Tulipokuwa tunahangaika na uchaguzi wa serikali za mitaa, Masanja Mkandamizaji alitoa waraka huu kwa watu wote

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,171
5,905
20 hrs

Image may contain: 1 person
Carol Gisimoy
June 7, 2016
Ameandika Masanja Mkandamizaji

Akili yako Utajiri wako:

Laki tano, Mshahara wa Ma-Teller wa Benki hapa mjini Laki Tano, Bei ya Tecno Phantom mpya kabisa kwa kujishau Snapchat na Istagram Laki Tano, Bajeti ya Mafuta ya Subaru mwezi Mzima.

Laki Tano, Bajeti ya Heineken100 kwa wanywaji wa pombe. Hela fulani mbuzi tu ambayo wengi wanaona haina ishu.

Lakini, Laki Tano hii ina uwezo wa kukodi shamba Ekari 13 pale Kiteto au Mpwapwa na ikakutengenezea Million 15 baada ya Miezi mitatu kwa kulima Matikiti maji.

Laki Tano hii hii ina uwezo wa kununua simtamk la lita 5000 (ndoo 250 za lita 20) ambalo inaweza kutumika kusolve shida ya maji mtaani kwako kwa kuuza ndoo 1 Sh 500 na ukaingiza 125,000 kwa kila simtank unalouza.

Laki tano hii hii inaweza kulima Ekari 2 za Maharage pale Simanjiro na baada ya Miezi Minne ukavuna si chini ya Million 3 ambazo zitaexpand kilimo chako mara 6 zaidi ya Mwanzo na Kuexpand Kipato chako mara 6 zaidi ya Mkupuo wa kwanza!

Laki Tano hii ina uwezo wa kulima Matikiti Maji Ekari 2 na zikakupa si chini ya Milion 2 na nusu baada ya siku 90!

Shida ni: Kila mtu anataka akae mjini aonekane Samaki Samaki, aonekane muvi Mlimani City, apost akiwa Escape 1, apige Snapchat akiwa 777. Kila mtu anataka aonekane Mdarisalama. Yuko mjini

Mdada yupo radhi aishi mjini kwa kuuza mwili wake kuliko kwenda Ruaha Mbuyuni Kuinvest kulima Vitunguu. Ataonyesha saa ngapi crop top yake Mpya kutoka Yahya Boutique? Sistaduu alime vitunguu? Hapana, bora atafute danga la laki 2 akalale nalo!!

Big up kwa wadada wote wajanja walioinvest kwenye kilimo, kila jumamosi wakati wewe unaona sifa kwenda High Spirit Lounge, wadada wenzako wako Ruvu wamekodi mashamba wanalima mpunga, unashangaa huyu mdada anafanya nini kumbe mwenzio analima.

Kudos kwa wanaume wenzangu ambao wamegundua siri kwamba kuuza sura hakulipi na wameinvest shamba, kila weekend wanapotea kwenda kusimamia nyanya na pilipili Bagamoyo.

Utaendelea kuwashangaa wenzio wanatajirika na kudhani kila mtu anauza unga hapa mjini, kilimo ndio unga mpya.

Mnadhani Mkandamizaji amenunua ile BMW X6 kwa episode za Orijino Comedy? Thubutu, nenda Mbarari umkute amejaa matope akipalilia mpunga wake ndo utajua na wewe kwa nini unapanda bajaji mpaka.

Ni hayo tu kwa leo.
 
Kilimo cha matikiti maji na mpunga kimekuwa kilimo kinyonge mtu akipata kilaki chake anawaza kulima tikiti maji.

Nimeona hapo anasema unaweza kulima heka 2 za tikiti kwa laki 5.

Tuanze kama ifuatavyo:

Shamba kukodi heka mbili iwe laki moja kila heka 50000 kwa vile shamba ni mjomba wako.

Mbegu za kupanda kwenye hizo heka mbili utanunua kwa laki moja kwa vile wauza pembejeo na mbegu ni mashemeji wa mama yako.

Uandae shamba kwa laki moja maana wafanyakazi na trekta ni la mkweo.

Ununue mbolea na dawa kwa laki moja kwa vile wauzaji wa mbolea ni classmate wako.

Ubaki na laki moja ya kuendea shambani. Kiteto heka 13 unakodi kwa laki 5?

Kilimo hakiwezi kuwa uti wa mgongo kwa Tanzania kama unaweza kukilima Instagram.
 
Kupanga ni kuchagua kila mtu anaishi vile anavyoona yeye Inafaa, sio kila mtu ataishi kama wewe au kama yule, never.

Kila mtu ana plan zake na lifestyle yake kiujumla, maisha hayafanani kama vidole.

Like what u do and don't do what u like...!
 
Kilimo cha matikiti maji na mpunga kimekuwa kilimo kinyonge mtu akipata kilaki chake anawaza kulima tikiti maji.

