Tulipotoka ni wapi? Tulipo ni wapi? Tunapokwenda na CCM ni wapi? Miaka 44 toka kuanzishwa kwa CCM

seif_tanzania

Member
Nov 23, 2017
14
2
Katika kipindi na nyakati tofauti toka kuundwa kwa CCM baada ya kuungana kwa Afro Shirazi Part na TANU ambapo viliungana tarehe 05/02/1977 ikiwa TANU ni chama cha kisiasa kutoka Tanganyika na ASP kutoka Zanzibar ikumbukwe TANU iliundwa 7/7/1954 na ASP iliundwa tar 5/02/1957 ambapo toka kuundwa kwa CCM itikadi ambayo imekuwa ikitumika ni UJAMAA NA KUJITEGEMEA. Itikadi hii ilipewa nguvu za kisera mwaka 1967 lilipotangazwa Azimio la Arusha.

Kutokana na azimio hilo uchumi uliwekwa mikononi mwa umma. Itikadi hiyo pia ilisisitiza umuhimu wa kuishi pamoja hasa katika vijiji vya Ujamaa.

Vyama vya TANU na ASP vilijenga historia ya kushirikiana na kuunga na mkono tangu kuundwa kwao. Kwa hiyo, mara baada ya mapinduzi ya Zanzibar, Serikali ya TANU iliyatambua mapinduzi hayo na kuyaunga mkono kwa vitendo. Miezi mitatu baada ya mapinduzi ya Zanzibar ushirikiano na udugu wa jadi wa wananchi wa Zanzibar uliimarishwa kwa kitendo cha kimapinduzi cha kuunganisha nchi mbili hizi katika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao sasa unaitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maadhimisho ya miaka 44 toka kuanzishwa kwa chama cha mapinduzi inatukumbusha wapi chama cha mapinduzi kimetoka,wapi ambapo tulipo na dira ya chama kwa nyakati zijazo. CCM ndio chama kikubwa Tanzania na Afrika lakini pia ndio chama ambacho kimebeba dira na muangaza wa maendeleo katika Taifa hili ambapo katika maadhimisho haya Kauli mbiu ni "CHAMA IMARA, SERIKALI IMARA NA MADARAKA YA WANACHAMA."

Chama cha mapinduzi ni chama chenye historia ya pekee Afrika, Historia yake ni kutokana na mafanikio juu ya uendeshaji wa siasa zake ambazo zimelenga nje na kujenga chama lakini kuangalia namna bora ya kuendesha Taifa kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa kwenye nyaja ya uchumi, siasa na utamaduni.

Chama cha mapinduzi ni chama cha kijamaa ambapo itikadi yake toka kuanzishwa kwake ni UJAMAA NA KUJITEGEMEA, ambapo kazi kubwa ya CCM kwa sasa ni kuziunganisha nguvu zote za kijamaa na za kimaendeleo nchini na kuziongoza katika kujenga Taifa lenye usawa ambao utakuwa na ushirikiano wa kimapinduzi baina ya watanzania na wapenda maendeleo wote katika Afrika na Duniani huku tukiendeleza mapambano dhidi ya unyonyaji, ukoloni mamboleo, ubepari na ubeberu.

Chama cha mapinduzi ni chama ambacho kimekuwa daraja la kuweza kuzalisha viongozi ambao wanatija katika Taifa ambapo kupitia Jumuiya zake mbalimbali hasa ya Umoja wa vijana imekuwa darasa bora la kuoka viongozi ambapo kwa kiasi kikubwa wamekuwa na tija katika Taifa letu.

Leo tunasherekea miaka 44 toka kuanzishwa kwa CCM muhimu tutambue CCM ndio chama na chombo ambacho kimekuwa kikiongoza serikali ya Taifa hili toka Uhuru mpaka sasa hivyo tuzungumziapo mafanikio ya Taifa kwa asilimia 100% ni mafanikio yatokanayo na CCM kupitia Utekelezaji wa Ilani yake vyema ambapo Mchango mkubwa wa CCM toka Uhuru tumeweza kupambana na maadui wakuu wa maendeleo ambapo ni UMASIKINI, UJINGA NA MARADHI.

Wanachama wa chama cha mapinduzi mnapaswa kujenga Itikadi ya Chama cha mapinduzi muhimu sana tukatambua kwamba Itikadi na uimara katika kuisimamia ndio itakayosaidia katika kuhakikisha tunakijenga chama vyema ambapo kwa maoni yangu kuna mambo matatu yakiendelea kufanya kwa kasi kubwa yataendelea kukijenga chama vyema.

1.Uimara wa chama
2. Tabia na mienendo ya viongozi wa chama
3. Utendaji wa Serikali ya CCM

Mambo haya matatu yakifanyika vyema yataisaidia kwa kiasi kikubwa chama kuendelea kushika Dola na kuwa chama chenye nguvu.

Heri ya kumbukizi ya miaka 44 ya chama cha mapinduzi.
ccm2.jpg
 
Heri ya kumbukizi ya miaka 44 ya chama cha mapinduzi.View attachment 1694962
Wakati tunapata Uhuru watanzania walikuwa wskila Milo mitatu kwa siku, chain asubuhi, chakula cha mchanga na cha jioni. Leo hii tuko kwenye uchumi wa kati wa juu! Watanzania wanapata mlo mmoja nao wamashaka!
 
Mwenyezi Mungu awasamehe na kuwarehemu wote walioshiriki kwa makusudi kabisa,au hata kwa bahati mbaya kuianzisha CCM
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom