Tulipoongea walitusema sie wapigaji, leo wanafanya tulioyasema

Ni vitu vya kushangaza sana Mkuu. Kibunga kumbakumba AKA Membe alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje alijitahidi sana kupigia debe hii issue ya uraia pacha lakini akakosa support ya Kikwete kwani alishaona maccm hayaungi mkono na yalikuwa na dhana POTOFU ya kwamba Watu wataiba au kufanya ufisadi Tanzania kisha kuikimbia Nchi kwenda huko walikopata uraia, lakini ukweli ni kwamba majizi na mafisadi wala hayana uraia pacha yanakwiba pesa chungu nzima huku yakingiana vifua hivyo kutochukuliwa hatua za kisheria.
Hawa jamaa wana akili za kuiba kuvukia barabara tu!! Ukiona wanavyopinga sera zilizoleta mapinduzi ya kiuchumi duniani kama mtu mwenye akili utaishia kuwasikitikia tu
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kikundi chenu cha wenye akili kina wabunge wangapi bungeni? Tuanzie hapa kwanza....
Utapataje wabunge Kwa uchaguzi uliogeuzwa kuwa uchafuzi??? Nadhani kama huna la kusema kwenye mada kuu ni bora ukae kimya kuliko kuleta tabia zako za kilumumba humu
 
Nakubaliana na wewe ndugu kwa sehemu kubwa. Ila Tatizo linakuwa sehemu moja tu. Haya yote yanasababishwa na sera mbovu za ccm
Sera mbovu za CCM zisingeweza kutekelezeka kama wananchi wangezikataa kundakindaki.

Wananchi, at the risk of sounding like I am blaming the victim, wamejilegeza sana na kukubali kwenda kwa falsafa za "hewala, hewala".

Imefikia wakati hata hao wapinzani wakianza kuikimbia nchi siwezi kuwalaumu.
 
Kweli kabisa mkuu. Nakubaliana na wewe!! Kuna shida sana kwa upande wa wananchi na ndo mana wanageuzwa geuzwq na kukandamizwa kila siku
 
Nakumbuka Membe alisafiri Nchi nyingi tu zenye kuruhusu uraia pacha zikiwemo Ghana, Nigeria ba baadhi ya Nchi za Caribbean ili kujifunza manufaa Nchi hizo zinazoyapata kutokana na uraia pacha ili atetee hoja yake kwa ushahidi wa kutosha lakini hakufanikiwa.
Hawa jamaa wana akili za kuiba kuvukia barabara tu!! Ukiona wanavyopinga sera zilizoleta mapinduzi ya kiuchumi duniani kama mtu mwenye akili utaishia kuwasikitikia tu
 
Sera mbovu za CCM zisingeweza kutekelezeka kama wananchi wangezikataa kundakindaki.

Wananchi, at the risk of sounding like I am blaming the victim, wamejilegeza sana na kukubali kwenda kwa falsafa za "hewala, hewala".

Imefikia wakati hata hao wapinzani wakianza kuikimbia nchi siwezi kuwalaumu.
Kipimo bado hakijajaa.Siku kikijaa ni balaa.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Nasikia Rais moi wa Kenya ndicho alichofanya aliwaambia wakenya walete pesa lakini wasitoe pesa nje na akawaambia hatawauliza wamezitoa wapi, naona na mwinyi kaamua kuuvaa ubeperi mzimamzia.
 
Kweli kabisa mkuu. Nakubaliana na wewe!! Kuna shida sana kwa upande wa wananchi na ndo mana wanageuzwa geuzwq na kukandamizwa kila siku

Mwananchi mwenye akili ni yule anayeangalia nani kashika panga, panga likishikwa na mwenye akili hapo mnaweza kulalamika lakini likishikwa na kichaa, uwiii 🤣
 
Tuliwahi ksema humu kwa sera za CCM hii na namna yao ya ufanyaji kazi kamwe Tanzania haitofikia kuwa nchi yenye maendeleo ya kweli ya wananchi na nchi kwa ujumla.

... sera za kutaifisha hela za watu wanazoingiza nchini kwao.

... sheria za kibank za kuwabana watu kufanya miamala ...

Miradi tunayohangaika nayo Tanzania kama ya treni, miundombinu na masoko ya uhakika yenye hadhi vyote vingeweza kufanywa kwa fedha zinazoingizwa nchini na watu hawa kwa utaratibu mzuri.
...