Nimeona hapo anasema unaweza kulima heka 2 za tikiti kwa laki 5.

Tuanze kama ifuatavyo:

Shamba kukodi heka mbili iwe laki moja kila heka 50000 kwa vile shamba ni mjomba wako.

Mbegu za kupanda kwenye hizo heka mbili utanunua kwa laki moja kwa vile wauza pembejeo na mbegu ni mashemeji wa mama yako.

Uandae shamba kwa laki moja maana wafanyakazi na trekta ni la mkweo.

Ununue mbolea na dawa kwa laki moja kwa vile wauzaji wa mbolea ni classmate wako.

Ubaki na laki moja ya kuendea shambani.

Kilimo hakiwezi kuwa uti wa mgongo kwa Tanzania kama unaweza kukilima Instagram.
Masanja mwanawani njoo huku utee hoja yako
 
20 hrs ·



Image may contain: 1 person
Carol Gisimoy
June 7, 2016
Ameandika #MASANJAMKANDAMIZAJI
AKILI YAKO UTAJIRI WAKO:
Laki tano, Mshahara wa Ma-Teller wa Benki hapa mjini Laki Tano, Bei ya TECNO PHANTOM mpya kabisa kwa kujishau Snapchat na Istagram Laki Tano, Bajeti ya Mafuta ya SUBARU mwezi Mzima.... Laki Tano , Bajeti ya HEINEKEN 100 KWA wanywaji wa Pombe... HELA FLANI MBUZI TU ambayo wengi wanaona HAINA ISHU .
Lakini , Laki Tano hii ina uwezo wa kukodi shamba Ekari 13 pale Kiteto au Mpwapwa na ikakutengenezea Million 15 baada ya Miezi MITATU kwa kulima Matikiti maji.
Laki Tano hii hii ina uwezo wa kununua SIMTANK la lita 5000 ( ndoo 250 za lita 20) ambal inaweza kutumika kusolve shida ya maji mtaani kwako kwa kuuza ndoo 1 Sh 500 na ukaingiza 125,000 kwa kila SIMTANK unalouza.
Laki tano hii hii inaweza kulima Ekari 2 za Maharage pale Simanjiro na baada ya Miezi Minne ukavuna si chini ya Million 3 ambazo zitaexpand kilimo chako MARA 6 zaidi ya Mwanzo na Kuexpand Kipato chako mara 6 zaidi ya Mkupuo wa kwanza!
Laki Tano hii ina uwezo wa kulima Matikiti Maji Ekari 2 na zikakupa si chini ya Milion 2 na nusu baada ya SIKU 90!
SHIDA NI: Kila mtu anataka akae mjini AONEKANE SAMAKI SAMAKI, aonekane Muvi Mlimani City, Apost akiwa Escape 1, Apige Snapchat akiwa 777 ... Kila mtu anataka aonekane MDARISALAMA... Yuko mjini
MDADA yupo radhi aishi mjini kwa kuuza mwili wake kuliko kwenda Ruaha Mbuyuni Kuinvest kulima Vitunguu... Ataonyesha saa ngapi CROP TOP yake Mpya kutoka YAHYA BOUTIQUE? Sistaduu alime vitunguu?? Hapana, bora atafute Danga la Laki 2 akalale nalo!!
Big Up kwa wadada wote wajanja WALIOINVEST KWENYE KILIMO., kila Jumamosi wakati wewe unaona sifa kwenda HIGH SPIRIT LOUNGE Wadada wenzako wako RUVU wamekodi mashamba wanalima mpunga, unashangaa Huyu mdada anafanya nini kumbe mwenzio analima.
KUDOS kwa wanaume wenzangu ambao wamegundua siri kwamba kuuza Sura hakulipi ma wameinvest Shamba, kila weekend wanapotea kwenda kusimamia nyanya na pilipili Bagamoyo.
Utaendelea kuwashangaa wenzio wanatajirika na kudhani kila mtu anauza UNGA hapa mjini, Kilimo ndio unga mpya... nnadhani mkandamizaji amenuunua ile BMW X6 kwa episode za ORIJINO COMEDY? Thubutu, nenda MBARARI umkute amejaa Matope akipalilia Mpunga wake ndo utajua na wewe kwa nini unapanda Bajaji mpaka
NI HAYO TU KWA LEO.
Usipokuwa makini utapigwa na ukiwa na bahati kilimo kitakutoa, ila usipoangalia pia kitakuingizia umaskini
 
Shida ya binaadamu wengi wakishapata utajiri hua wanajiona wao ndio wana akili sanaa, wanawaona maskini wote ni mafala wasiopenda kujishughulisha.
Lusekelo alifikia mpaka kutuaminisha ya kwamba kufa masikini ni ufala.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom