Tulipotoka, Tulipo na Tunapoelekea kuna Mabadiliko?

Mafuchila

JF-Expert Member
Apr 29, 2006
752
62
Wana JF,
Bila ni muhimu kukumbushana tulipotoka kwa kuangalia mifano mbali mbali na matendo mbali mbali ya viongozi na wanasiasa wetu, ili tujue wapi tunasimamia na wapi tunaweza kuondoa boriti kwenye macho yetu kabla ya kuondoa boriti kwenye macho ya jirani zetu. Bila shaka tumetoka mbali na nukuu hii niliyoipata kwenye makala ya Joseph Mihangwa inaweza kututhibishia hilo. Swali je sisi ni bora zaidi kuliko majirani zetu? nini kinatufanya tuwe bora zaidi kuliko wenzetu? Tutafakari kwa pamoja nukuu hii:

Oktoba 1, 1968, Mbunge wa Rungwe, Wilfred Mwakitwange alitaka ufafanuzi bungeni kama ni Chama cha TANU kilichokuwa kinaongoza Serikali, au ni Serikali iliyokuwa ikiongoza TANU. Alitaka pia kujua, kati ya Bunge na Serikali ni kipi kilicho juu ya kingine?.

Richard Wambura, Naibu Waziri katika ofisi ya Makamu wa pili wa Rais, alijibu kwa kiburi: “ Nataka ieleweke kwamba Chama ndiye “Mfalme,” na wabunge wanatakiwa kufanya kazi chini yake, na waelewe kuwa Bunge hili si la wananchi bali ni la Chama…”

Mwakitwange alikuja juu, akahoji, kwa kuwa Chama kimejichukulia jukumu la kudhibiti na kuadabisha Wabunge, ni nani atakayekiadabisha Chama? Na kwa nini Chama chenye wanachama wasiofikia hata asilimia moja ya Watanzania kipewe nguvu hizo za kidikteta? Ndipo aliposimama Makamu wa Pili wa Rais mwenyewe, Rashidi Mfaume Kawawa, akasema: “ Chama ni kikuu kwa vyote, na ndicho pekee kinachosimamia mapinduzi ya nchi. Nataka hili lieleweke hivyo kwa wote, na asiyetaka aondoke…”. (The Standard, Oktoba 2, 1968). Siku chache baadaye, Mwakitwange na wabunge wenzake sita walifukuzwa uwanachama wa TANU na hivyo kupoteza ubunge kwa sababu ya kuhoji “utukufu” wa Chama.


Source: Raia Mwema 2/07/2008
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom