzibari bado hawawezi kujitoa kwenye makucha ya Ushawishi wa Dola la Kisultani uliowahi kutokea huko kwao visiwani.

Tanganyika yetu imepata uhuru wake mwaka 1961 lakini bado mpaka leo hii ukiangalia kwa umakini sana hutamuona Mirambo, Mangi wala Chief Kingalu Mwanabanzi, wala Chief Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga(Mkwawa) wala Chief Machemba, wala Chief Rumanyika, wala Kinjekitile Ngwale bali utamwoma Malkia au Mfalme wa Uingereza: Vivyo hivyo Zanzibari ya leo Ukiangalia katika mifumo yake mingi bado utaona mengi yaliyowahi kuwepo kabla ya Mapinduzi ya 1963 na kabla ya Muungano na Tanganyika wa mwaka 1964.

Tunapozungumzia tulipotoka kama Taifa wanazuoni wengi wa ndani na nje ya mipaka yetu hupenda kuanzia miaka ya 1960's hasahasa baada ya Azimio la Arusha la mwaka 1967 ambapo Tanzania iliitangazia dunia msimamo wake katika Siasa na mahusiano ya kimataifa.Katika kuitangazia dunia Uhuru wetu wa kisiasa kama Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere alitangaza misingi mikuu miwili ya kifalsafa . Mosi, falsafa ya Umajumuhi wa Kiafrika (Pan-Africanism) na Pili, falsafa ya Ujamaa (Marxist Socialism).Misingi hii ilitufanya tuwe Taifa la Kijamaa,lenye undugu, haki na usawa kwa kila mmoja wetu.

Mwalimu Julius Nyerere aliazimia kuijenga Tanzania kama nchi ya Kijamaa, ambayo inakubali haki na usawa kwa kila mmoja wetu na pia inakubali itikadi za kidini na kisiasa za kila mmoja wetu na haki za binadamu.Uchumi wa Taifa ujengwe kwenye usawa pasipo kumnyonya mfanyakazi wa mjini wala kijijini.Watu wawe wenye kuchangia na kumiliki kiasi katika uchumi wa Nchi, Mwalimu Nyerere hakuwa mbali na Kiongozi,Baba wa Taifa la Ghana,Kwame Nkrumah ambaye Alikuwa na ndoto ya kulikomboa Taifa la Ghana toka kwenye ubeberu na ubepari, ambapo alimtaka kila Mghana,kuchangia katika uchumi wa Taifa kwa uwezo alionao na nguvu alizonazo na kuja na Mpango wa miaka 7 ya maendeleo kwa Taifa la Ghana.

If the plan Nkrumah wrote was allowed to be fully implemented, Ghana would have been a middle income country by 1978 and as an advanced country by 1989 onwards. We would have reached and passed S. Korea, Singapore etc by now.

The Singapore president that time came to Nkrumah and took the plan to help his country and that is why Singapore is what it is right now. The West will never leave us to grow since if we do, they wouldn't have our raw materials for cheap anymore. So any leader that comes to power in Africa is bought right in your first month of being in office.

The only way Ghana and Africa can progress is to go back to nkrumah's plan which Botswana and few African countries inncluding Ethiopia and Tanzania are now on. Magufuli of Tanzania has also come on board and Tanzania is progressing.

Plan ya Kwame Nkrumah iliigwa na Singapore na hivi sasa Singapore ni Nchi iliyoendelea sana, Ethiopia imeiga plan na Sasa Tanzania, chini ya Rais John Magufuli anaitekeleza plan.

-Tulipo na tunapoelekea kama Taifa.

Nadhani wote tunafahamu na tunakumbuka juhudi za Rais John Magufuli katika kuyafuatilia mapato ya maliasili zetu na hasa suala la mchanga wa madini.

Kuna baadhi ya watanzania waliunga mkono kampuni ya ACACIA hata sasa wanapoendelea na kesi na wengine walimuunga mkono Mh Rais Magufuli hata sasa Serikali inaposhughulika na suala hilo.

Sasa tunapoadhimisha sherehe ya miaka 57 ya Uhuru wa Taifa letu, tujaribu kusoma historia ya ukombozi wa Tanzania bara na Visiwani.

-Malengo ya kuja kwa Wakoloni.

1. Kutafuta malighafi kwa ajili ya viwanda vyao huko Ulaya.

2. Kutafuta masoko ya kuuzia bidhaa zilizozalishwa na viwanda vyao huko Ulaya.

3. Ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo cha mazao ya biashara.

4. Vibarua wa gharama ndogo ili waweze kuzalisha malighafi.

Haya ni baadhi ya malengo ya kuja wakoloni katika bara la Afrika. Nchi nyingi za Afrika zimepata uhuru, je Mataifa ya Ulaya bado wana malengo haya?

-Mapambano dhidi ya Uvamizi kutoka Ulaya.

Baada ya kuingia kwa wakoloni katika nchi yetu wazee wetu walipigana sana ili kuwaondoa wakoloni. Haya ni baadhi ya madhumuni ya kupinga uvamizi wa wakoloni.

1.Nia ya kuendelea kujitawala na kulinda heshima yetu sisi Watanzania.

2. Kupinga Sera za kinyonyaji za wakoloni.

3. Kupinga kunyang'anywa ardhi yetu na mali zetu za asili.

4. Kutetea biashara zetu.

5. Kupinga kunyang'anywa rasimali zetu.

Babu zetu walitumia mbinu mbalimbali ili kupinga ukoloni licha ya kuwa walikuwa na silaha duni lakini walijitoa kwa moyo mmoja kuingia vitani na wakoloni. Kumbuka wakoloni kwa kipindi hiko walikuwa tayari wana silaha za kisasa kama bunduki, mizinga huku Wazee wetu enzi hizo wakiwa na mapanga, mikuki, mishale na mawe.

-Mashujaa wetu,Viongozi wa Jadi/Machifu waliopigana Vita na Wakoloni.

Machifu kutoka maeneo mbalimbali waliongoza mapambano dhidi ya wakoloni kwa lengo ya kuendelea kujitawala. Licha ya kuwa na silaha duni.

(1) Maeneo ya Pwani na Bahari ya Hindi; Maeneo ya Kilwa, Bagamoyo, Dar es Salaam na Pangani wakiongozwa na Abushiri bin Salim na Bwana Heri na Hassani bin Omari Makunganya walipigana vita dhidi ya Wajerumani.

Wajerumani walishinda vita hivyo na kumkamata na kumnyonga Abushiri mnamo 15/12/1889 Pangani.

Hassani bin Omari Makunganya aliongoza watu wake kupigana dhidi ya Wajerumani kuanzia mwaka1894-1895. Makunganya alishindwa vita na kutoroka November 1895 baadae alikamatwa na kunyongwa huko Kilwa Kivinje mahali palipoitwa"Mwembe Kinyonga"mwaka 1896.

(2)Wahehe; Wakiongozwa na Mtwa Mkwawa walipigana dhidi ya Wajerumani kuanzia mwaka 1891-1898. Mkwawa alikuwa na jeshi imara hivyo alifanikiwa kuwashinda Wajerumani na kumuua kamanda Emil Von Zelewisky.

Wajerumani walijipanga na kuanzisha tena vita hivyo Mkwawa alishindwa na mwaka 1898 alipiga risasi na kufa ili asishikwe mateka.

(3)Wanyamwezi; chini ya Mtemi Isike wa Tabora walipigana na Wajerumani kuanzia mwaka 1886-1893

(4)Wamatumbi; chini ya uongozi wa Kinjeketile Ngwale wakishirikiana na baadhi ya makabila kama Wangoni, Wasangu, Wamakonde, Wangindo, Wabena, Wapogoro na Wambungu walipigana vita dhidi ya Wajerumani kuanzia mwaka1905-1907 vita hivyo viliitwa vita vya majimaji.

Hawa ni baadhi ya Machifu na makabila waliopigana vita dhidi ya wakoloni kwa njia ya vita, baadhi ya viongozi walinyongwa kinyama na wengine walijiua ili wasikamatwe na wakoloni.

Historia hii lazima tujikumbushe ili tuweze kuwa wazalendo kwa ajili ya Nchi yetu kwa vizazi vijavyo kama walivyofanya wazee wetu. Mzungu ni mzungu tu alikuja kama mkoloni lakini Leo anakuja kama mwekezaji.Makampuni mengi hivi leo Ma CEO na Ma MD ni wageni kutoka nje ya Tanzania.

Hivi leo baadhi ya Watanzania waliogopa Mh Rais kazuia makontena ya mchanga wa dhahabu, Je wangekuwa enzi za harakati za ukombozi wangeweza kutoka kifua mbele na kupigana vita dhidi ya wakoloni?

Mgogoro kati ya Marekani na North Korea nilitegemea ungekuwa kama mwalimu wetu mzuri sisi Watanzania ambao tumebarikiwa utajiri wa asili wa kila namna kiasi cha kulinga kabisa mbele ya Mzungu, lakini tunakuwa wa kwanza kwa baadhi yetu kuisaliti nchi kwa vipande vya fedha.

Korea Kaskazini ni Nchi masikini lakini walisimamia maamuzi yao licha ya Marekani kutaka kuishambulia. Je tungekuwa sisi si Chadema wangetangaza maandamano nchi nzima kuipinga Serikali!? Tungeweza kusimamia maamuzi yetu kweli?

Siku yoyote ukisikia wazungu wanamyooshea kidole kiongozi wa Afrika Kwa lolote na chochote ujue kwamba kiongozi yuko sahihi kwa hilo analolifanya kwa nchi na watu wake lakini sio sahihi kwa maslahi yao.Mfano,Mwalimu Nyerere alitenda mengi mema Kwa watu wake na Africa lakini wazungu walimpenda kumkweza Mandela kuliko Nyerere kwa kuwa tu Nyerere aliupinga kabisa ubepari wao, na ubeberu.

Wazungu walimpenda Mobutu Tsetseseko, Dr Kamuzu Banda, Ngwema lakini sio Mwalimu Nyerere,Kenneth Kaunda,Patrice Lumumba,Nkwame Nkrumah,MuamnarGhadaffi, Maduro, Edogan, Saadam Hussein.

Kelele za Wazungu ni dalili za usahihi wa kiongozi wa Africa kwa taifa lake kiuchumi na uchumi wa Nchi ya Afrika unapokua, ni hatari kwa nchi za Wazungu.

Ndoto ya Kwame Nkrumah, Patrice Lumumba, Kenneth Kaunda inatimia ama kutimizwa na Rais John Pombe Magufuli, ni furaha na heshima kubwa kutimiza ndoto za Mashujaa wetu toka kale akina Chef Rumanyika, Chief Mkwawa, Kinjekitile Ngwale, Kwame Nkrumah, Patrice Lumumba, Julius Nyerere na Kenneth Kaunda.Waafrika popote walipo wanaokerwa na wizi na uporaji wa mali zao unaofanywa na Mafisadi ama vibaraka wa Mabepari wangefurahia laiti wangekuwa na rais kama wa kwetu, John Pombe Magufuli ambae katika Vita ya kiuchumi dhidi ya Mabepari hana mpinzani chini ya jangwa la Sahara
Kwa sasa. Lakini wazungu kamwe huwa hawataki viongozi wa Africa wa aina hii.
Wazungu wanakumbatia maslahi yao tu,Viva Rais John Magufuli, Viva Uhuru Day, Mungu ibariki Tanzania.

Nikiishia hapa, Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
 
Back
Top Bottom