Mkuu Lord denning, uchaguzi umeisha na Serikali iko kazini wewe unaendelea na lawama, kulalamika na kujashifu pasipo kuwa na hoja za nini kifanyike ili hayo madai yako yapate suluhisho la kudumu.

Yawezekana madai yako yakawa na ukweli lakini bahati mbaya ndani ya kambi ya vyama vya siasa hakuna kiongozi mwenye maono ya kutenda na kutatua kero hizo. Wengi wao, kama siyo wote, wana fikra za utegemezi na ndiyo maana lawama, kama hizo zako, huzungumzwa katika misingi ya kulalamika ndani na nje ya nchi. Tungetegemea matatizo ya ndani kijamii, kisiasa na kiuchumi, yangetatuliwa ndani kwa ndani kwa ushirikiano na Chama Tawala ili Serikali yake itekeleze kwa faida ya nchi na siyo chama.

Isitoshe nimepitia Ilani za Uchaguzi, za vyama vyote zilizopo, ni Ilani ya CCM tu yenye Sera zinazohusu uchumi wa kujitegemea. Natoa nukuu chache, kama ifuatavyo:

Chama Cha Mapinduzi kinatambua umuhimu wa kujenga uchumi wa kitaifa ili kuhakikisha kwamba Watanzania ndio wanufaika wakuu wa uchumi na maliasili za nchi na ndiyo wenye kauli juu ya namna uchumi unavyoendeshwa. Kwa muktadha huo CCM itaelekeza Serikali kuendelea na juhudi za kuifanya Tanzania kuwa nchi inayojitegemea kiuchumi pamoja na kuimarisha mahusiano ya kiuchumi na nchi nyingine. Juhudi maalum zitaelekezwa kuhakikisha rasilimali za asili za nchi hii, hasa ardhi, madini, gesi asilia, mafuta, maji na misitu zinanufaisha wananchi na Taifa kikamilifu.

Uchumi ni nyanja kuu katika maendeleo ya binadamu. Kwa kutambua hilo Chadema kimejipanga kuutafsiri ukuaji wa uchumi kwa vitendo ili kuwepo kwa mabadiliko chanya katika maisha ya kila Mtanzania. Hili litawezekana kwa kufumua mfumo wa sasa wa uchumi wa kijamaa ambao umeshindwa kuboresha hali ya maisha ya Watanzania, na kuanzisha mfumo wa soko jamii ambao unalenga kufungua fursa kwa kila mtu kutumia vipaji vyake katika kuzalisha na kumiliki mali. Mfumo huu mpya wa uchumi wa soko utaambatana na uanzishaji wa uchumi wa kidigitali ambao unazidi kushika kasi katika nyanja zote za uzalishaji na utoaji huduma katika dunia ya utandawazi.

Dhamira yetu (ACT-Wazalendo] ni kujenga Tanzania yenye uchumi wenye manufaa kwa wananchi na Serikali kwa ujumla; na siyo kukuza uchumi wa Serikali pekee au kusherehekea ukuaji wa takwimu za kiuchumi na ongezeko la mapato ya kikodi huku walipakodi (wananchi) wakiachwa katika ufukara, kukata tamaa, hali ngumu za maisha na mazingira magumu ya kutengeneza kipato.

Ukichambua nukuu hizo, kuhusu uchumi, ni dhahiri dhana ya KUJITEGEMEA ni KUJITAWALA na KUJITEGEMEA ni HESHIMA, haiko kwenye Sera za CHADEMA (Uk 21wa Ilani) na ACT-Wazalendo (Uk 30 wa Ilani), isipokuwa CCM (Uk 9 wa Ilani)

Naambatanisha Ilani za hivyo vyama IKIKUPENDEZA usome kurasa hizo kwa umakini.
 
Attachments

  • ILANI YA CCM 2020.pdf
    5.5 MB · Views: 4
  • ILANI YA CHADEMA 2020-2025.pdf
    5.1 MB · Views: 4
  • UNIFORUMTZ. COM_ACT.pdf
    5 MB · Views: 4
Nasikia Rais moi wa Kenya ndicho alichofanya aliwaambia wakenya walete pesa lakini wasitoe pesa nje na akawaambia hatawauliza wamezitoa wapi, naona na mwinyi kaamua kuuvaa ubeperi mzimamzia.
Kweli kabisa. Watu na wawekezaji wanazingatia sana usalama wa fedha zao kabla ya kuamua kuwekeza. Hawa watu wetu pamoja na kulipwa mishahara minono lakini hawajawai hata kuweka hili kwenye sheria zao. Wao wanaona ufahali kutangazwa kwenye vyombo vya Habari kuwa wametaifisha fedha na mali za watu
 
Tanzania kuwa nchi inayojitegemea kiuchumi pamoja na kuimarisha mahusiano ya kiuchumi na nchi nyingine.

Fafanua hapo ilani ya CCM ya kuimarisha uchumi na nchi zingine.

Katika ilani za uchumi za CDM na ACT, wao wamesisitiza uchumi wa jamii the public centred economy (soko huria) ambao ndiyo misingi ya kujitegemea kiuchumi.
 
Mkuu Lord denning, uchaguzi umeisha na Serikali iko kazini wewe unaendelea na lawama, kulalamika na kujashifu pasipo kuwa na hoja za nini kifanyike ili hayo madai yako yapate suluhisho la kudumu.

Yawezekana madai yako yakawa na ukweli lakini bahati mbaya ndani ya kambi ya vyama vya siasa hakuna kiongozi mwenye maono ya kutenda na kutatua kero hizo. Wengi wao, kama siyo wote, wana fikra za utegemezi na ndiyo maana lawama, kama hizo zako, huzungumzwa katika misingi ya kulalamika ndani na nje ya nchi. Tungetegemea matatizo ya ndani kijamii, kisiasa na kiuchumi, yangetatuliwa ndani kwa ndani kwa ushirikiano na Chama Tawala ili Serikali yake itekeleze kwa faida ya nchi na siyo chama.

Isitoshe nimepitia Ilani za Uchaguzi, za vyama vyote zilizopo, ni Ilani ya CCM tu yenye Sera zinazohusu uchumi wa kujitegemea. Natoa nukuu chache, kama ifuatavyo:

Chama Cha Mapinduzi kinatambua umuhimu wa kujenga uchumi wa kitaifa ili kuhakikisha kwamba Watanzania ndio wanufaika wakuu wa uchumi na maliasili za nchi na ndiyo wenye kauli juu ya namna uchumi unavyoendeshwa. Kwa muktadha huo CCM itaelekeza Serikali kuendelea na juhudi za kuifanya Tanzania kuwa nchi inayojitegemea kiuchumi pamoja na kuimarisha mahusiano ya kiuchumi na nchi nyingine. Juhudi maalum zitaelekezwa kuhakikisha rasilimali za asili za nchi hii, hasa ardhi, madini, gesi asilia, mafuta, maji na misitu zinanufaisha wananchi na Taifa kikamilifu.

Uchumi ni nyanja kuu katika maendeleo ya binadamu. Kwa kutambua hilo Chadema kimejipanga kuutafsiri ukuaji wa uchumi kwa vitendo ili kuwepo kwa mabadiliko chanya katika maisha ya kila Mtanzania. Hili litawezekana kwa kufumua mfumo wa sasa wa uchumi wa kijamaa ambao umeshindwa kuboresha hali ya maisha ya Watanzania, na kuanzisha mfumo wa soko jamii ambao unalenga kufungua fursa kwa kila mtu kutumia vipaji vyake katika kuzalisha na kumiliki mali. Mfumo huu mpya wa uchumi wa soko utaambatana na uanzishaji wa uchumi wa kidigitali ambao unazidi kushika kasi katika nyanja zote za uzalishaji na utoaji huduma katika dunia ya utandawazi.

Dhamira yetu (ACT-Wazalendo] ni kujenga Tanzania yenye uchumi wenye manufaa kwa wananchi na Serikali kwa ujumla; na siyo kukuza uchumi wa Serikali pekee au kusherehekea ukuaji wa takwimu za kiuchumi na ongezeko la mapato ya kikodi huku walipakodi (wananchi) wakiachwa katika ufukara, kukata tamaa, hali ngumu za maisha na mazingira magumu ya kutengeneza kipato.

Ukichambua nukuu hizo, kuhusu uchumi, ni dhahiri dhana ya KUJITEGEMEA ni KUJITAWALA na KUJITEGEMEA ni HESHIMA, haiko kwenye Sera za CHADEMA (Uk 21wa Ilani) na ACT-Wazalendo (Uk 30 wa Ilani), isipokuwa CCM (Uk 9 wa Ilani)

Naambatanisha Ilani za hivyo vyama IKIKUPENDEZA usome kurasa hizo kwa umakini.View attachment 1638077View attachment 1638078View attachment 1638079
Asante mwengeso kwa uchambuzi wako!!

Ila umekosea sana kusema kuwa hapa tunalalamika. Hakuna aliyelalamika hapa ila linalosemwa hapa ni kuwa ametokea mtu leo kutoka kwenye Chama chenu ambaye sasa amesema atafanya kama tulivyokuwa tunasema sisi ila mkawa mnatukebehi kwa ngebe nyingi.

Labda hujui ila Ngoja nikwambie, Tanzania haijawai kuwa na shida kwenye Ilani za vyama vyake. Tatizo la Tanzania ni sera kutungwa kwa utashi wa aliye madarakani na pia kutekelezwa kwa utashi wa huyo Kiongozi.

Siku zote sera zinatungwa na wataalamu tena baada ya kufanya utafiti wa kutosha.

Wewe kama mwana Ccm labda nikuulize, mlipokuwa mnataifisha pesa zilizokuwa zinakamatwa uwanja wa ndege , kwa sababu tu mtu haja declare mlikuwa mnataka kuachieve nini??? Hamkujua kuwa kuna madhara makubwa kiuchumi???

Mlipotunga sheria za kudhibiti miamala ya kibenki na kuwafanya watu kwa miamala ya kawaida tu kuiliizwa maswali lukuki hamkujua kuwa lina madhara kiuwekezaji???

Huko Ulaya mnafikiri wameendelea kwa pesa safi??? Pesa chafu ndo zinaenda kujenga chumi za huko na wanazifanya kuwa safi na kutengeneza ajira na kodi. Nyie watu wenu hawakujua haya??? Au mnafikiri maendeleo ni kuwa wakali na kutaifisha Mali za watu tu???
 
Tiss badala ya kuhangaika na kushauri kutatua kero na changamoto kama hizi,..wao wako busy kuisaidia ccm ishinde na kumpamba kayafa.
Tuna chombo cha hovyo sana.
Mie walikuja wawekezaji, wakafanya taratibu zote za awali na kumaliza Ila nilishangaa sana badae walinifuata wakaniambia tumeona kwa Tanzania hawawezi kuendelea kutokana na ukiritimba na sheria za ovyo. Wameamia Kenya na Rwanda ambapo wamesema sheria na taratibu za kiuwekezaji ziko vizuri
 
Hata mimi uwa sioni mantiki wka mtu anayeingiza pesa nchini kumsumbua, bora usumbue anayetoa. Leo kutokana na sheria ngumu za BOT paypal haipokea pesa Tanzania ukitaka fungua online shop kwa Ebay, au Shopify njia ya kulipwa watu wengi wanayoiamini ni paypal na paypal Tanzania haipokei pesa.

Imagine kenya wanapokea pesa mpaka kutoka Upwork kwa Mpesa Safaricom, Skrill ina withdraw kwa Mpesa, paypal pia lakini sisi hizi sheria unajiuliza mtu anapokea pesa analeta pesa ya kigeni sasa sheria zote za nini?
Anaweza akawa anafadhili ugaid,who knows?
 
Ndo mana tunasema kwa maendeleo ya kweli ya watanzania na Tanzania ni lazima Ccm ikae pembeni na hii nchi iongozwe na akili mpya yenye mawazo chanya na uelewa mpana wa dunia hii na sera bora na za uhakika
Jamani, acheni kuota ndoto zisizoshikika. Akili hiyo iko wapi? Akili ya kuwapeleka wake wakawe wabunge kesho mambo yakiwa magumu wanawageuka? Hebu onesha alternative basi Kama kweli ipo.

Halafu haya mambo ya kuambiwa nchi haiendelei, hivi ukilinganisha na muda gani na nchi gani?

Msije kuwa mnajisemea tu, wakati huna pa kufanyia ulinganisho. Muwe mnafanya ulinganisho basi na pia muainishe sababu za kidunia za nchi ya dunia ya tatu kuendelea kubaki huko na mziseme sababu binafsi za nchi moja moja zinazozifanya wabaki.

Tusiwe mabingwa wa maneno matupu, tuwe mabingwa wa maneno yenye mantiki
 
Back
Top Bottom